Afisi ya Habari
Tanzania
H. 30 Sha'aban 1439 | Na: 1439/03 |
M. Jumatano, 16 Mei 2018 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mwezi Huu Ulio Barikiwa na Uwashajiishe Waislamu Kulinda na Kutetea Matukufu Yetu
Tunatoa pongezi za dhati kwa Ummah wa Kiislamu nchini Tanzania na ulimwengu mzima kwa kuanza kwa mwezi wa Ramadhan. Mwezi wa baraka, msamaha na kuachwa huru na Moto wa Jahannam.
Ummah wa Kiislamu Mashariki na Magharibi unaukaribisha na kuukumbatia mwezi huu wa Ramadhan kutokana na hadhi yake na utukufu wake. Hivyo basi, ni wajib pia katika mwezi huu kuukumbusha Ummah wetu kufanya kazi ya ulinganizi bila ya kuchoka ili tuweze kulinda, kutetea na kukirimu matukufu yetu ipasavyo. Miongoni mwayo ni yafuatayo:
1. Maisha, Heshima na Hadhi ya Waislamu.
Leo, tunashuhudia ulimwenguni Waislamu wakidhulumiwa, wakidhalilishwa, wakiuwawa, wakiteswa nk. umwagwaji damu wa hivi karibuni ulifanywa siku chache zilizopita na umbile la Kiyahudi kwa zaidi ya waandamanaji kwa amani 50 (Mashahidi) katika kampeni ya kutetea ardhi ya Waislamu kufuatia hatua ya Marekani ya kuhamisha ubalozi wake hadi Jerusalem. Zaidi ya hayo, damu ya Waislamu inamwagika kila dakika nchini Syria, Yemen, Iraq, Afghanistan, Burma, Afrika ya Kati, Somalia nk. bila ya kutaja mauaji na mateso ya Waislamu mikononi mwa Makafiri na vibaraka wao (katika magereza yao) pamoja na kuwakosea heshima wanawake Waislamu na wazee kila mahali.
2. Utukufu wa Quran
Kuilinda Quran Tukufu yamaanisha kuhifadhi cheo chake na kuipa dori yake kama uongofu kwa nyanja zote za maisha ya mwanadamu. Quran Tukufu iliteremshwa katika mwezi huu mtukufu kwa Ummah huu bora. Haingii akilini kuikirimu Ramadhan pasi na kuikirimu Quran, kwa sababu tumeipata Ramadhan kutoka kwa Quran.
3. Heshima ya Mtume (saw)
Leo kuna kampeni ovu ya kumdhalilisha na kumkosea heshima Mtume (saw) kwa kisingizio cha uhuru wa maoni. Makafiri bila ya aibu wamewekeza juhudi kubwa hata kujaribu kuwakinaisha Waislamu kuikubali kadhia hii ya kumtusi Mtume (saw) kama jambo la kawaida. Mtume (saw) alikuwa na hamu kubwa kwa Ummah wake, ni wajib juu ya Ummah wetu kuonyesha hamu kubwa kwa Mtume (saw).
4. Misikiti Mitukufu
Fiqhi ya Kiislamu inafafanua waziwazi juu ya utukufu (Haram) wa Misikiti mitukufu, ambayo ni misikiti mitatu, kwa bahati mbaya misikiti yote mitukufu mitatu, kimsingi Waislamu hawana nafasi nayo ipasavyo. Msikiti wa Haram na Msikiti wa Mtume mjini Madina iko mikononi mwa watawala vibaraka, ambao wanaitumia kama maduka ya familia zao kujipatia faida, huku Msikiti wa Al-Aqsa uko mikononi mwa mvamizi aliye laaniwa, dola ya Kiyahudi ya "Israel". Ramadhan na itusukume zaidi na zaidi kuikomboa misikiti hii mitatu mitukufu
Ili kulinda, kuhifadhi na kutetea kikamilifu matukufu yetu tunahitaji kuwa na nguvu na mamlaka ya Dola ya Kiislamu ya Khilafah, hii ndio nguzo na ngao ambayo Waislamu watakuwa nyuma yake katika kuangalia na kusimamia mambo yote. Ramadhan na iwe ni kishajiisho kwetu cha kufanyia kazi suluhisho hili.
﴾ذَلِكَ وَمَنْ يُعَظِّمْ حُرُمَاتِ اللَّهِ فَهُوَ خَيْرٌ لَهُ عِنْدَ رَبِّهِ﴿
“Ndio hivyo iwe! Na anaye vitukuza vitakatifu vya Mwenyezi Mungu basi hayo ndiyo kheri yake mbele ya Mola wake Mlezi.” [Al-Hajj: 30]
Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Tanzania
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Tanzania |
Address & Website Tel: +255778 870609 |
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz |