Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Ujumbe kutoka kwa Kaka na Dada Zetu Nchini Sri Lanka
(Imetafsiriwa)

Tunawasalimu kwa salamu ya dini iliyotukutanisha pamoja na nanyi na kutufanya mwili mmoja, endapo kiungo chake chochote kitaumwa mwili wote unashiriki nacho kwa kukosa usingizi na homa, tunawasalimu kwa salamu ya Uislamu: Assalamu Alaikum wa Rahmatullahi wa Barakatuh…

Kwa kuwa mipaka iliyoundwa imetutenganisha, kwa hivyo tunashiriki mateso yenu na kuhuzunika kwenu kwa yale yanayojiri kwenu, na endapo dola yetu inayotuunganisha na kutulinda haipo, na mwili wetu umechoka, viungo vyake vinanyofolewa na mazimwi wakali ambao wanajitahidi kushinda hisa kubwa zaidi ya viungo vyake, basi mwili huu bado ungali ni mmoja – licha ya maradhi yanayousibu - unaoteseka kwa maumivu ya kila kiungo ndani yake.

Fungamano letu ni thabiti na imara, halikatwi kwa mipaka wala masafa, wala kuzuiwa na dola au serikali, na nyoyo zetu zimefungamanishwa pamoja, zikitazama kinachotokea kwa kila kiungo cha mwili huu na kushiriki maumivu yake, na kufanya kazi kufichua vitendo vya kikatili vya uhalifu wa mfumo fisidifu wa kirasilimali kwa Waislamu. Ikiwa mfumo huu wa kiulimwengu unatafuta kuficha sifa za uhalifu wa serikali zake vibaraka au kuzihalalisha kwa visingizio visivyo vya kipuzi kama vile vita dhidi ya msimamo mkali na ugaidi, vyombo vyetu mbadala vya habari vitazifichua, vitafichua ubatili wa taarifa na tuhma zake za uongo, na kufichua chuki yake dhidi ya Uislamu na Waislamu.

Mateso yenu, ndugu na dada zetu, ni mateso yetu, na ukiukaji na udhalimu ambao makafiri hawa wanawafanyia haujafichika kwetu. Tulifuatilia kile kilichokuwa kinatokea kwenu kwa nyoyo zilizovunjika na macho yenye machozi. Tuliishi kupitia hofu ya kile mnachoteseka katika uhai na kifo. Habari zenu zimetufikia na tumejua juu ya yale muliopokea mikononi mwa wahalifu wa Kibudha wanaokuchukieni nyinyi na Uislamu. ﴿وَمَا نَقَمُوا مِنْهُمْ إِلَّا أَن يُؤْمِنُوا بِاللَّهِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ﴾  "Nao hawakuona baya lolote kwao ila kuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa." [Al-Buruj: 8], na ikawa dhahiri kwetu chuki yao kwa dini hii na hamu yao ya kupandikiza chuki na vurugu ili kukudhoofisheni. Wanaeneza hofu katika nyoyo zenu, hadi muogope kuzuru misikiti yenu na kuitelekeza kwa kuogopa kulipizwa kisasi, haswa baada ya shambulizi la Pasaka mnamo Aprili 2019, ambapo walielekeza kidole cha lawama kwenu.

Taarifa ya dada yetu mwenye umri wa miaka 60, Zarina Begum, "Tunakaa majumbani mwetu, tukiogopa kutoka", imegusa nyoyo zetu na ikawa wazi kwetu uonevu, dhuluma na hofu mnayoishi ndani yake. Lakini yanayojiri kwenu - na haswa kwa wafu wenu ambao utakatifu wa miili yao umekiukwa na kuchomwa kwa visingizio visivyo na maana - imevunja nyoyo zetu na kutusukuma kufanya kazi kwa bidii zaidi kufikisha sauti na maombi yenu hadi serikali ya Sri Lanka ikomeshe maamuzi yake ambayo yanapingana na hukmu za dini yetu ya kweli, ili tuwaheshimu wafu wetu - huko - kwa kuwazika, sio kuwateketeza.

Imetufikia kile kilichomsibu Dada Fatima Reynosa. Tunamwomba Mwenyezi Mungu ampokee kwa rehema na awabariki watoto wake, mumewe na familia yake yote kwa uvumilivu na faraja, na anayetutosheleza sisi ni Mwenyezi Mungu, na Yeye ndiye Mtekelezaji Bora wa Mambo, HasbunAllahu wa Ni'mal Wakeel, dhidi ya wahalifu hawa ambao hawakuridhika na kumteketeza, lakini walinyofoa viungo kutoka kwa mwili wake. Tulipata habari juu ya Muislamu mwingine ambaye mwili wake uliteketezwa bila ya kuswaliwa, jambo ambalo liliwakasirisha Waislamu kule, kwa hivyo waliruhusiwa kumswalia Muislamu mwingine kabla ya mwili wake pia kuchomwa moto. Sera ambayo haizingatii vifungu vya dini ya Kiislamu na kupuuza sifa na hukmu zake.

Mamlaka zimeendelea katika ukiukaji wenu, katika uhai na kifo, na hizi hapa tena, chini ya kisingizio cha kuzuia kuenea kwa janga la maambukizi la Covid-19, zinawachoma wafu wenu ambao wameambukizwa au wanashukiwa kuambukizwa navyo. kama hatua ya kuzuia iliyochukuliwa na Sri Lanka, ikifanya hivyo bila ya ulimwengu uliosalia kufanya na pasi na kuidhinishwa na Shirika la Afya Ulimwenguni ambalo liliruhusu mazishi ya wafu.

Sisi, kaka na dada zenu katika Hizb ut Tahrir, tunatoa wito kwa serikali ya Sri Lanka kusitisha sera ya kuchoma maiti za Waislamu na kupeana miili hiyo kwa familia zao ili waweze kuwaheshimu kupitia mazishi yao; kuwaswalia na kuwazika makaburini mwao. Tunaitaka iwatendee vyema na kwa haki, ili ipate kitu cha kupata shufaa kwetu siku ambayo Dola ya Khilafah itasimamishwa, ambayo italipiza kisasi kwa kila mtu ambaye ametaka kumdhuru mwanamume au mwanamke wa Kiislamu.

Tunakujulisheni kuwa tunashirikiana nanyi yale mulioko ndani yake, na tunamwomba Mwenyezi Mungu aharakishe kusimama kwa dola yetu ambayo itatukutanisha pamoja na atalipiza kisasi kutoka kwa wale wote walioukosea Uislamu na Waislamu na kuwaregeshea utu, utukufu na umoja.

Kuanzia hapa tunayageukia majeshi ya Umma na watoto wake wenye ikhlasi wa watu wenye nguvu na nusra kuweka mikono yao na kuipa nusra Hizb ut Tahrir katika kufanikisha azma yake na kusimamisha Khilafah, ambayo umekuwa ni uhalisia usio epukika kueneza amani, na usalama kote ulimwenguni ambao imesibiwa na mfumo uliopo wa kirasilimali.

Tunawageukia wanachuoni wa Ummah huu kuupeleka mkono wao katika njia sahihi ya ukombozi na kuutoa ulimwengu kutoka katika giza hadi katika nuru ya Uislamu.

Tanakwambieni, Enyi wale tunaokupendeni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kuweni na subra mithili ya ile subra ya familia ya Yasser, na Mwenyezi Mungu atatunusuru na atakunusuruni dhidi ya maadui zake na maadui wa dini yake… Mwenyezi Mungu anakataa isipokuwa aitimize Nuru Yake, hata kama makafiri watachukia.

#StopMuslimCremation
#أوقفوا_حرق_موتى_المسلمين
#MüslümanCenazeleriYakmayaSon

#KomesheniUchomajiMotoMaitiZaWaislamu

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Zeinah As-Samit

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumamosi, 02 Januari 2021 08:50

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu