Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vita vya Afghanistan: Kutoka Kwenye Uongo wa Ubabaishi Hadi Kwenye Ukweli wa Wazi!

(Imetafsiriwa)

Katika hotuba yake ya kwanza kwenye kikao cha pamoja cha bunge la Congress, Rais wa Amerika Joe Biden alihutubia kwamba: “Vita nchini Afghanistan havikukusudiwa kamwe kuwa mpango wa vizazi vingi wa ujenzi wa taifa. Tulikwenda Afghanistan ili kuwakamata magaidi waliotushambulia tarehe 9/11. Tulitenda haki kwa Osama bin Laden na kutokomeza vitisho vya magaidi wa al Qaida nchini Afghanistan. Baada ya miaka 20 ya ushujaa wa Amerika na kujitolea, ni wakati wa kuregesha majeshi yetu nyumbani.”

Joe Biden alitangaza kuwa Amerika imetimiza lengo lake kwa kumuua Osama Bin Laden: ndio maana, anaondoa majeshi ya Amerika kutoka Afghanistan. Kiukweli, Osama Bin Laden aliuawa nchini Pakistan mwaka wa 2011; hata hivyo, Wamagharibi bado huchukulia Ummah wa Kiislamu kama tishio la kihakika dhidi ya hadhara yake. swali muhimu ni kwamba ikiwa lengo kuu la Amerika lilikuwa kumuua Osama, basi kwa nini Amerika iliweka vikosi vyake nchini Afghanistan kwa miaka mingine kumi kufanya uhalifu wa kikatili?!

Kwa upande mwengine, baada ya uvamizi wa Afghanistan, Amerika ilizungumzia juu ya vita dhidi ya ugaidi, hatua za kupambana na dawa za kulevya, serikali na ujenzi wa taifa ingawa ilikuwa zaidi ya miaka ishirini iliyopita wakati wa uvamizi wa Amerika ambao kilimo cha mihadarati kilifikia kilele cha juu ambapo iliifanya Afghanistan kuwa katika kiwango cha kwanza ulimwenguni. Ingawa baada ya miaka ishirini, rais wa Amerika atangaza kwamba vita nchini Afghanistan havikukusudiwa kuwa mpango wa ujenzi wa taifa.

Watawala wasaliti wa Pakistan na Afghanistan walichangia vikosi vya Amerika katika kumshinda Osama bin Laden nchini Pakistan. Amerika imekuwa ikiwadanganya Umma kwa kauli mbiu zao (yaani ustawi, amani, haki za binadamu, haki za wanawake, demokrasia na ujenzi wa dola), hata hivyo mamilioni ya Waislamu wameuwawa kikatili na kujeruhiwa na makumi ya maelfu ya watu wakipoteza familia zao na kukimbia makazi yao chini ya miito hiyo ya kidanganyifu.

Ukweli wa kusikitisha ni kwamba vita ambavyo Amerika ilivianza mnamo 2021 ilisababisha Amerika kurudi nyuma kupitia (mpango wa kijanja) wa mazungumzo ya amani na Taliban, huku ikisababisha vita vikali kati ya Waafghani. Kwa hivyo, je! Kuna yeyote wa kuiuliza Amerika juu ya vita vyake vinavyoendelea nchini Afghanistan kwa kisingizio cha ile inayoitwa miito na malengo ya udanganyifu?! Mliwatoa mamilioni ya Waislamu kutoka katika ardhi zao kwa njia tofauti tofauti na mukawahamisha kutoka kwenye majumba yao!

Haya yote ni sawa sawa na taarifa za uongo ambazo Amerika ilitumia kudai kuhusu silaha za Iraq za maangamizi makubwa na/au silaha za kinyuklia na vilevile uhusano baina ya Iraq na al-Qaida ambao baadaye ulisaidia Amerika kuikalia Iraq kwa kisingizio hiki, ingawa ilikuja mwishowe kuthibitisha kuwa Iraq haikuwa na silaha kama hizo kabisa, na kwamba Amerika ilitaka kuonesha nguvu zake kwa ulimwengu na vilevile kuanzisha kambi madhubuti ndani ya Mashariki ya Kati ili kupigana dhidi ya ‘ugaidi’ vita ambavyo kimsingi vilipangwa dhidi ya Ummah wa Kiislamu. Amerika iliua mamilioni ya Waislamu nchini Iraq na kuiangamiza nchi hiyo, hata kuisababishia kusambaratika.

Marais watatu wa Amerika, George Bush, Barrack Obama, na Donald Trump waliongoza vita hivi kwa kueneza ugaidi wa kikatili huku wakionyesha kusita dhahiri kutangaza malengo yao. Upeo wa matukio kama hayo ya kigaidi uliendelea hadi zaidi ya ardhi ishirini za Kiislamu hadi Amerika mwishowe ilifikia hitimisho kwamba haitaweza kuvunja upinzani wa Mujahidina wa Afghanistan au serikali bandia ya Afghanistan haitaishi bila msaada wa Amerika na NATO. Kwa hivyo, kwa mtazamo wa jeshi, Amerika na NATO walipata kushindwa dhahiri nchini Afghanistan; ndio sababu waligeukia kulinda hadhi yao ya kiulimwengu kupitia mbinu ya mazungumzo ya amani na Taliban. Walakini, ahadi za uhuru, demokrasia, ujenzi wa taifa, haki za binadamu, haki za wanawake, na ujenzi upya wa Afghanistan ziliimbwa sana katika Kongamano la Bonn na makongamano mengine mtawalia ya kikoloni, baada ya miaka ishirini ya ugaidi na mateso, Amerika inarudi mwanzoni kabisa.

Uvamizi wa Amerika na NATO wa Afghanistan pamoja na nia yao mbaya ya ukoloni pia ililenga kutoa ushawishi juu ya akiba ya haidrokaboni ya Bahari ya Caspian, ikisafirisha rasilimali hizi kutoka Asia ya kati kwenda Asia ya kusini, ikishinikiza kuzidhibiti China na Urusi na mwishowe kuzuia kuibuka kwa Dola ya Kiislamu (Khalifah) katika eneo hilo.

Kama Richard Dannatt, Mkuu wa zamani wa Jeshi la Uingereza na mshauri wa Waziri Mkuu wa Uingereza wakati huo, katika mahojiano na Redio 4 ya BBC, alipothibitisha kwamba, “Vita vya Afghanistan vinalenga kuzuia kuanzishwa tena kwa Dola ya Kiislamu (Khilafah)”. Alipoulizwa juu ya uvamizi wa Afghanistan, alisema: “kuna ajenda ya Kiislamu ambayo ikiwa hatutapinga na kuisafisha huko kusini mwa Afghanistan, au Afghanistan, au kusini mwa Asia, basi kusema ukweli ushawishi huo utakua. Inaweza kukua vizuri, na hii ni hatua muhimu, tunaweza kuiona ikihamia kutoka Asia kusini kwenda Mashariki ya Kati hadi Afrika ya Kaskazini, na hadi kilele cha juu katika Khilafah ya Kiislamu katika karne ya 14 na 15.”

Miaka ishirini iliyopita, kila mtu alishuhudia jinsi Amerika, kama dola kubwa, ilipanga njama ya kuwaunganisha viongozi wa ulimwenguni, pamoja na watawala wa nchi za Kiislamu, kwa kisingizio cha ajenda ya ‘vita dhidi ya ugaidi’ kukandamiza Uislamu na Waislamu. Kwa sasa, uongo wa miaka ishirini wa Amerika umedhihirishwa kwani vita vya Amerika vimepoteza uhalali, hata kuvunja kanuni na sheria za ubepari na demokrasia. Kwa hivyo, Amerika inajaribu njama yake mpya ili kuhakikisha uwepo wake nchini Afghanistan. Kwa kweli, Amerika imekusudia kuondoa askari wake wa kijeshi kutoka Afghanistan. Lakini inasukuma kudumisha uwepo wa nguvu kwa muda mrefu nchini Afghanistan kwa kuimarisha ushawishi wake wa kijasusi, kisiasa na kithaqafa nchini humo pamoja na uwepo wa kijeshi katika eneo hilo.

Kwa hivyo, kufichuliwa kwa uongo wa Amerika kumedhoofisha hadhi ya Amerika machoni mwa umma, ikionyesha kuwa Amerika na Uingereza iliyopo sasa sio Amerika na Uingereza walivyokuwa miaka ishirini iliyopita na kwamba ulimwengu wa Magharibi hauwezi tena shughulikia shida za wanadamu, maumbile na ulimwengu. Ndio sababu, Waziri wa zamani wa Kigeni wa Amerika, Hillary Clinton aliiambia CNN bila wasiwasi wakati akizungumzia kujiondoa kwa wanajeshi wa Amerika kutoka Afghanistan kwamba, “Hili ndilo tunaloliita tatizo baya.” Aliongeza kuwa “kuna matokeo ambayo yalitarajiwa pamoja na kutodhamiriwa ya kukaa na kuondoka.” Vinginevyo, Umma uliopo umebadilika sana ikilinganishwa na miaka ishirini iliyopita. Ingawa watawala wasaliti na tawala ovu bado zinatawala ardhi za Kiislamu, mawimbi ya mapinduzi ya kisomi na kisiasa katika jamii, na kugeuza mada ya kuanzishwa tena kwa Khilafah kuwa moja ya maswala yanayotafutwa sana katika nyakati hizi. Kwa hivyo. Lazima tuongeze kiwango cha uchaji Mungu wetu kwa kuamini kikamilifu Nussurah (msaada) ya Mwenyezi Mungu (swt) na kupigania mabadiliko ya kimsingi miongoni mwa Ummah na pamoja na Ummah kwa pamoja.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Saifullah Mustanir

Mkurugenzi wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Afghanistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu