Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Tanzania

H.  9 Rabi' I 1444 Na: 1444 / 02
M.  Jumatano, 05 Oktoba 2022

 Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi

 [مِنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُمْ مَنْ قَضَى نَحْبَهُ وَمِنْهُمْ مَنْ يَنْتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلًا]

“Miongoni Mwa Waumini Wapo Waliotimiza Waliyoahidiana Na Mwenyezi Mungu. Baadhi Yao Wamekwisha Kufa, Na Baadhi Wanangojea, Wala Hawakubadilisha (Ahadi) Hata Kidogo.” [Al-Ahzaab: 23]

(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir / Tanzania inaombeleza kifo cha mlinganizi wake kijana kwa jina Abdi Gibu Barie (38) wa mkoani mwanza, Kaskazini Magharibi ya Tanzania.

Amerejea kwenda kwenye rehma ya Mwenyezi Mungu (swt) mnamo siku ya Jumatatu, 03 Oktoba 2022 miladi sawa na tarehe 08 Rabi' al-Awwal 1444 Hijria.

Abdi Gibu Barie (Mwenyezi Mungu airehemu roho yake), licha ya kuwa alikuwa bado mwanafunzi (katika Hizb) alikuwa mmoja kati ya wanaharakati thabiti mwenye bidii na mwenye muhanga wa hali ya juu katika da’awa ya kurejesha tena maisha ya Kiislamu, kiasi kwamba hata katika muda wake wa mwisho katika uhai wake, ndani ya siku ya Jumapili 02 Oktoba 2022 alishiriki kikamilifu katika amali za Hizb. 

Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) kummiminia marehemu katika rehma zake zilizoenea, amsamehe na kumpokea katika Pepo yake yenye wasaa. Pia (sisi Hizb) tunaungana katika maombolezo haya na familia, ndugu na marafiki (wa marehemu), huku tukiomba kwa Mwenyezi Mungu Subhanahu Wa Ta’ala  kutupa sisi nao wao subra na faraja ya hali ya juu.

[إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]

“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na hakika kwake Yeye tunarejea” [Al-Baqarah:156]

 

Masoud Msellem

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari

Hizb ut Tahrir Tanzania

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tanzania
Address & Website
Tel: +255778 870609
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu