Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Tanzania

H.  1 Jumada II 1440 Na: 1440/03
M.  Jumatano, 06 Februari 2019

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Katika Urasilimali, Kamari ni 'Bidhaa yenye Manufaa'

Kuna kilio kikubwa juu ya kukua kupita kiasi kwa vitendo vya kamari nchini Tanzania ambavyo vimeenea na kuwavutia vijana wengi kujihusisha navyo.

Wanabiashara wa vitendo hivi vya kamari wanaendesha biashara yao kwa uhalali, zilizo sajiliwa na serikali pamoja na kulipa ushuru wote unao hitajika na malipo mengineyo ya dola ambayo ni sehemu ya mapato ya serikali.

Uchezaji kamari una athari mbaya nyingi, sio tu kiakhlaqi pekee, bali hudhuru kifedha, hukuza uvivu miongoni mwa watu, na kuleta uhasama na mizozo ndani ya familia, kwani baadhi ya wazazi hufadhilisha kamari kuliko kujihusisha na vitendo vyenye natija, bila ya kutaja kuwasukuma wengi katika matarajio ya ndoto za mchana ya kuwa matajiri kwa urahisi.  

Serikali huvuna kiwango kikubwa cha maslahi na manufaa kutokana na kamari. Na hiyo ndio sababu inajifanya kutojua, na kushajiisha uchezaji huo kukua zaidi na zaidi. Takriban kila chombo cha habari hutangaza na kupigia debe kamari pamoja na kuwahadaa vijana kuwa kupitia kamari kuna njia ya urahisi ya kupata utajiri na uhuru wa kiuchumi. 

Katika mwaka wa 2014/15 serikali ilikusanya kutokana na kamari Tsh bilioni 15.3, katika 2015/16 ikapanda hadi Tsh bilioni 24.4, huku 2016/2017 ikifikia Tsh bilioni 36.8 https://www.mwananchi.co.tz/habari/Makala/Bahati-nasibu-sekta-inayokua-kwa-kasi-lakini-inahitaji-tahadhari/1597592-4390516-13prbquz/index.html

Ili kurahisisha ukusanyaji wa mapato ya kamari, serikali kupitia Sheria ya Fedha Sehemu ya 4 ya 201, ililiomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuifanyia marekebisho Sheria ya Kamari Na. 166 kupitia kuipa Mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru Tanzania (TRA) jukumu la kukadiria, kukusanya mapato ya kamari.

Kukua kupita kiasi kwa vitendo rasmi vya kamari kuna fichua umbile la nidhamu ya kiuchumi ya kirasilimali ambayo nchi zinazo endelea ikiwemo Tanzania zimeiiga. Nidhamu ambayo hukadiria na kuangazia kitu kimoja pekee, kuongeza manufaa kwa hali yoyote ile, hata kwa gharama ya kuwadhuru watu au jamii kwa jumla. 

Kimsingi, serikali zote zinazo tabanni urasilimali haziangazii tu juu ya maslahi pekee, bali huyafukuzia haswa. Kwa umbile la urasilimali, ni dhahiri kuwa kamwe hauna huruma, haujali, na hauna upole wowote kwa wanadamu wala sifa ya kutumikia na kutawala dunia. Ili kupambana kikweli na janga la kamari unahitaji kuwa na mfumo wa Kiislamu mahali pake, ambao kipimo chake cha kisheria ni 'halali' na 'haramu' na kamwe hautilii maanani kadhia ya maslahi na manufaa.

Sheria ya Kiislamu hufanya kazi kama ibada pamoja na kulinda maisha, mali, heshima na hali nzuri ya wanadamu. Kwa mfano, huharamisha kadhia kama ulevi, zinaa, riba nk, ingawa huenda zikaleta manufaa ya kimada kwa baadhi ya watu. Zaidi ya hayo, Uislamu umeharamisha kwa mkato vitendo vya kamari bila ya kuzingatia manufaa yoyote ndani yake. Ni jambo ambalo kwa kila mtu mwenye akili hutambua kwamba kamari huleta uhasama, chuki na kushajiisha uadui pamoja na kuhadaa watu katika kuota ndoto za mchana za kupata utajiri kwa urahisi.

إِنَّمَا يُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَنْ يُوقِعَ بَيْنَكُمْ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ فِي الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ وَيَصُدَّكُمْ عَنْ ذِكْرِ اللَّهِ وَعَنْ الصَّلاَةِ فَهَلْ أَنْتُمْ مُنتَهُونَ﴿

“Hakika Shetani anataka kutia kati yenu uadui na chuki kwa ulevi na kamari, na akuzuieni kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kusali. Basi je, mmeacha?” [Al-Maida 91].

Hii ni changamoto wazi kwa Waislamu, wanao himizwa kufanya kazi pasi na kuchoka ili nidhamu ya Kiislamu chini ya dola ya Khilafah ipate kutawala juu ya miamala yote, ama kwa wasiokuwa Waislamu, wakati umewadia sasa kwa wao kuuchunguza Uislamu kwa makini kama badali ya urasilimali, mfumo ambao unasifa zote za kuokoa wanadamu kutokana na minyororo miovu ya kirasilimali.

Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Tanzania

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tanzania
Address & Website
Tel: +255778 870609
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu