Ijumaa, 24 Rajab 1446 | 2025/01/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  3 Dhu al-Qi'dah 1445 Na: HTS 1445 / 41
M.  Jumamosi, 11 Mei 2024

Taarifa ya Habari
Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan Yakutana na Nazir wa Bani Amer Al-Mutahidah
(Imetafsiriwa)

Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan ulikutana afisini kwao mjini Port Sudan mnamo siku ya Alhamisi, tarehe 1 Dhul-Qi'dah 1445 H sawia na 9 Mei 2024 M, ukiongozwa na Ustadh Nasser Ridha, Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir/Wilaya ya Sudan, na wanachama wa Hizb: Abdullah Hussein, Mratibu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano, na Montaser Karar, Mratibu wa Kamati ya Mawasiliano wa Amali mjini Al-Qadarif, na Mohammed Mukhtar, Mwanachama wa Hizb ut Tahrir. Ujumbe huo ulikutana na Nazir Mohammed Darrar Abd al-Qadir, Nazir (kiongozi wa kabila) la Bani Amer Al-Mutahidah.

Mkutano huo ulijadili kazi ya Hizb ut Tahrir na juhudi zake kwa Ummah kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, na kuregesha mamlaka ya Uislamu, ambayo kukosekana kwake kumewasibu Waislamu na mitihani na dhiki, na hali yao mbaya ya sasa haitarekebishwa isipokuwa kwa lile walilorekebisha kwalo wa mwanzo wao, ambalo ni Uislamu mtukufu.

Ummah unaishi katika wakati muhimu, ima kurudisha mradi wa Khilafah ambao unafanikisha umoja, utu na heshima yake, au kuendeleza mradi wa Magharibi, ukoloni kupitia uongozi batili wa kidemokrasia na dola za kisekula ambazo zinagongana na itikadi ya Uislamu.

Nazir aliishukuru Hizb ut Tahrir kwa juhudi ya dawah ya kuelimisha inayofanya, na akaitakia Hizb mafanikio na uongofu, akieleza utayari wake wa kuhudhuria semina, makongamano, vikao, na shughuli nyenginezo.

Kwa kumalizia, pande zote mbili zilithibitisha kuendelea kwa mawasiliano na ziara.

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu