Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uholanzi

H.  1 Muharram 1443 Na: 01 / 1443
M.  Jumatatu, 09 Agosti 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Uhuru, Usawa, Udugu na Unafiki

 (Imetafsiriwa)

Wakati Waziri wa Mambo ya Ndani wa Mrengo wa kulia wa Ufaransa Gerald Darmanin aliposema mnamo Desemba 2020 kwamba Mwenyezi Mungu kwa njia yoyote si mtukufu zaidi ya jamhuri ya Ufaransa yeye kwa kweli alionyesha unafiki wa hadhi ya watu wa kawaida wa Ufaransa. Sasa serikali ya Ufaransa imeanzisha tume mpya ya mawaziri kwa ajili ya usekula ambayo itageuka na kuwa 'afisi ya usekula'. Kitendo ambacho ni wazi kinakusudiwa kuwafundisha Waislamu 'kuipenda jamhuri'.

Katika safu ndefu ya Twitter ya 'Kamati ya kuzuia uhalifu na misimamo mikali', Kamati hiyo ilitangaza kwamba kamati mpya ilitangaza kuwa hadhi ya watu wa kawaida ni "uhuru kwanza". Kwa kweli, hadhi ya watu wa kawaida ni chapa ya Kifaransa ya usekula ambayo ni razini na ya kinyama. Wanasiasa wa Ufaransa wameutumia usekula mara kwa mara kama chombo cha kibaguzi kuikandamiza idadi ya Waislamu inayokua.

Tume hiyo ya usekula pia inapanga kuwashawishi wanawake wa Kiislamu kwamba usekula ni "njia kuelekea ukombozi" na "haki za wanawake" kuchagua jinsi watakavyotekeleza imani yao, kwa ukamilifu au kwa kiasi. Baada ya tangazo hilo wengine walikuwa wepesi kusema kuwa wasichana wengi wa Kiislamu katika shule za umma wamenyimwa uhuru wao wa kuvaa wanachotaka baada ya marufuku ya hijab mnamo 2004 na kwamba hili, kiuhalisia, ni hali ya unafiki wa watu wa kawaida wa Ufaransa.

Kama sehemu ya mapendekezo yao dola pia itatumia wafanyikazi wa umma ambao watawakagua wanasiasa wa nchi hiyo na kuwahimiza kuandaa matukio yenye kauli mbiu za kisekula. Tume hiyo ya usekula pia itaweka "siku ya usekula" mnamo tarehe 9 Disemba, siku ya kuzaliwa ya sheria mnamo 1905 ambayo ilianzisha usekula nchini Ufaransa. Na yote haya ni kwa jina la msimamo usioegemea upande wowote wa dola ya Ufaransa dhidi ya raia wa Ufaransa na kinyume chake.

Huo unaoitwa msimamo usioegemea upande wowote haujawahi kuwa hivyo kwa muda na kinyume chake kilithibitishwa na jaribio la kujihusisha katika maswala ya (kidini) ambayo haikuwa ni jukumu lake pamoja na tangazo la udhihirishaji mwanzoni mwa 2021 (mpango wa Baraza la Kitaifa la Maimamu ili kuwafuatilia viongozi wa dini ya Kiislamu nchini Ufaransa).

Msimamo huu wa kinafiki wa Magharibi hauishii kwa Ufaransa pekee. Uamuzi wa mahakama ya Ulaya wa kuwawezesha waajiri kupiga marufuku wafanyikazi wao kuvaa hijab, uchapishaji wa "Ramani ya Uislamu" yenye utata (uchapishaji wa majina yote, kazi, anwani za taasisi za Kiislamu ikiwemo mafungamano yao ya kisiasa nje ya nchi) na Serikali ya Austria na ukosefu wa uangaziaji wa vyombo vya habari kuhusiana na nia na fikra zilizo dhidi ya Uislamu za afisa wa kijeshi wa Ubelgiji ambaye alikuwa mafichoni wiki chache zilizopita na kupatikana amekufa mwishoni mwa Juni 2021 nchini Ubelgiji vyote ni visa vya uhasama wa Ulaya dhidi ya Uislamu.

Waislamu huko Magharibi wanapaswa kujua uwindaji dhidi ya Uislamu. Hawatamkumbatia kikamilifu Muislam isipokuwa ikiwa amelowa kikamilifu na fikra ya kisekula, ya kidemokrasia. Watu wa kawaida wanaweka wazi kwamba wana fikra yote au la linapokuja suala la Waislamu. Jambo ambalo Waislamu walikuwa tayari wanalijua wakati aya ifuatayo ilipoteremshwa:

(وَلَن تَرْضَى عَنكَ الْيَهُودُ وَلاَ النَّصَارَى حَتَّى تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ قُلْ إِنَّ هُدَى اللّهِ هُوَ الْهُدَى وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ أَهْوَاءهُم بَعْدَ الَّذِي جَاءكَ مِنَ الْعِلْمِ مَا لَكَ مِنَ اللّهِ مِن وَلِيٍّ وَلاَ نَصِيرٍ)

“Mayahudi hawawi radhi nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate mila yao. Sema: Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu ndio uwongofu. Na kama ukifuata matamanio yao baada ya ujuzi ulio kwisha kujia, hutapata mlinzi wala msaidizi kwa Mwenyezi Mungu.” [Al-Baqara: 120].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Uholanzi

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uholanzi
Address & Website
Tel:  0031 (0) 611860521
www.hizb-ut-tahrir.nl
Fax:  0031 (0) 611860521
E-Mail: okay.pala@hizb-ut-tahrir.nl

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu