Jumatano, 23 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  24 Dhu al-Qi'dah 1444 Na: HTS 1444 / 43
M.  Jumanne, 13 Juni 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Amerika Inarefusha Mzozo nchini Sudan ili Kuwalazimisha Raia Kukubali Utawala wa Kijeshi
(Imetafsiriwa)

Marekani ilizindua kile ilichokiita jukwaa la Kuchunguza Mzozo wa Sudan. Mnamo tarehe 9 Juni 2023, afisi ya msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilitoa taarifa kuhusu suala hili, “Jukwaa la Kuchunguza Mzozo wa Sudan linathibitisha dhamira ya Marekani ya uwazi tunapofanya kazi na washirika ili kukomesha mzozo wa kijeshi nchini Sudan; kushughulikia ukiukaji na unyanyasaji wa haki za binadamu; na kuhakikisha ufikiaji wa haraka, salama, na usiozuiliwa wa msaada wa kibinadamu kwa mashirika yanayotoa usaidizi wa kuokoa maisha kwa wale walio hatarini zaidi na wale waliohamishwa kutokana na mapigano. Marekani haiyumbishwi katika kuunga mkono kwetu matakwa ya kidemokrasia ya watu wa Sudan na matakwa yao ya uhuru, amani na haki.”

Imefahamika kwa kila mfuatiliaji wa siasa za Sudan kwamba Marekani ndiyo iliyowaagiza vibaraka wake, Burhan na Hemeti, kuchochea vita hivi vinavyoendelea nchini Sudan ili kuhujumu Azimio la Katiba linaloweka jeshi chini ya mamlaka ya kiraia, ambayo ina maana halisi ya uhamisho wa madaraka kutoka mikononi mwa wanajeshi wa Marekani kwenda kwa raia wa Uingereza ambao wanasimamia vita hivi kwa njia ambayo inazuia upande wowote kupata ushindi wa uhakika, kurefusha muda wa vita na kusukuma vyama vya kisiasa, hasa raia, katika hali ya kukata tamaa na hatimaye kukubali masharti yake, huku nguvu halisi ikibakia mikononi mwa wanajeshi wake. Taarifa hii iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani haiachi nafasi ya shaka kuhusu usimamizi wa Marekani wa mzozo huu, licha ya madai yake kwamba inajaribu kuumaliza, kama ilivyoelezwa katika taarifa hiyo ya kupotosha. Uhalisia unagongana na wanachosema, na kurudiwa kwa usitishaji mapigano ambao pande zote mbili haziuzingatii kuthibitisha uwongo na udanganyifu wa Marekani.

Ama ajabu kubwa kuliko maajabu yote kama msemo unavyosema, "msiba mbaya zaidi unakufanya ucheke" ni kile kilichosemwa katika taarifa kwamba Marekani inaunga mkono matarajio ya watu wa Sudan ya uhuru, amani na haki, wakati huo huo ikidumisha mshiko wake kwa Sudan kupitia jeshi! Inajulikana vyema kuwa Marekani inaunga mkono tu tawala za kidikteta na kijeshi katika nchi za Kiislamu zinazotawala watu wao kwa chuma na moto.

Sudan ni ardhi ya Kiislamu, na haitakombolewa kutoka kwa Marekani na watu wake, au kutoka kwa Uingereza na wafuasi wake, isipokuwa kwa kusimamisha dola iliyojengwa juu ya msingi wa Aqidah tukufu ya Uislamu, Aqidah ya Ummah wa Kiislamu, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume inayoziunganisha nchi za Waislamu, kukata mikia ya makafiri na wafuasi wao, na kurudisha izza, adhama, na kheri ya Umma huu.

[وَيَقُولُونَ مَتَى هُوَ قُلْ عَسَى أنْ يَكُونَ قَرِيباً]

“na watasema: Lini hayo? Sema: A'saa yakawa karibu!” [Al-Isra:51]

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu