Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
H. 5 Dhu al-Hijjah 1443 | Na: 1443 / 75 |
M. Jumatatu, 04 Julai 2022 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Meja (Mstaafu) Khalid Butt, Mwenyezi Mungu (swt) Amrehemu, ni Mfano kwa Maafisa Wote wa Jeshi wa Msimamo Imara Unaohitajika katika Kumtumikia Mwenyezi Mungu (swt)
[إِنَّا ِلِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]
“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Surah Al-Baqarah 2:156]
(Imetafsiriwa)
Mwenyezi Mungu (swt) amfufue Meja Khalid Butt akiwa hana dhambi, kwa maradhi makali aliyoyavumilia kwa subira ya hali ya juu. Mwenyezi Mungu (swt) aipe Subira Njema familia yake kwa msiba huu mkubwa. Tunaomba kizazi chake chema kiwe chanzo cha malipo tele kwa ajili yake, kupitia malezi yake bora kwao na usaidizi wa kudumu, usio na kikomo. Hakika, tunakumbuka mapenzi makubwa ya Meja Khalid kwa Dini hii ya Haki, huzuni juu ya hali ya kusikitisha ya Ummah wa Kiislamu na kujali sana Dawah kwa ajili ya utabikishaji Dini hii.
Tunakumbuka juhudi zisizo choka za Meja Khalid kuhakikisha kuachiliwa huru kwa Naveed Butt, shemeji yake na msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Pakistan. Hakika, tunakumbuka msimamo thabiti wa Meja Khalid dhidi ya madhalimu, ukivumilia kisasi chao cha kikatili kwa subira, wakati wa ugonjwa na uzee. Tunakumbuka jinsi yeye binafsi alivyofikisha barua kutoka kwa Hizb ut Tahrir kwenda kwa dhalimu Musharraf, iliyomuamrisha kuamrisha mema na kukataza maovu, huku akimtaka aukabidhi Ummah mamlaka aliyoyanyakua kutoka kwa Waislamu, ili Khilafah kwa Njia ya Utume isimamishwe, bila ya kuchelewa tena kwa gharama kubwa.
Ewe Mwenyezi Mungu! Nyoyo zetu zimejaa huzuni na macho yetu yamejaa machozi kwa mapenzi yetu kwa Meja Khalid. Kwa hiyo, tunakuomba, Mwenyezi Mungu (swt), katika siku hizi zilizobarikiwa za Dhul Hijjah, umkirimu Meja Khalid pamoja na kundi la Manabii (as), mashahidi, wakweli na wema, katika makaazi ya milele yenye neema. Mwenyezi Mungu (swt) amesema:
[مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلًا]
“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Surah Al Ahzab 33:23].
Enyi Maafisa wa Vikosi vya jeshi la Pakistan! Ndugu yenu mwanajeshi na mzee wa kuheshimika, Meja Khalid, amefariki kwenda kwenye rehema za Mola wake (swt), baada ya kumtumikia vyema Mwenyezi Mungu (swt). Misimamo yake thabiti, katika uzee na ugonjwa wake, ni ukumbusho mkubwa kwenu nyote wa wajibu wenu leo. Mcheni Mwenyezi Mungu (swt) kama anavyopaswa kuogopwa na mtumikieni Mwenyezi Mungu (swt) kama anavyopaswa kutumikiwa. Mtumikieni Mwenyezi Mungu (swt) kwa nguvu kamili, katika ujana wenu na afya zenu, ili mpate kukutana na Mwenyezi Mungu (swt) kwa hoja kwa ajili yenu na sio dhidi yenu. Hali hii mbaya inataka misimamo imara wa kukatikiwa kutoka kwa kila mmoja wenu, ambapo muhamasishe nguvu zenu katika kuwanusuru Waislamu na Dini ya Mwenyezi Mungu (swt). Wang'oeni madhalimu na mutoe Nussrah kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Pakistan |
Address & Website Tel: https://bit.ly/3hNz70q |