Jumanne, 22 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  27 Shawwal 1445 Na: HTS 1445 / 37
M.  Jumatatu, 06 Mei 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Nazir wa Makabila yote ya Darfur Akutana na Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan ilimpokea afisini mwake adhuhuri mnamo siku ya Jumapili, 26 Shawwal 1445 H sawia na 05/05/2024 M,  Al-Nazir Faisal Musa Shugar, Nazir wa makabila yote ya Darfur, na pamoja naye alikuwa Meya Babiker Harun Adam.

Ujumbe wa Hizb ukiongozwa na Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano Ustadh Nasser Ridha na Mratibu wa Kamati ya Mawasiliano Ustadh Abdullah Hussein na Ustadh Muhammad Mukhtar na Al-Hadi Muhammad Othman wanachama wa Hizb ut Tahrir.

Mkutano huo ulishughulikia kuitambulisha Hizb ut Tahrir, na kwamba kazi yake ni kurudisha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, na kwamba Hizb inaamini kwamba utatuzi wa matatizo unaweza tu kwa kupitia kuufanya Uislamu kuwa ndio msingi wao, sio tawala zinazotungwa na mwanadamu, wala uingiliaji wa kigeni unaozusha fitna na kutaka kuigawanya nchi, na kwamba njia ya kutokea katika haya yote ni kufanya kazi ya kusimamisha dola kwa msingi ya Uislamu mtukufu. Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan iko katika mchakato wa kufanya kongamano ambalo litajadili masuala ya nchi hii, kwa kushirikisha viongozi na wanasiasa kutoka kwa watu wa nchi hii.

Al-Nazir Faisal Musa, na Meya waliukaribisha mradi huu uliowasilishwa na Hizb ut Tahrir, ambao ni wa kuwaleta pamoja watu wa nchi hii kwa msingi wa Uislamu mtukufu, na wakaeleza furaha yao kwa mkutano huu.

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

2024 05 06 Sudan OS 3 Pic

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu