Jumatano, 23 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia

H.  12 Safar 1444 Na: 1444/03
M.  Alhamisi, 08 Septemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Taasisi ya Afisi ya Rais na Kushindwa Kifikra Kuikabili Hizb ut Tahrir
(Imetafsiriwa)

Mnamo Jumanne, tarehe 30/8/2022, ujumbe kutoka Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir/Wilaya ya Tunisia, ukiongozwa na Ustadh Yassin Bin Yahia, wakiwemo wajumbe Ustadh Al-Habib El Madini na Mohammad Ali Bin Salim, walitembelea Taasisi ya Tunisia ya Mafunzo ya Kimkakati, ambayo ni taasisi rasmi chini ya usimamizi wa Afisi ya Rais wa Jamhuri. Hii ni kuwasilisha nakala za kitabu, Kukanusha Fikra ya Kirasilimali ya Kimagharibi kama Mfumo, Hadhara na Thaqafa, kilichochapishwa hivi karibuni na Hizb ut Tahrir. Hata hivyo, licha ya majaribio ya mara kwa mara na mashauriano ya muda mrefu yaliyofanywa na afisi ya udhibiti ya taasisi hii, uamuzi wao ulikuwa kutozipokea nakala hizo, na kupuuza umbile la dori ya kifikra na kitafiti ya taasisi yao wanayodai, kwa sababu tu walijikuta wako mbele ya pendekezo linalokanusha misingi ya fikra za Kimagharibi ambazo wamejiweka kuwa walinzi wake katika nchi yetu! Huku usimamizi wa Taasisi hii ya Tunisia ya Mafunzo ya Kimkakati hauoni ubaya wowote katika kushirikiana na taasisi za kikoloni za Magharibi ambazo zimejengwa katika ardhi yetu, kama vile Wakfu wa Konrad Adenauer wa Ujerumani (KAS). Imefikia hata hatua ya kujivunia kufanikiwa kukamilisha tafiti 20 za kimkakati za kisekta, pamoja na taasisi hii ya kigeni, katika mwaka wa 2020 kuhusiana na uchoraji ruwaza ya Tunisia baada ya Uviko-19 kwenye upeo wa mwaka wa 2025.

Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir/Wilaya ya Tunisia imekuwa ikisambaza kitabu hicho kilichotajwa hapo juu kwa muda kwa watu wenye fikra na maoni, maprofesa wa vyuo vikuu na wajuzi wa fikra za kisasa ambao wamegubikwa na hadhara ya Kimagharibi, wakiongozwa na wajumbe wa Idara ya Masomo ya Kibinadamu na Sayansi ya Jamii, Idara ya Hadhara ya Kiislamu na wanachama waheshimika wa Wakfu wa ‘House of Wisdom’. Kwa kufanya hivi, Hizb ut Tahrir inatoa changamoto kwa wale ambao wamerogwa na thaqafa ya Kimagharibi, wakiongozwa na wajumbe wa ‘House of Wisdom’ na Taasisi ya Kimkakati ya Tunisia yenye mafungamano na afisi ya rais, wajadiliane nao kifikra ili kudhihirisha ufisadi wa mfumo wa kirasilimali na utukufu wa mfumo wa Uislamu. Hii ni ili waachane na utegemezi wao wa kifikra na kisiasa kwa mkikoloni kafiri Magharibi na kuregea kwenye mikono ya Ummah wao na kuunga mkono mfumo mtukufu wa Uislamu, ili wafidie kwa hili uhalifu wao wa kueneza fikra ya Kimagharibi na kupapatika katika kuihami.

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[بلْ نَقْذِفُ بِالْحَقِّ عَلَى الْبَاطِلِ فَيَدْمَغُهُ فَإِذَا هُوَ زَاهِقٌ وَلَكُمُ الْوَيْلُ مِمَّا تَصِفُونَ]

“Bali tunaitupa kweli juu ya uwongo ikauvunja na mara ukatoweka. Na ole wenu kwa mnayo yazua.” [Al-Anbiya: 18].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Tunisia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
Address & Website
Tel: 71345949 / 21430700
http://www.ht-tunisia.info/ar/
Fax: 71345950
E-Mail: tunis@htmedia.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu