Afisi ya Habari
Tanzania
H. 1 Safar 1444 | Na: 1444 / 01 |
M. Jumapili, 28 Agosti 2022 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Marekani haina Mamlaka ya Kimaadili Kulazimisha Rafiki au Adui kwa Afrika
(Imetafsiriwa)
Marekani inalazimisha kwa Bara la Afrika sheria yake ya kikoloni na ya kinafiki katika jaribio lake la kujeruhi athari ya Urusi, kuitenga na kuidhoofisha kufuatia uvamizi wake nchini Ukraine.
Marekani kwa kupitia ‘Sheria ya Kupambana na Matendo Maovu ya Urusi barani Afrika iliyopitishwa na Baraza lao la Wawakilishi, inaitaka Afrika kusitisha kujihusisha na Urusi ili kuhakikisha vikwazo vyake (dhidi ya Urusi) vinatekelezwa ndani ya bara hilo.
Kwa Sheria hiyo tajika ya Marekani inaelekeza na kulilazimisha bara la Afrika kwa kupitia Waziri wake wa Kigeni libainishe wazi wale wote wanaojihusisha na matendo ya Urusi barani Afrika, ambapo Marekani italazimika kuwaadhibu washirika hao (wa Urusi) kwa namna ambayo Marekani itaona inafaa, ikiwemo kuwawekea vikwazo au adhabu nyengine yoyote itakayoamuliwa na dola ya Marekani.
Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika imepinga hatua hizi za Marekani katika Mkutano wa karibuni wa 42 katika kikao chao cha kawaida cha wakuu wa nchi zao kilichofanyika jijini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo mkutano huo kwa pamoja walitoa msimamo kupitia waraka wao uliokataa rasmi, kuonesha kutoridhishwa kwao na kutokubaliana na sheria hiyo ya Marekani dhidi ya Urusi, wakiitaja sheria hiyo kuwa sio ya haki inayoilenga Afrika kwa hatua za kuidhabu kwa matakwa ya Marekani pekee.
Ni jambo la aibu ya wazi na unafiki usio na shaka kwa Marekani inayojizatiti kuinyoshea kidole Urusi na kuipaka matope kwa uvamizi wake nchini Ukraine, ilhali dola hiyo ya Marekani ikijisahaulisha uvamizi na ukaliaji wake wa kimabavu nchini Iraq, Afghanistan na nchi nyingine, wakiuwa kwa maelfu na kupora kusikokuwa na mfano. Pia Marekani daima imekuwa kimya kwa uvamizi wa Urusi na mauwaji yake kwa Waislamu wa Syria, kwa sababu tu jambo hilo liko sambamba na sera yake dhidi ya Uislamu wa kimfumo na kuuwa Waislamu.
Ukweli wa mambo si Marekani wala Urusi wana urafiki (wa kweli) kwa Afrika. Wakati Marekani ikiwa haijatosheka kunyonya utajiri mkubwa wa Afrika na rasilmali (zake), pia inatumia mbinu za kisiasa na kisheria kama hii ili kusahilisha njia ya sera zake za kigeni ikipatiliza udhaifu wa kimfumo wa bara la (Afrika)
Pia, kwa upande wa Urusi, maslahi yake ndani ya Afrika yanasukumwa na kitu kimoja tu, nacho ni unyonyaji wa kiuchumi, kwa kuwa nayo inakumbatia ubepari baada ya kuachana na ukomunisti, ikijihusisha kwa kiasi kikubwa na biashara kubwa ya silaha na vifaa vya kijeshi inayochukuwa zaidi ya asilimia 50 ya biashara zake barani Afrika. Maamiliano ya kibiashara baina ya Afrika na Urusi yalifikia dolari za kimarekani 17.4 billioni ndani ya mwaka 2017.
Marekani na ajenda yake ya kikoloni na ya kibepari haina kwa namna yoyote mamlaka ya kimaadili ya kulichagulia na kulilazimishia bara la Afrika rafiki au adui, bali inachohitaji Afrika ni mfumo wa kiuadilifu ambao ni wa Uislamu chini ya dola yake ya Khilafah, hapo (Afrika) itaweza kujikomboa na aina zote za idhilali za Marekani na za dola nyengine za kibepari.
Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir Tanzania
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Tanzania |
Address & Website Tel: +255778 870609 |
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz |