Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  8 Jumada II 1443 Na: 1443 / 33
M.  Jumanne, 11 Januari 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Madeni ya Riba Yanayotolewa Kwetu na Dola za Wakoloni na Vyombo vyao Huhakikisha tu Uchumi Wetu Unazama Katika Madeni, Sio Maendeleo

 (Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 9 Januari 2022, Rais wa Sri Lanka, Gotabaya Rajapaksa, wakati wa mkutano na Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi huko Colombo, aliomba kupunguzwa kwa ulipaji wa deni kwa China. Katika muongo uliopita China imeikopesha Sri Lanka zaidi ya dolari bilioni 5 kwa ajili ya barabara kuu, bandari, uwanja wa ndege na kiwanda cha kuzalisha nishati ya makaa ya mawe, kama sehemu ya Mpango wa China wa Belt and Road Initiative (BRI). Hata hivyo, sasa taifa hilo la kisiwa kwa sasa liko katikati ya mgogoro wa ubadilishanaji wa fedha za kigeni, na kuliweka katika ukingo wa kushindwa kulipa.

Sawa na watawala wa Pakistan, watawala wa Sri Lanka waliiuza ndoto ya mito ya maziwa na asali kwa watu wao, ili kuwa sehemu ya Mpango wa China wa Belt and Road Initiative (BRI), ambao sasa umethibitishwa kuwa jinamizi tu lilojaa madeni. Watawala wa Pakistan walidai kwamba wakati Marekani, Ulaya na zana zao za kikoloni, IMF na Benki ya Dunia, zikitoa mikopo kwa masharti angamivu, mikopo kutoka China haina masharti haya na hivyo uchumi wetu utafufuka. Watawala wa Pakistan hata waliita CPEC, sehemu ya Mpango wa Belt and Road Initiative (BRI) nchini Pakistan, "mbadilishi wa mchezo." Hata hivyo, hali ya Pakistan leo si tofauti sana na ile ya Sri Lanka. Kulingana na nyaraka zilizotolewa na wizara ya fedha ya Pakistan, deni la nje la Pakistan lilifikia dolari bilioni 44.35 mwezi Juni 2013. Hata hivyo, kufikia Aprili 2021, deni hili la nje lilikuwa limepanda hadi dolari bilioni 90.12, huku Pakistan ikidaiwa dolari bilioni 24.7 za deni lake la nje kwa China. Sehemu kubwa ya mapato ya kodi ya Pakistan sasa inatumika kwa malipo ya riba.

Kwa hakika, chini ya mfumo wa sasa wa kirasilimali wa kiulimwengu, mikopo inatolewa na mataifa makubwa ya kikoloni kwa wengine, ili kuwafanya watumwa na kuwanyonya kiuchumi. Hali ya Sri Lanka na Pakistan inathibitisha kwamba China ni sehemu ya mfumo wa sasa wa kirasilimali wa kiulimwengu, unaoongozwa na Marekani. Kwa hiyo, katika mfumo wa sasa wa kirasilimali wa kiulimwengu, iwe fedha zitakopwa kutoka China, Marekani, IMF, ADB au nchi au taasisi nyingine yoyote, nchi zilizotawaliwa na ukoloni kiuchumi zitazama tu ndani ya madeni ya riba. Mfumo wa kiuchumi wa kirasilimali hauwezi kamwe kutoa ustawi kwa ulimwengu, kwani unahakikisha tu ukandamizaji wa kiuchumi na mrundiko wa mali mikononi mwa dola kuu za kikoloni.

Ulimwengu unahitaji mfumo mpya wa kiuchumi wa kiulimwengu ambao hutolewa na Uislamu pekee na unaweza kutolewa tu na dola ya Waislamu, Khilafah. Mfumo wa kiuchumi wa kiulimwengu wa Uislamu unakataa mikopo yenye riba, unatumia dhahabu na fedha kama sarafu na unaitumia sarafu hii pekee katika biashara ya kimataifa na miamala ya pande zote mbili. Ni Khilafah hii pekee ndiyo itakayomaliza utawala wa dolari, kukataa taasisi za kikoloni kama vile IMF na Benki ya Dunia na kutangaza viwanda vya mafuta, gesi na umeme kuwa mali ya umma. Khilafah pekee ndiyo inayoweza kutekeleza mfumo huu wa kimapinduzi wa kiuchumi duniani, huku Mwenyezi Mungu (swt) ameyatajirisha maeneo ya Waislamu. Ulimwengu wa Kiislamu una maliasili nyingi, huku njia kuu za baharini, nchi kavu na anga kwa biashara ya kimataifa hupitia ardhi zake. Zaidi ya yote, Umma wa Kiislamu una hazina ya Iman, ambayo kwayo Waislamu wanaweza kuuchana mfumo wa sasa wa kiuchumi wa kirasilimali wa kinyonyaji. Enyi Waislamu wa Pakistan! Simameni ili kuung'oa mfumo dhalimu wa kiuchumi wa kirasilimali, kuhakikisha utabikishwaji wa Dini pekee mbele ya Mwenyezi Mungu (swt), al-Islam, kwa kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume. Mwenyezi Mungu (swt) amesema:

(وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ)

 “Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao.” [Surah An-Noor 24:55].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu