Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  16 Rajab 1444 Na: HTS 1444 / 31
M.  Jumanne, 07 Februari 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan Wakutana na Profesa Ali Baldo, Mshauri wa Tiba ya Akili na Uraibu wa Mihadarati
(Imetafsiriwa)

Ndani ya wigo  wa kampeni inayofanywa na Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Sudan, kupambana na mihadarati, ujumbe ulikutana leo, Jumanne 07/02/2023, ukiongozwa na Ustadh Ibrahim Othman (Abu Khalil) - msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Sudan, akiandama na Ustadh Ahmed Abkar, mwanasheria - mjumbe wa Baraza la Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan, Ustadh Abdullah Hussein - Mratibu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir Wilaya ya Sudan, na Dkt. Muhammad Abdul Rahman – Mwanachama wa Hizb ut Tahrir. Ujumbe ulikutana na Profesa Ali Baldo, mshauri wa tiba ya akili na uraibu katika kliniki yake ya kibinafsi jijini Omdurman, ambaye aliukaribisha ujumbe huu.

Mazungumzo yalianza kwa mkuu wa ujumbe huo Ustadh Abu Khalil kuwatambulisha wajumbe wa ujumbe huo, kisha akaeleza kuwa lengo la mkutano huo linakuja ndani ya kampeni ambayo hizb inaifanya ya kupambana na dawa za kulevya hali inayoashiria kuwa serikali haiko makini kuhusu kupigana na madawa ya kulevya, bali inampokea waziri wa mambo ya nje wa umbile la Kiyahudi; kijidola hiki kidogo cha uhalifu kinachafua matukufu ya Waislamu nchini Palestina, kinaua wanawake, wazee na watoto, na kuijaza Sudan na dawa za kulevya.

Abu Khalil pia alionyesha kazi ambayo hizb inafanya katika maeneo mbalimbali ya Sudan, akiwakumbusha watu wajibu wao wa kukabiliana na vita vya dawa za kulevya; ambazo zinachukuliwa kuwa moja ya vita vya kisasa; vita vya kizazi cha tano, na kwamba suluhisho msingi ni kufanya kazi ya kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume; Ambayo itamaliza vita hivi na kuvishinda kwa nguvu zake za kiroho na kiakili, pamoja na nguvu zake za kijeshi.

Baada ya hapo Profesa Baldo alizungumza huku akithibitisha alichotaja Abu Khalil na kusisitiza kuwa serikali kweli haiko makini katika kupambana na dawa za kulevya na akataja mifano katika suala hili. Baldo pia alionyesha kuwa wageni wanaotembelea vituo vya matibabu ya uraibu mihadarati wanazidi watu 1350 kila siku, ambapo ina maana kwamba idadi halisi ni kubwa zaidi, kwa sababu baadhi ya waraibu hawaji katika vituo vya matibabu ya uraibu kwa sababu zilizotajwa na profesa.

Mwisho , ujumbe huo ulimkabidhi Profesa Baldo baadhi ya machapisho yanayohusiana na maudhui ya mihadarati yaliyotolewa na hizb, pamoja na matoleo ya gazeti la kila wiki la Al-Raya linalotolewa na Hizb ut Tahrir, na ikasisitizwa kuwa mawasiliano yataendelea.

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu