Afisi ya Habari
Tanzania
H. 26 Rabi' I 1439 | Na: 1439 / 01 |
M. Alhamisi, 14 Disemba 2017 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Taasisi za Dola Nchini Tanzania Zimewakamata kwa Dhulma Wanachama Watatu wa Hizb ut Tahrir Bila ya Sababu Yoyote!
Hizb ut Tahrir / Tanzania inashutumu vikali vitendo vya mamlaka za dola zilizo wakamata wanachama wake watatu na kuwafungia pasi na kuwa na mawasiliano yoyote bila ya maelezo au uwakilishi wa kisheria kwa zaidi ya mwezi mmoja kinyume na sheria kisha kubuni mashtaka ya uongo na maovu dhidi yao ya 'njama ya kutekeleza ugaidi' na 'utekelezaji ugaidi'. Madai haya ni maovu waziwazi, urongo na yasiyo na msingi wowote!
Mwanachama wa kwanza kukamatwa alikuwa Waziri Suleiman Mkaliaganda (miaka 31), mwalimu wa sekondari aliye nyakuliwa mnamo 21/10/2017 nje ya msikiti karibu na nyumba yake, mjini Mtwara kusini mwa Tanzania, wengine wawili walikamatwa jijini Dar nao ni Omar Salum Bumbo (miaka 49), fundi muashi aliye nyakuliwa kwa nguvu na watu wasio julikana ambao hatimaye walikuja kutambulika kuwa maafisa wa usalama mnamo 27/10/2017 kisha Ramadhan Athuman/Ustadh Moshi (miaka 39), mwalimu wa Kiislamu na mfanyi biashara aliye nyakuliwa mnamo 30/10/2017 kutoka nyumbani kwake.
Omar Salum Bumbo alinyakuliwa na maafisa wa usalama baada ya mmoja wao kumwalika sehemu ili kumwajiri kama fundi muashi. Alipofika sehemu hiyo waliyo kubaliana, alitekwa nyara kwa nguvu, na kutiwa ndani ya gari lililoondoka naye kwa kasi baada ya kumuonya mwendeshaji pikipiki wake kuondoka mara moja.
Ustadh Ramadhan Moshi alikamatwa mbele ya familia yake akiwepo pamoja naye mwenyekiti wa mtaa wake kwa jina Magomeni Makuti 'A' na maafisa wa usalama wakaahidi kuwa maelezo ya kukamatwa kwake yangepatikana baadaye katika kituo cha polisi karibu naye. Lakusikitisha hili lilithibitika kuwa ni urongo! Omar Salum pamoja na Ramadhan Moshi 'walipotea' kwa wiki nyingi pasi na habari zozote kuwahusu licha ya familia na jamaa zao walio na wasiwasi kuzuru vituo vingi vya polisi kujulia kuwahusu. Wakati huu wote, wanachama wote watatu walinyimwa haki zao msingi kama uwakilishi wa kisheria.
Kwa kujibu, Hizb ut Tahrir / Tanzania inaanza kwa kuuliza: Je, kuna yeyote ulimwenguni asiyejua kwamba tangu kuasisiwa Hizb ut Tahrir imeshikilia barabara njia iliyo wazi ya kubadilisha mujtama iliyo fuatwa na Mtume Muhammad (saw) inayo hitaji kujifunga na amali za kifikra na kisiasa pasi na kutumia nguvu au ghasia wakati wowote? Hii ni njia isiyo badilika ambayo wanachama wote wa Hizb ut Tahrir kote ulimwenguni wanahitajika kuidumisha na kuiamini, njia ambayo imeifafanua waziwazi katika vitabu vyake na matoleo yake kadha wa kadha ambavyo tunataka ummah kuvisoma wenyewe kutoka katika mitandao yetu mingi na maarufu ya kijamii ya kiulimwengu.
Kisha tunauliza: Je, mamlaka za dola zilizo wakamata ndugu zetu wakati wa uchunguzi wao kamwe hawakuisoma taarifa kwa vyombo vya habari inayo fafanua lengo letu, njia na muundo wa kazi ya Hizb ut Tahrir nchini Tanzania na kiulimwengu tuliyoichapisha mara tu baada ya kongamano letu kubwa la kimataifa lililo fanyika mnamo 19 Julai, 2007 katika Msikiti wa Kichangani, Dar es Salaam kwani tunafanya kazi hadharani katika mujtama kwa miaka mingi bila ya kujificha? Tunawaomba Ummah tena kuisoma hii hapa taarifa kwa vyombo vya habari:
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI UFAHAMU WA KIMAKOSA KUHUSU HIZB UT TAHRIR KUWA NI ‘CHAMA CHA KISIASA'
http://www.hizb-ut-tahrir.info/sw/index.php/taarifa-kwa-vyombo-vya-habari/kenya/511.html
Kwa mara nyingine tena tunauliza: Je, mamlaka za dola hazijui kuwa Hizb ut Tahrir inafanya kazi hadharani kulingania Uislamu kifikra ulimwengu mzima ikiwemo kuendesha kazi yake waziwazi katika nchi nyingi mashuhuri zinazo ongoza vile vinavyoitwa 'Vita dhidi ya Ugaidi' ikiwemo Marekani, Uingereza nk bila ya nchi hizi kuwahi kudai kuwa Hizb ut Tahrir imewahi kutekeleza kitendo chochote cha kigaidi? Je, Tanzania ina vyombo imara na bora vya usalama na ujasusi kushinda nchi hizo kiasi cha kusema urongo wazi wazi na kudai kuwa wanachama hawa watatu wa Hizb ut Tahrir wameshirikiana katika kitendo cha kigaidi?
Ikiwa huo unaoitwa uchunguzi umepuuzia kadhia hizi msingi basi hauko wazi na si chengine isipokuwa ni dhulma na unyanyasaji pasi na msingi wowote dhidi ya Uislamu, Waislamu na wanachama hawa watatu waliokuwa mashuhuri katika mujtama katika kuepusha ghasia, uovu na vitendo vyovyote vya kigaidi?
Hizb ut tahrir / Tanzania imerudia mara kwa mara na kutangaza hadharani, na tutaendelea kufanya hivyo bila ya hofu, kuwa Sheria ya Kupambana na Ugaidi ni sheria ya kimapendeleo iliyo lazimishwa na nchi zenye nguvu na inatumiwa kuwakandamiza, kuwahofisha, kuwatesa, kuwapoteza na kuwauwa jamii ya Waislamu ikiwemo kuwanyima haki zao msingi za kutekeleza waziwazi ulinganizi wa Uislamu. Kuwakamata wanachama hawa ambao kamwe hawajawahi kutekeleza au kupigia debe ugaidi katika kulingania Uislamu ni mojawapo ya mifano ya kutamausha ya dhulma zinazo wakumba Waislamu kutokana na sheria hizi za kidhalimu.
Kwa kutamatisha, Hizb ut Tahrir / Tanzania inataka kuondolewa mara moja mashtaka na kuachiliwa bila masharti kwa wanachama wake kwani hawajafanya uhalifu wowote.
Fauka ya hayo, tunawaomba viongozi wote katika mujtama, wasomi, wanahabari na umma kwa jumla kutusaidia kulitangazia hadharani tukio hili katika kutafuta kuachiliwa kwa ndugu zetu kutoka katika udhalimu na unyanyasaji huu kwani kila mwenye busara anajua kuwa unyanyasaji unaoendelea wa sheria hizi za kuwakandamiza Waislamu wasio na hatia ya lawama si chengine isipokuwa ni ukumbusho mbaya wa enzi katili ya ukoloni na mtindo hatari sio tu kwa Waislamu pekee bali kwa haki katika mujtama mzima.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Tanzania
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Tanzania |
Address & Website Tel: +255778 870609 |
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz |