Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ufaransa na Udanganyifu Wake wa Uhuru wa Kujieleza

Tunachokishuhudia nchini Ufaransa ni mgongano wa hadhara. Kwa muda mrefu ulimwengu wa Kiislamu umekuwa ukilazimishwa na tabaka lake tawala na wanafikra waikubali dhana ya kuishi pamoja na kuichukua hadhara ya Kimagharibi ikiwa na baadhi ya marekebisho. Juhudi zote za kisheria, kifikra na kisiasa kwa ajili ya kuvumbua mtindo mpya wa utawala kwa ajili ya Ulimwengu wa Kiislamu ambapo nidhamu za Kimagharibi za kisiasa na kiutawala, zilizojengwa kwa maadili ya Kimagharibi, zinabadilishwa ili kushirikisha baadhi ya unafiki kwenye maadili ya Kiislamu, kisha kulazimishwa juu ya Waislamu, zimekuwa zikiendelea kwa takriban karne sasa tangu kuvunjwa kwa utawala wa Khilafah. Chukua kwa mfano hoja hii ya kuwa Uhuru wa Kujieleza unapaswa uwe na mipaka. Hoja hii ina chukulia kuwa changamoto na kukataliwa sio fikra ya Uhuru wa Kujieleza bali ni kwa matumizi huru na yasiyo na vikwazo. Msimamo huu ni sehemu ya ushurutishaji wa kiakili ambao umelazimishwa juu ya Ulimwengu wa Kiislamu na tabaka teule la Kimagharibi ambapo misingi ya maadili ya kisiasa ya Kimagharibi haipewi changamoto, bali kutumika kwake tu kwenye “matukio fulani” huonekana kuwa na utatanishi. Hivyo ajenda inabakia kuwa imefungwa kwa “kuutaka Ulimwengu wa Kimagharibi” kufikiria tena matumizi ya mifumo yake ya kimaadili. Huu ni muelekeo mbaya na wenye kasoro.

Hadhara ya Kimagharibi imejengwa juu ya chuki ya dini. Hivi tumeshawahi kuuliza huu Uhuru kutoka kwenye Uhuru wa Kujieleza unatoka kwa nani? Wanasiasa wajinga walio na fikra za Kimagharibi na tabaka la wasomi katika Ulimwengu wa Kiislamu wanaweza kudai kuwa huu ni Uhuru jumla kutoka kwa “mipaka ya kidhalimu” inayowekwa na mtu yeyote, na hasa watawala. Huu sio uaminifu na ni uongo. Uhuru ndani ya Uhuru wa Kujieleza unatokana na vikwazo vilivyowekwa na dini. Mwanafunzi yeyote wa historia ya Ulaya atakuambia hivi. Fikra ya Kisekula, kutenganisha Dola na Kanisa, ni msingi unaofafanua mtazamo wa kisasa wa Hadhara ya Kimagharibi. Mapambano ya Ulaya ya Ukristo pamoja na dini yalilazimisha kuja kwa njia mpya ya maisha ambapo yaliasi dhidi ya dini katika uwanja wa kisiasa. Dini haikuwa na haki ya kuweka makatazo yoyote kwenye maisha ya kisiasa ya wakaazi wa Ulaya. Muelekeo wa Uliberali na ule wa hadhara ya Kimagharibi ni wa kupinga dini. Ilikuwa ni uthibitisho huu wa uhakika wake, asili, unaorudi nyuma katika mizizi inayosisitiza mtazamo wa Hadhara ya Kimagharibi na inachokisimamia wakati Emanuel Macron, Mwenyezi Mungu (swt) amuangamize, alipotangaza kuwa: “(Ufaransa) haita achana na katuni zetu.” Maraisi watatu wa Ufaransa sasa wameshatangaza wazi uungaji mkono wao kwa “haki ya kukufuru Mungu” tangu kuchapishwa kwa katuni za kukufuru Mungu na magazeti ya Ulaya. Mahakama za Ufaransa zilitoa ulinzi wa kisheria kwa Charlie Hebdo na zikatetea haki yake ya Kukufuru wakati mashtaka dhidi ya matendo yake yalipoletwa na washitaki Waislamu. Ulaya na Ulimwengu wa Kimagharibi uliandamana kwa mshikamano huku Charlie Hebdo mnamo mwaka 2015 ikitangaza “Mimi ni Charlie” kwa ujasiri waziwazi na kushambulia matukufu ya Uislamu.

Huu ni muda kwa Ummah wa Kiislamu kupinga hadhara ya kimagharibi, mifumo ya kisiasa na kiutawala na maadili yake. Suala ni Uhuru wa Kujieleza wenyewe, sio utekelezaji wake. Uislamu hauturuhusu kulaani, hauturuhusu kusengenya, hauturuhusu kuwakashifu Waislamu wengine. Waislamu wanatakiwa kuwa Wabebaji Daawa. Tuna amrisha mema na kukataza Munkar (uwovu). Uislamu hauturuhusu kuamrisha Munkar. Hauturuhusu hata kuunyamazia Munkar, isipokuwa katika baadhi ya hali. Hivyo, Uhuru gani wa Kujieleza tunaouzungumzia? Tuna sheria safi zilizo wazi, zinazo husiana na kujieleza  kama zinavyo patikana kwenye Quran na Sunnah. Na maadili yetu sio Uhuru wa Kujieleza, bali ni kujieleza kama ilivyo amrishwa na Quran na Sunnah.

Huu ni muda kwa Ulimwengu wa Kiislamu kukataa kabisa Hadhara ya Kimagharibi na kufanya kazi ya kuhuisha tena Hadhara yao (ya Kiislamu) ambayo itawezekana tu kupitia kusimamisha tena Dola ya Kiislamu ya Khilafah. Tukiwa na nguvu za Dola katika milki yetu, tutalinda utukufu wa Mwenyezi Mungu (saw) kwa vitisho vya nguvu ya kijeshi dhidi ya wanaokufuru. Kisha tutaona kama wapumbavu wa Dunia kama Macron au yeyote mwengine ataweza kusubutu kufanya kufuru hata katika ardhi zao wenyewe. Na ndio, hilo ndilo tunalosimamia kwa ajili yake. Vita au vitisho vya Vita vya Dola ya Khilafah dhidi ya wote watakao subutu kumshambulia Mtume wetu kipenzi (saw).  

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Mhandisi Moez - Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu