Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  5 Muharram 1444 Na: 1444 / 02
M.  Jumatano, 03 Agosti 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
 Ili Kuongeza Matarajio ya Uchaguzi wa Rais wa Amerika wa Katikati ya Muhula, Uongozi wa Kijeshi wa Pakistan Wahatarisha Anga na Usalama Wetu

(Imetafsiriwa)

Uongozi wa kijeshi wa Pakistan umevuka mipaka yote ili kuthibitisha manufaa yake kwa bwana wake, Marekani. Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari PR-64/2022-ISPR, afisi ya habari ya jeshi la Pakistan ilithibitisha maongezi ya simu ya kina mnamo 29 Julai 2022, kati ya Jenerali Bajwa na Jenerali wa Marekani, Michael Kurrila, kamanda wa USCENTCOM. Kwa hakika, ni uongozi wa kijeshi wa Pakistan ndio unaoruhusu droni za Marekani kufika Kabul kwa urahisi, kutoka makao makuu ya mbele ya USCENTCOM katika Kambi ya Anga ya Al-Udeid nchini Qatar, kwa njia ya ugavi wa anga kupitia anga ya Pakistan, ambayo waendeshaji wa droni hizo za Marekani wanaiita “Boulevard. .” Ni baada tu ya ushirikiano wa karibu na uongozi wa kijeshi wa Pakistan, ambapo Marekani iliweza kuzindua shambulizi la droni mnamo 31 Julai 2022, ambalo lilipiga nyumba moja jijini Kabul, na kumuua shahidi mujahid mwenye ikhlasi, Ayman Az-Zawahari, Mwenyezi Mungu (swt) amfufue miongoni mwa mashahidi.

Eni Waislamu wa Pakistan! Huu, basi, ndio uongozi wa sasa wa kijeshi wa Pakistan. Umeanzisha mgogoro wa muda mrefu wa kisiasa, ukidhibiti jukwaa la kisiasa na idara ya mahakama, hata baada ya kuyataka majeshi yetu kudumisha umbali wao kutokana na siasa. Umelemazwa na machafuko ya ndani, Pakistan imeachwa wazi kwa uharibifu wa kiuchumi mikononi mwa IMF, pamoja na vitisho vinavyoongezeka dhidi ya usalama wetu wa ndani kutoka India, huku Modi akiimarisha mshiko wake wa kikatili kwa Kashmir Iliyokaliwa kimabavu, bila kusumbuliwa. Kwa kupuuza kabisa droni hizo za Marekani zinazopeleleza mali nyeti za kijeshi chini ya ukanda wa anga wa "Boulevard", uongozi wa kijeshi wa Pakistan umewezesha shambulizi muhimu la anga la Rais wa Marekani, Joe Biden, ili kuongeza hadhi yake, huku akikabiliwa na uchaguzi mgumu wa katikati ya muhula. Na hivyo basi uongozi wa kijeshi wa Pakistan umeegemea upande wa wakoloni, dhidi yetu na majeshi yetu.

Ni juu yetu sote, enyi Waislamu, kufanya kazi kwa ajili ya kumuondoa Raj wa Kiamerika nchini Pakistan. Ni Khilafah kwa Njia ya Utume, pekee, ndiyo itakayokomesha muungano, mafungamano, ushirikiano na uratibu na adui mkubwa wa Waislamu, Marekani. Ni Khilafah peke yake ndiyo itakayofanya hivyo, kwa sababu ni Khilafah pekee ndiyo inayojifunga na kamba ya Mwenyezi Mungu (swt), inayohukumu kwa yale yote aliyoyateremsha Yeye (swt). Mwenyezi Mungu (swt) amesema:

(الَّذِينَ يَتَّخِذُونَ الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِ الْمُؤْمِنِينَ أَيَبْتَغُونَ عِندَهُمُ الْعِزَّةَ فَإِنَّ الْعِزَّةَ لِلَّهِ جَمِيعًا)

“Wale ambao huwafanya makafiri kuwa ndio marafiki badala ya Waumini. Je! Wanataka wapate kwao utukufu? Basi hakika utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu.” [Surah An-Nisa’a 4:139]. Basi wale wanaompenda Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw) na wapaze sauti zao kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah Rashida nchini Pakistan!

Enyi Maafisa wa Jeshi la Pakistan! Kuanzia wakati wa Jenerali Musharraf hadi leo hii, je, hamjaona khiyana ya kutosha kutoka kwa uongozi wenu, wa kuwafanyeni kusukuma mabadiliko sasa? Je, humkuona usaliti wa kutosha wakati wa Jenerali Kiyani, wakati uongozi wa kijeshi ulipofungua anga zetu kwa ajili ya mashambulizi ya Marekani dhidi ya Abbotabad, wa nyinyi kuhamasika wakati huo? Je, bado humjaona usaliti wa kutosha kutoka kwa uongozi wa sasa wa kijeshi, ili muweze kuhamasika sasa, mara moja? Mcheni Mwenyezi Mungu (swt) peke yake na musoge sasa, fanyeni biashara ya nafsi zenu kwa furaha ya milele ya Jannah katika Akhera. Songeni sasa na mutoe Nussrah yenu kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume. Songeni sasa na muhakikishe kuwa watu wenu wema wanatawaliwa na Quran Tukufu na Sunnah za Mtume. Songeni sasa ili watu wenu wawe na watawala wanaowapenda, wakiunganisha mchana wao na usiku wao katika usimamizi wenye kujali. Songeni sasa ili hatimaye muwe na uongozi wa kijeshi unaokutangulieni kwenye uwanja wa vita, katika ushindi pamoja na kifo cha kishahidi. Hizb ut Tahrir inakutakeni musonge nayo sasa, kwa hiyo, kwa ajili ya radhi za Mwenyezi Mungu (swt), songeni!

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu