Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ukosefu wa Mpangilio wa Vipaumbele vya Sera ya Kigeni kwa India Unawaangamiza Watu Wake Wenyewe Kutokana na Uhaba wa Chanjo.

(Imetafsiriwa)

Waziri Mkuu wa Delhi Arvind Kejriwal siku ya Alhamisi alisema majimbo kadhaa yaliyo tangaza zabuni mbali mbali kununua chanjo ya ugonjwa wa UVIKO-19 kutoka nje ya nchi inajenga picha mbaya kwa India ulimwenguni. Akitetea serikali juu ya ununuzi wa chanjo kutoka nje ya nchi, Waziri Mkuu alisema, “Majimbo ya India yameachwa kushindania/kupigania soko la kimataifa. UP inapigana na Maha, Maha inapigana na Orissa, Orissa inapigana na Delhi.’ Iko wapi “India”? Inaonesha picha mbaya kwa India” [Hindustani times, 13 Mei 2021]

Mwishoni mwa Aprili 2021, serikali ya umoja wa India ilikuwa imefungua usajili kwa wenye umri zaidi ya miaka 18 kuwapatia chanjo kwa awamu ya tatu kupitia jukwaa lake la Co-WIN. Hata hivyo, serikali kuu haikuweza kutoa dozi za kutosha kutekeleza harakati za chanjo kwa watu wake. Hii imesabisha majimbo kadhaa ndani ya India kukimbilia zabuni za kimataifa na kuagiza chanjo kutoka mataifa mengine. Angalau Majimbo kadhaa ya India yameamua kutafuta zabuni za kununua chanjo na kujigharamia wenyewe.

Kulingana na taarifa iliyochapishwa na wizara ya mambo ya nje, India imesambaza karibu dozi milioni 66.37 za chanjo duniani hadi kufikia mwezi Aprili 2021, wakati mataifa tajiri duniani kama Amerika imesafirisha dozi milioni 3 tu na Uingereza imesafirisha dozi milioni 1 tu. Jeff M smith kutoka katika shirika la The Heritage Foundation kitengo cha wa bobezi alisema, “Idadi ya chanjo za ziada zinazopatikana-baada ya kila mmarekani kupatiwa inakadiriwa kuwa karibu milioni 70… Amerika ina chanjo za kutosha na ziada…” tuna vifaa vya kutosha na zaidi…” Rais Joe Biden na mtangulizi wake Donald Trump wakati wa mapambano ya uhitaji wa chanjo waliomba DPA ambayo inayaacha makampuni ya Amerika bila chaguo bali kutoa kipaumbele katika uzalishaji wa chanjo ya UVIKO-19 na vifaa vya kujikinga (PPEs) kwa uzalishaji wa ndani ili kupambana na janga hatari ndani ya  Marekani.

Wakati mataifa yaliyoendelea kiuchumi na yenye idadi ndogo ya watu walikuwa wameweka vipaumbele kwa watu wao wenyewe na kufanikiwa kutoa chanjo karibu nusu ya idadi yao japo kwa mara moja, balozi wa India katika Umoja wa Mataifa alisikia raha kujivunia, “Tumetoa chanjo nyingi ulimwenguni kuliko ambazo tumetoa kwa watu wetu.” Kulingana na uhariri uliochapishwa katika jarida la kitabibu liitwalo The Lancet, India imetoa chanjo chini ya asilimia 2 ya idadi ya watu bilioni 1.4 kwa sababu ya kasi ndogo ya chanjo. Mnamo Mei 2021, India iliishiwa na chanjo mara tu baada ya kuanza usajili wa awamu ya tatu ya utoaji chanjo kwa watu wenye umri zaidi ya miaka 18. Sasa visa vya India vya COVID vinaongezeka ambavyo vilikuwa vimevuka milioni 25 na idadi ya vifo ilikuwa 274,000 ikiwa inashika nafasi ya pili zaidi kwa nchi ziliyoathiriwa na korona baada ya Amerika.

India ilishindwa kukabiliana na shinikizo la sera za kimataifa na kupelekea kujiingiza yenyewe kwenye mtego wa matakwa ya Wamagharib, imechukua jukumu la kusafirisha chanjo kwenye mataifa ulimwenguni kabla ya kuwapatia watu wake wenyewe. Mwaka jana India iliamua kuondoa marufuku ya madawa iitwayo Hydroxychloroquine sio mara tu baada ya ombi la Trump lakini baada ya nukuu ya kulipiza kisasi, ambapo alijibu swali kwenye mkutano wa waandishi wa habari na jibu lifuatalo, "ikiwa hataruhusu itoke itakuwa sawa lakini, kwa kweli, kunaweza kuwa na kisasi, kwa nini hakungekuwa nacho?"

Amerika imeingiza India katika mkakati wake wa QUAD katika eneo la Indo-pacific na mfano mwengine kama huo ambapo India ilijiunga na muungano wa kimkakati wa Amerika kuishinda China. Katika miaka mitano iliyopita Amerika imeipata India kupitia kutia saini mikataba mingi ya kushirikiana Kijeshi, kiteknolojia na vifaa kama LEMOA (makubaliano ya mabadiliko ya usafirishaji), COMCASA (mkataba wa utangamano wa mawasiliano na usalama) na BECA (Mkataba wa kubadilishana msingi na ushirikiano) sawa na mikataba kama hiyo. Kwamba Amerika ina muungano wa NATO ambao unawapa Amerika uongozi mkubwa katika kuchukua maamuzi ya kijeshi kwa tamaa za kijeshi. Nchi hizo zinazoingia katika mkataba kama hiyo hutegemea zaidi Amerika na teknolojia zake kwa hatari yao wenyewe.

Mfumo wa sasa wa ulimwengu uliojengwa juu ya Ubepari wa Kimagharibi unayanyonya mataifa mengine ili kudumisha mamlaka yake kwa gharama yeyote. Amerika ambayo ndio dola kuu zaidi ulimwenguni, inadumisha uongozi wake kwa kutoruhusu nchi zingine zaidi ya mipaka yao kujitegemea na kupunguza maswala kama hayo kupitia uwepo wa jeshi, ikiongoza miungano kama NATO au kuunda ushirika mpya kama QUAD. Nchi kama China ambayo imekubali mfumo huu wa Wamagharibi katika miundo iliyopo, hujikuta ikishindwa kuidhinisha sera zake zenyewe kwa mataifa mengine.

Mwenyezi Mungu (swt) asema katika Surah Al-Nisa:

[وَلَن يَجْعَلَ اللَّهُ لِلْكَافِرِينَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ سَبِيلًا]

“wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini.” [An-Nisaa 4:141]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Faizul ibn Ahmed

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu