Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  23 Dhu al-Hijjah 1443 Na: 1443 / 77
M.  Ijumaa, 22 Julai 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kuanguka Kusiko na Kikomo kwa Rupia ya Pakistan ni Thibitisho Kubwa la Haja Kuu ya Sarafu ya Dhahabu na Fedha ya Uislamu

(Imetafsiriwa)

Mawaziri mashuhuri wa muundo wa sasa wa raia wa Pakistan, Ahsan Iqbal, Khurram Dastagir na Miftah Ismail, wanadai kwa uwongo kwamba hakuna mgogoro wa dolari wala hatari ya kushindwa kulipa madeni. Jaribio lao la kuyapa imani masoko ni juhudi iliyopotea bure, ambayo, kwa uchache, haifaidi mtu yeyote, wakiwemo wao wenyewe. Kwa kweli, Rupia imeanguka hadi Rs. 226 kwa dolari, ilhali inaning’inia katika alama ya Rs. 241, kwa madhumuni ya Barua za Mikopo katika biashara ya kimataifa.

Kwa hivyo, tangu mpangilio wa kiraia wa PDM ulipowekwa madarakani, Rupia imepoteza kati ya Rupia 43 na 44 dhidi ya dolari ya Marekani. Rupia inayodhoofika kwa kasi imesababisha dhoruba ya mfumko wa bei, na kuchangia kupanda kwa bei ya mafuta, umeme na mambo mengine muhimu. Miongoni mwa matokeo mengine, huku ikizama kwa kasi, Pakistan sasa inakabiliwa na kuhama kwa haraka kwa wataalamu, huku talanta yake bora zaidi ya ndani ikipanda meli, kutokana na kukata tamaa kabisa. Sarafu yoyote ya karatasi isiyo na thamani ya kidhati anatarajiwa kushuka thamani kadri muda unavyo kwenda, kwani inaungwa mkono tu na imani katika serikali pekee.

Kwa hivyo, kwa nini Rupia iwe tofauti pekee kwa kanuni hii, ambayo imeimarishwa barabara kote ulimwenguni? Rupia kwa kweli haina thamani zaidi kuliko karatasi ya usalama iliyochapishwa juu yake, ambayo hununuliwa kwa dolari mia chache tu kwa tani, ilhali thamani yake ni nyembamba, hadi mamilioni na mabilioni ya Rupia. Huku imani, katika dola iliyofeli ya Pakistan na sarafu inayoitoa, ikianguka, watu sasa wanabadilisha mapato yao ya Rupia kuwa dolari kwa haraka, kwa nia ya kuhifadhi thamani ya akiba zao walizochuma kwa bidii, lakini wanazidisha mgogoro wa Rupia. Hakika, ni dhulma kwa sarafu kuanguka kote duniani, kwa sababu Hifadhi ya Majimbo ya Serikali ya Marekani, jimbo moja tu ambalo liko mbali na bahari, limepandisha viwango vya riba ili kuimarisha dolari. Ni dhulma kubwa zaidi kwamba vibaraka wa Marekani walio madarakani nchini Pakistani bado wanasisitiza kuifunga minyororo Rupia kwenye dolari, huku hata bila kuzingatia njia mbadala ya mfumo katili wa kiuchumi wa Kimagharibi.

Sarafu ya dhahabu na fedha ya Uislamu imeegemezwa juu ya nyenzo zenye thamani halisi ya asili, sio juu ya usemi tu wa serikali au, hata, domo tupu, maombi na kejeli za wamiliki wake wa afisi walioingiwa na hofu. Kwa hivyo sarafu ya Uislamu imejikita katika nyenzo za mali halisi, dhahabu na fedha, na hivyo inabakia na utulivu katika thamani yake, bila kujali imani katika dola inayoitoa, au hata uwepo wa daima wa dola hiyo duniani. Sehemu kubwa ya dhahabu na fedha iliyochimbwa na kusafishwa hadi sasa, juu ya eneo kubwa la historia ya wanadamu, ingali imehifadhiwa hadi leo. Kuhusu uundaji wa sarafu mpya, si kwa kubofya tu swichi kwenye mashini ya uchapishaji, bali kupitia mchakato mgumu wa uchimbaji madini na usafishaji, dhahabu pamoja na fedha. Kwa hivyo, maumbile ya sarafu ya dhahabu na fedha huweka nidhamu katika matumizi na ukusanyaji wa mapato, hivyo kuzuia serikali kutokana na uchapishaji wa kivivu wa sarafu zaidi ili kufadhili mapungufu, huku ikimaliza kabisa sababu ya mfumko wa bei uliokithiri ambao umeisumbua dunia kwa miongo kadhaa. Kutabanniwa kwa viwango viwili sarafu vya Uislamu kutamaliza utawala wa kimataifa wa dolari, kuleta utulivu wa bei na kumaliza mgogoro mkubwa uliopo sasa.

Ni Khilafa pekee ndiyo itakayokuwa na dhamira ya lazima kwa Uislamu, uhuru wa utashi wa kisiasa na rasilimali nyingi za pamoja za Ulimwengu mpana wa Kiislamu, ili kuifanya tabanni ya sarafu ya dhahabu na fedha, iwe ya kivitendo pamoja na kuwa rahisi, huku ikimtegemea Mwenyezi Mungu (swt), Ambaye Peke Yake Anatawala Utawala Wake kikamilifu. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

 (وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لَا يَحْتَسِبُ وَمَنْ يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّهِ فَهُوَ حَسْبُهُ إِنَّ اللَّهَ بَالِغُ أَمْرِهِ قَدْ جَعَلَ اللَّهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْرًا)

“Na humruzuku kwa jiha asiyo tazamia. Na anaye mtegemea Mwenyezi Mungu Yeye humtosha. Hakika Mwenyezi Mungu anatimiza amri yake. Mwenyezi Mungu kajaalia kila kitu na kipimo chake.” [Surah At-Talaq 65:3].

Enyi Maafisa wa Jeshi la Pakistan! Je, mumeona inatosha sasa kwenu kuchukua hatua?! Songeni, wang'oeni wasaidizi waajiriwa wa IMF na muipe Nussrah yenu Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume. Hapo ndipo Waislamu watakapochukua mambo yao mikononi mwao, huku wakichukua nafasi yao inayostahiki kama uongozi wa kiulimwengu kwa ajili ya wanadamu wote, wakiikomboa dunia kutokana na Raj mkoloni dhalimu.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu