Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
H. 21 Dhu al-Hijjah 1441 | Na: 1441 / 87 |
M. Jumanne, 11 Agosti 2020 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Muundo Mpya ya Afghan Uliojengwa juu ya Fikra ya Kisiasa ya Kimagharibi Utakuwa ni Ushindi kwa Amerika, Sio kwa Waislamu, Ilhali, Serikali ya Bajwa-Imran Imeshughulishwa na Kusahilisha Mpango Huu wa Wakoloni
Waislamu na watahadhari juu ya hatua za sasa katika njia ya mpango wa Amerika wa Muundo mpya wa Afghan. Mnamo 7 Agosti 2020, Waziri wa Kigeni wa Amerika, Mike Pompeo, aliandika katika Twitter, "Mwito wenye tija wa Waziri wa Kigeni wa Pakistan, Shah Mahmood Qureshi, leo kuhusu kuendelea kushirikiana juu ya amani ya Afghan na umuhimu wa kusaidia utulivu wa eneo. Natazamia kuendeleza malengo yetu shirika na kuongeza ushirika." Lakini, wale walio na utambuzi wa kisiasa hawawezi kudanganywa na balagha tupu ya "amani ya Afghan" na "utulivu wa eneo." Kikombe cha fedha na dhahabu cha balagha ya Pompeo kina sumu kali ya mpango wa wakoloni wa muundo mpya wa Afghan, uliobuniwa juu ya fikra ya kisiasa ya Kimagharibi. Katika ulimwengu wa Kiislamu, maslahi makubwa zaidi ya kistratejia ya Magharibi ni muundo wa kisiasa uliojengwa juu ya ubwana wa wanadamu, ambao unajumuisha fikra ya mgawanyiko wa dola za kitaifa, sheria ya kimatata iliojengwa juu ya ubwana wa wanadamu ima kupitia demokrasia au udikteta, mpangilio huru wa kijamii uliojengwa juu ya uhuru fisidifu wa Kimagharibi, nidhamu ya unyonyaji ya kiuchumi ya kirasilimali, kanuni dhalimu za mahakama za Kimagharibi na sera ya kigeni inayo chechemaa, inayo duru ndani yake maslahi ya Kimagharibi, yanayo chipuza kutokana na maadili ya Westphalia.
Ili kuupa umaarufu muundo wake wa kisiasa ndani ya Ummah wa Kiislamu, Magharibi iko tayari hata kuzitumia istilahi za Kiislamu. Kihistoria, ili kuyapata maslahi haya ya kistratejia, Waingereza na Wafaransa polepole waliyaondoa majeshi yao kutoka katika ulimwengu wa Kiislamu, katika miongo ya arubaini na hamsini ya karne iliyopita, wakifaulu kupandikiza mfumo wao katika ulimwengu wa Kiislamu. Kuendelea kwa mfumo wa Kimagharibi katika ulimwengu wa Kiislamu hakujawafanya kuwa huru katika mambo yao, baada ya miaka satini au sabiini ya uhuru. Leo, Amerika inatumia mbinu ile ile ya kikoloni nchini Afghanistan. Amerika inahakikisha kuwa upinzani wa Afghan unakubali kugawanya mamlaka na vibaraka wa Amerika nchini Afghanistan na muundo wa kisiasa wa Kimagharibi kupitia kulegeza msimamo wa ufafanuzi wa Dini ya Uislamu. Ili kuharakisha mpango wa Amerika, watawala wa Pakistan wanatekeleza sera ya "karoti na kijiti" dhidi ya upinzani wa Afghan, ili kuwalazimisha kukaa katika meza ya majadiliano. Mara kwa mara, uongozi wa sasa wa Pakistan, akiwemo msemaji wa ISPR, wamepata sifa kwa ajili ya dori hii ya aibu.
Hakika, muundo mpya wa Afghan unabeba hatari kubwa kwa Waislamu. Iweje maadui wa Uislamu wakaribishe kuachiliwa huru "wanamgambo hatari 5000" wa upinzani wa Afghan? Iweje wale wanaojibu ulinganizi wa utabikishaji Uislamu kwa risasi, droni na ndege za kivita aina ya B-52, wanahamu sana na "mazungumzo ya kindani ya Afghan" na makubaliano ya kusitisha vita? Kugawanya mamlaka na vibaraka wa Amerika ni konde la mauti kwa utawala wa Shariah. Inapeana ushindi kwa Amerika katika meza za mazungumzo, ambao hangeweza kuupata kati viwanja vya vita. Bila ya kujali nia nzuri, inajumuisha usaliti kwa damu ya maelfu ya mashahidi, waliomwaga damu zao wakipambana na uvamizi wa kigeni katika miongo minne iliyopita. Amerika inataka kuinasa Afghanistan ndani ya wavu wa mfumo wake wa kimataifa, ili iweze kutaga mayai ya jeshi lake la kibinafsi na jeshi ndani ya tumbo lake, kwa jina la usaidizi wa kiusalama, na kula rasilimali zake nyingi za madini, kwa jina la uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni.
Ni wajibu kwa Waislamu wa Pakistan na Afghanistan kukataa ule unaoitwa "mpango wa amani wa Afghanistan." Vilevile ni wajibu kwa majeshi na ujasusi wa Pakistan kutibua njama hii ya wakoloni, kupitia kutoa Nusrah kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume nchini Pakistan. Hapo, ndipo Pakistan na Afghanistan zitakuwa umbile moja chini ya Uislamu, baada ya kuwa na mafungamano ya karne nyingi ya Kiislamu, kithaqafa na kihistoria. Na kisha Khilafah itaweza kuupa nguvu Ummah huu kwa jumla, kupitia kusonga mbele na kuziunganisha ardhi za Waislamu za Mashariki ya Kati na Asia ya Kati na zaidi. Hili pekee litatoa njia ya ukombozi wa Kashmir na Palestina, ikitupa mafanikio ya hapa duniani na kesho Akhera. Mwenyezi Mungu (swt) ametangaza,
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَنصُرُوا اللَّهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ]
“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [Muhammad 47:7]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Pakistan |
Address & Website Tel: https://bit.ly/3hNz70q |