Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uholanzi

H.  4 Rabi' I 1443 Na: 02/1443
M.  Jumatatu, 11 Oktoba 2021

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ripoti ya Pano Iso Haya juu ya Elimu ya Kiislamu ni Njama ya Wazi na Uchochezi

 (Imetafsiriwa)

Wiki hii kwenye "Pano" ya VRT (Kampuni ya Umma ya Utangazo ya Kiflemi nchini Ubelgiji) ilichunguza jinsi elimu ya Kiislamu mashuleni imepangiliwa katika upande wa maalumati na ushawishi ulionao Morocco, Uturuki na Dola za Ghuba kwa misikiti anuwai nchini Ubelgiji. Miongoni mwa mambo mengine, ripoti hiyo ilijadili Waislamu wanaopitia shinikizo la kisiasa kuhusiana na uzoefu wao wa kidini na kwamba uangalizi fulani hufanywa na ubalozi wa Morocco. Maimamu wa Kituruki wanaojiunga na mwavuli wa Diyanet huegemea kwa karibu upande wa chama cha Rais Erdogan na ufadhili unaopokewa kutoka kwa Dola za Ghuba unatoka kwa mashirika ambayo yanadaiwa kufungamana chembechembe za kigaidi. Kutoka na haya serikali ya Ubelgiji inafuata nyayo za serikali ya Uholanzi kuhusiana na ushawishi wa kigeni na ufadhili wa misikiti.

Ni jambo la kusikitisha kwamba kile kinachoitwa uchunguzi adilifu ni wa mapendeleo mno unaojumuisha vielelezo vya uwongo vya kawaida ili kuzidi kuutia Uislamu matatani. Hili halishangazi kwani kumekuwa na sera ya uoanishaji inayoendelea kwa muda mrefu yenye lengo la kubadilisha utekelezaji wa Uislamu wa Waislamu unaoungwa mkono na miradi mingi ya kile kinachoitwa "Uislamu wa kisasa". Licha ya hivyo, bado ni jambo la kusikitisha kuona namna gani kila wakati wanasongea mbali zaidi. Leni Franken (mtafiti na mtaalam wa masomo ya kimfumo na kidini) analalamika juu ya yaliyomo ndani ya mipango na vitabu vya masomo ya Kiislamu na kwamba hayakutabanniwa kwa "muktadha wa Ubelgiji". Hii ni hatua duni mpya katika kuvuka mpaka baina ya kanisa na serikali katika kile kinachoitwa mazingira ya kisekula.

Malalamishi yanatolewa kwa sababu wanafunzi wa Kiislamu wameelimishwa juu ya uwepo wa Mwenyezi Mungu (swt), ambao ndicho kiini cha imani ya Kiislamu. Na kisha kuna mada za kawaida kama vile jinsi gani imani inahusiana na sayansi, haki za wanawake na ushoga. Franken anasema katika uchunguzi huo huo kuwa ni muhimu kuwapa vijana wa Kiislamu kwa fahamu kama nadharia ya mageuzi ya kimaumbile. Hata alielezea ukosoaji wake dhidi ya watendaji wa Kiislamu ambao walianzishwa na serikali ya Ubelgiji ili kuendeleza "Uislamu wa Ulaya", akisema wanapaswa kuwa kama chombo cha ufuatiliaji.

Bila aibu yoyote, Wabelgiji wanaendelea kuushambulia Uislamu kikamilifu kwa njia ya kupaka tope na kuiomba serikali ya Kiflemi kuamuru jinsi Waislamu watakavyo uelewa na kutekeleza Uislamu, jambo ambalo moja kwa moja linapingana na kanuni zao wenyewe. Kwa kuongezea, malalamiko haya ya kirongo juu ya ushawishi wa kigeni hayana msingi kabisa kwani Magharibi ya kikoloni na sera yake ya kibeberu inafurahi kufanya kazi pamoja na vibaraka wao katika nchi za Waislamu kuwanyenyekesha Waislamu.

Ni muhimu sana kwetu Waislamu tutambue ajenda zao na kushikilia kikiki kitambulisho chetu cha Kiislamu, kwa ajili yetu wenyewe pamoja na vizazi vijavyo. Hatuwezi kukubali aina hizi za njama na uwongo. Hivi sasa tunapaswa kuungana zaidi kama jamii kulinda msingi wa Dini yetu wanaoutilia shaka kuliko wakati mwengine wowote. Mwenyezi Mungu atusaidie.

 [وَيَمكُرونَ وَيَمكُرُ اللَّهُ وَاللَّهُ خَيرُ الماكِرينَ]

Wakapanga mipango yao, na Mwenyezi Mungu akapanga yake. Na Mwenyezi Mungu ndiye mbora wa mipango. [Al-Anfaal: 30]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Uholanzi

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uholanzi
Address & Website
Tel:  0031 (0) 611860521
www.hizb-ut-tahrir.nl
Fax:  0031 (0) 611860521
E-Mail: okay.pala@hizb-ut-tahrir.nl

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu