Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  19 Dhu al-Hijjah 1441 Na: 1441/86
M.  Jumapili, 09 Agosti 2020

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ikiazimia Kukwepa Hatua za Kivitendo za Kuikomboa Kashmir, Serikali ya Bajwa-Imran Yawasaliti Waislamu Kupitia Taratibu za Kiishara

Sera ya kuisalimisha Kashmir ilianzishwa na Musharraf kwa maagizo ya Amerika. Sasa, ili kuikomboa Kashmir Pakistan haina chaguo jengine, isipokuwa kutumia nguvu za kijeshi, baada ya serikali ya Modi kufutilia mbali hadhi spesheli ya Kashmir na kuiunganisha kwa lazima na Muungano wa India, ambao huu ni msitari wa mwisho mwekundu kuvukwa na India. Hata watoto wanajua kwamba Raja Dahir wa leo anaweza tu kushindwa kupitia kuwahamasisha kina Muhammad Bin Qasim wa majeshi ya Pakistan. Lakini, unapofika wakati wa kupiga ngoma za vita, serikali ya Bajwa-Imran hupiga ngoma za burudani na udanganyifu. Huku Waislamu wakiyatazama kwa matarajio Makao Makuu ya Jeshi (GHQ), Mshauri wa Usalama wa Taifa, Moeed Yousuf, ametangaza kampeni ya kipuzi ya kutekeleza kimya cha dakika moja. Ikiwa ni wakati wa kupiga ving'ora nchi nzima ili kujitayarisha kwa vita, Imran Khan amejishughulisha na kutuma jumbe za Twitter ndani ya vyumba vyake vilivyo na viyoyozi. 

Sasa, Waziri wa Kigeni, Shah Mehmood Qureshi, anajaribu kutoa taswira kwamba endapo mkutano wa mawaziri wa kigeni wa OIC utaitishwa, meza huenda zikageuzwa dhidi ya Dola ya Kibaniani. Anaendelea kudai kwamba endapo mkutano wa OIC hautafanyika, basi Imran Khan ataitisha mkutano wa nchi za Kiislamu ili kuisaidia Kashmir. Kiuhalisia, hawezi kuwahadaa Waislamu wa Pakistan, kwani wanajua kuwa watawala walioko sasa ni vibaraka tu wa watawala wa Magharibi, walio mbali na mifano ya Salahuddin Ayubi, Alauddin Khilji au Harun ul-Rasheed. OIC ni mkusanyiko wa mizoga, ambayo mikutano yao ni kuzima hasira za Ummah kwa kuchafuliwa matukufu yake na hivyo natija yake kamwe haijawahi kupelekea ukombozi wa ardhi yoyote iliyokaliwa. Zaidi ya hayo, watawala walioko sasa ima wanawauwa Waislamu kwa njia ya moja kwa moja au wanawaruhusu makafiri kufanya hivyo, pasi na upinzani wowote. Ama kuhusu kulifanya swala hili kuwa la kimataifa, inazipa njia dola za kikoloni kuingilia kati mambo ya Ummah, kuongeza madhara juu yake na kuupokonya haki zake.

Watawalaa madhalimu na wanyanyasaji wanachukua tahadhari kwa nguvu za kijeshi, sio taratibu za kiishara, namna zitakavyokuwa nyingi au tofauti tofauti. Hatujatengeneza makombora ya Shaheen, Abdali, Ghouri na Baber kama mapambo ya gwaride. Hatujakazanisha mikanda yetu ili kutoa mahitaji yote yanayo wezekana kwa majeshi yetu, ili kuwasikiza watawala kuwa "vita sio chaguo," wakati ikiwa ndio chaguo pekee lililo salia. Ikiwa watawala hawa ni waoga, wasioweza kuona mbali zaidi ya maslahi yao ya kibinafsi, basi hawana haki ya kutawala juu ya Ummah jasiri na majeshi yake. Watawala hawa ni lazima wajiuzulu, kwani hatuna uhaba wa watoto wa Khalid bin Walid (ra), waliojaa hamu ya shahada au mafanikio, wanaotamani kuchukua tena Kashmir na kutimiza amri za Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw). Mbinu hadaifu za kudanganya za serikali ya Bajwa-Imran zimefichuka. Imedhaminiwa na mabwana wake wakoloni kuyatia minyororo majeshi ya Pakistan, ili Modi aweze kukabiliana na China na mwamko wa Kiislamu, bila ya hofu yoyote ya majeshi ya Pakistan. Uunganishaji Ummah na majeshi yake kamwe hautapatikana kupitia OIC. Umoja utapatikana kupitia Khilafah kwa Njia ya Utume pekee, kwani ndiyo itakayo unganisha ardhi zote za Waislamu, rasilimali na majeshi yao chini ya bendera moja, ili wawe nguvu kuu. Na kisha Khalifah wa Waislamu atayahamasisha majeshi kuikomboa Kashmir, ili kufikia radhi za Mwenyezi Mungu (swt)

[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]

“Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Surah ar-Rum 30:4-5].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu