Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki

H.  5 Safar 1444 Na: 1444 / 05
M.  Alhamisi, 01 Septemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Sababu ya Bei ya Juu ya Umeme na Gesi Asilia ni Sera za Kirasilimali
(Imetafsiriwa)

Mamlaka ya Udhibiti wa Soko la Nishati la Uturuki (EPDK) ilitangaza ongezeko la ushuru wa umeme kwa vikundi vya utumizi wa nyumbani kwa 20%, na kwa vikundi vya utumizi wa viwanda kwa 50%. Wakati huo huo, Shirika la Mabomba ya Mafuta la Uturuki (BOTAŞ) lilitangaza ongezeko la 20.4% la ushuru wa gesi asilia kwa utumizi wa nyumbani na ongezeko la 50.8% la ushuru wa gesi asilia kwa utumizi wa viwandani. Kwa hivyo, viwango vya ongezeko la gesi asilia na umeme kwa utumizi wa nyumbani vilizidi 200% katika mwaka uliopita.

Sababu ya kuongezeka huku kwa EPDK pamoja na BOTAŞ, ambazo zinachukuliwa kuwa za kawaida kwa watu wetu, sio janga au mgogoro wa nishati wa kiulimwengu, kama inavyosemwa. Ingawa inachukuliwa kuwa sehemu ya sababu yenye kuathiri kwa kiasi fulani ongezeko hilo, kwa kweli ni kisingizio tu cha ongezeko hilo. Ama chanzo halisi cha tatizo, ambacho kinachukua nafasi ya kwanza, ni mfumo wenyewe wa kirasilimali. Isitoshe, sera mbovu za kiuchumi za serikali, zinazobinafsisha hitaji msingi la wananchi, na kuwaacha watumizi kwenye huruma ya mashirika yanayoungua kwa ulafi wa faida, ambayo ni moja ya sababu kuu. Kwa kuwa serikali imetabanni dhana kwamba "dola haiingilii uchumi, bali inasimamia tu", imetabanni ubinafsishaji wa nishati kama mfano, na haswa imetoa biashara nzima ya usambazaji wa umeme kwa udhibiti wa sekta binafsi. Kutokana na ubinafsishaji huu, gharama zote kama vile gharama za usambazaji, gharama za upotevu na uvujaji, gharama za uwakilishi na ukarimu, hasa ongezeko la deni la mikopo la makampuni yaliyoorodheshwa kwa fedha za kigeni, zilikuwa na zinaendelea kutozwa kwa mtumizi. Ushuru wa dhulma ambao dola inapokea kutoka kwa huduma hizi ni zao la dhulma inayotabikishwa. Hata hivyo rasilimali hizo mfano umeme na gesi asilia ambazo zimekuwa zikiibiwa na makampuni ya kibepari kwa jina la ubinafsishaji, kimsingi ni mali ya wananchi na haiwezi kupeanwa na kuuzwa kwa watu binafsi au makampuni kwa namna yoyote ile.

Enyi Watawala: Kama vile mlivyokabidhiwa utawala na usimamizi, rasilimali za nishati zinazomilikiwa na watu pia zimekabidhiwa kwenu. Hamuwezi kuwasaliti watu kwa kuuza rasilimali hizi kwa makampuni binafsi. Na hamuwezi kutoa mali inayomilikiwa na raia wote na kuyapa makampuni machache ya kirasilimali; Mukifanya hivyo, munasaliti uaminifu. Kinachopaswa kufanywa, ni kuhisi wajibu wa kuwaletea wananchi mapato ya mitambo yote ya kuzalisha umeme, makaa ya mawe, migodi mingine, rasilimali za mafuta na gesi asilia ambazo zimeachwa kwa matumizi ya makampuni kupitia ubinafsishaji, kwa wananchi bila nia ya faida yoyote kutoka kwa serikali.

Enyi Waislamu: Mfumo wa kirasilimali, kwa umbile lake, ni mfumo wa kidhalimu unaochukua kutoka kwa maskini na kuwapa matajiri. Katika mfumo huu, mabepari wakubwa, mabenki, makampuni ya fedha na kipote cha watawala wanaoshirikiana nao daima hushinda. Ama watu, wameshutumiwa kufanya kazi ili kupata riziki, na kuishi kwa madeni na taabu. Hivyo basi, ili kutatua matatizo yote ya kiuchumi kama vile bili zinazotulemea migongo yetu, gharama kubwa ya maisha na dhuluma ya mapato, ni lazima tuondoe mfumo huu kutoka kwenye mizizi yake na kuubadilisha kwa mfumo wa uchumi wa Kiislamu, ambapo hakuna unyonyaji na riba na ambapo mali ya umma inalindwa na kuhifadhiwa. Ni dola ya Khilafah Rashida ndiyo itakayokomesha mfumo wa kirasilimali, chanzo cha matatizo yote. Hivyo basi, tujitahidi kufanya kazi pamoja bega kwa bega ili kuisimamisha tena hivi karibuni, Mwenyezi Mungu akipenda.

[كَيْ لَا يَكُونَ دُولَةً بَيْنَ الْاَغْنِيَٓاءِ مِنْكُمْ]

ili yasiwe yakizunguka baina ya matajiri tu miongoni mwenu. [Al-Hashr:7]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Uturuki

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu