Afisi ya Habari
Tanzania
H. 21 Shawwal 1438 | Na: 1438/05 |
M. Jumamosi, 15 Julai 2017 |
Taarifa Kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir Kamwe Haijawahi na Kamwe Haitakuwa Shirika la Kigaidi!
Katika msururu wa kipindi "Jihad na Ugaidi" kilicho peperushwa hewani na Radio/TV Iman mnamo 03/07/2017 (marudio yake kupeperushwa mnamo 06/07/2017), mwendesha kipindi Muhammad Issa aliituhumu kirongo Hizb ut Tahrir kwa tuhuma hatari baada ya kuitaja kuwa ni shirika la kigaidi.
Muhammad Issa aliituhumu Hizb ut Tahrir bila ya kunukuu dalili yoyote, ingawa chama hiki kina machapisho mengi, kama vitabu, vijitabu, majarida nk ambayo yanafafanua waziwazi fikra zake na njia yake. Kuhusu njia yake, Hizb ut Tahrir imeweka wazi zaidi kuwa imejifunga katika mvutano wa kifikra na wa kisiasa pekee bila ya kutumia ghasia au kujihusisha na nguvu yoyote ili kufikia lengo lake.
Hizb ut Tahrir inashutumu vikali tuhuma hii ambayo inabeba ajenda chafu dhidi ya Ummah wa Waislamu kwa jumla na hususan Hizb ut Tahrir. Hakika, tuhuma hii isiyokuwa na msingi sio tu inatusikitisha sisi pekee bali kila mwenye akili timamu na muadilifi. Fauka ya hayo, ni ukiukaji wa maadili ya utangazaji na msingi wa uadilifu wa kimaumbile na kuwanyima wengine haki ya kusikika.
Sisi katika Hizb ut Tahrir licha ya kukutana ana kwa ana na uongozi wa Radio/TV Iman, tumepeleka malalamishi ramsi na kuwataka warekebishe tuhuma hiyo, vilevile tunajaribu kwa dhati kukutana ana kwa ana na Muhammad Issa (mwendesha kipindi), ambaye la kusikitisha ni kana kwamba anasita na anatukwepa kwa uoga. Idadi ya hatua kadhaa ziko katika mchakato wa kukabiliana na kadhia hii.
Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Tanzania
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Tanzania |
Address & Website Tel: +255778 870609 |
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz |