Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Covid-19: Je Inaweza kuwa ni Udanganyifu Mkubwa Zaidi ili Kudhibiti Utawala?

Propaganda ya serikali za ulimwengu imewazamisha watu kwenye COVID-19. Hofu iliyoenea imewafunika watu akili zao na zimedumu kushughulishwa katika kupambana na maambukizi ya COVID-19. Mkuu wa UM ameikadiria kuwa ndio janga baya zaidi kuwahi kutokea tangu Vita vya Pili vya Dunia. Katika kuchunguza homa ya mafua na mkondo unaopelekea maradhi hayo (Influenza Led Ilness) katika muongo uliopita na mipango na sera za serikali zinazo zunguka maambukizi haya, COVID-19 huenda ikawa ni udanganyifu mkubwa zaidi ili kudhibiti utawala kiulimwengu!

Shirika la Afya Dunia (WHO) linaeleza kuwa kesi za maradhi ya homa ya mafua ni takriban milioni 3-5 kwa mwaka zinazo pelekea vifo kiasi ya 250,000 hadi 500,000. Kifua kikuu katika mwaka 2016 kilisababisha vifo milioni 1.3 [1]. Njaa ni sababu kubwa zaidi ya vifo vinavyo uwa watu wengi kuliko UKIMWI, kifua kikuu na malaria kwa pamoja, vinauwa watu milioni 9 kila mwaka [7].

Vifo vya homa ya mafua vya msimu wa (Disemba-Machi) nchini Amerika vinafikia wastani wa 25,470 kwa mwaka kutoka msimu wa mafua wa 1976-77 hadi 2002-03 [8]. Katika msimu wa mafua wa 2017-2018 pekee, Amerika ilishuhudia kesi za kiwango cha juu zaidi zikisababisha hospitali kushindwa kuhimili na kesi za mafua, na idadi ya vifo kufikia 61,099 miongoni mwao 50,903 walikuwa rika la umri wa zaidi ya miaka 65 [9]. Uchunguzi wa 2019 katika chapisho la Lancet limekisia kiwango cha wastani cha vifo vya kila mwaka vya homa ya mafua nchini China vilikuw 88,100 na asilimia 80 ya vifo hivi vilitokea rika la umri wa miaka 60 na zaidi [10]. Italia ilishuhudia vifo 68,000 katika misimu ya baridi katika kipindi cha 2013-14 hadi 2016-17 [11]. Katika utafiti huu, idadi kubwa ya vifo nchini Italia vilinasibishwa na idadi kubwa ya raia wazee wanaoishi huko.

Kiwango cha vifo vinavyo tokana na homa ya mafua pia imeathiriwa na mambo kama uchafuzi wa mazingira na kukosekana huduma bora za afya zilizopo nchi humo. Italia imerikodi kasi kubwa zaidi cha vifo kutokana na homa ya mafua kutokana na kiwango cha juu cha uchafuzi wa mazingira katika miji [14]. Kiwango cha juu cha uchafuzi wa mazingira kimehusishwa na ufanisi mdogo wa mapafu na visa vingi vya magonjwa sugu ya upumuaji kama Pumu. Watu kama hao wamekuwa ni wahanga wa homa ya mafua ya msimu ikiambatana na kasi kikubwa cha vifo. Ujerumani ina vitengo vya wagonjwa mahututi mara 2.5 zaidi ya Italia [15]. Huduma hizi pia zimeonekana kuchangia katika kupunguza kasi ya vifo katika baadhi ya nchi.

Katika waraka uliochapishwa hivi karibuni mnamo Machi 2020, kiwango cha vifo vya virusi vipya vya Korona imeonyeshwa kutokuwa na tofauti sana na aina iliyopo ya virusi vya Korona [13]. Zaidi ya hayo hofu na wasiwasi ulioletwa na vyombo vya habari katika miezi michache iliopita imesababisha kunakiliwa kwa takwimu sahihi zaidi au hata kuongezwa chumvi unakili kwa idadi kupitia kunasibisha uwepo wa virusi hivi wakati wa kifo kuliko mazingira halisi ya vifo kama ilivyo semwa na Daktari Sucharit Bhakdi katika barua yake kwa Chansela wa Ujerumani [2].

Kwa mujibu wa nukta hizo za juu, ni wazi kuwa COVID-19 haiko tofauti sana na mazingira ya homa ya mafua ya muongo mmoja uliopita. Homa ya mafua (almaarufu Flu) au Maradhi yanayo pelekea Homa ya Mafua (hasa ile yenye kubadilisha hali ya upumuaji) ni yenye kuambukiza kupitia kugusa na kuchangamana, na yana kiwango cha juu cha vifo kwa watu wazee mithili ya COVID-19. Endapo COVID-19 itawasha mfadhaiko, basi mtindo unaohusiana na homa ya mafua katika muongo uliopita unaonyesha kuwa mfadhaiko ulipaswa kuanza muda mrefu uliopita kwa maambukizi ya kila siku, mwezi na hesabu ya vifo kama COVID-19. Ili kuuweka muktadha huu, uchunguzi ufuatao unaweza kufanywa kuhusu mazingira yanayoizunguka COVID-19:

1. Shirika la Afya Duniani (WHO) lilikuja na ripoti mnamo Novemba 2019 kuhusiana na haja ya kufikia masoko mapya ya chanjo nayo ni Brazil, India, Pakistan, Uhabeshi, Nigeria na Ufilipino [3]. Ripoti za WHO za miongo iliyo pita zimeregea kukiri haja ya kupambana na athari za homa ya mafua kupitia chanjo mpya! Propaganda ya kiulimwengu ya COVID-19 umetilia mkazo zaidi utekelezaji imara wa upimaji, utoaji chanjo na kuripoti mifano kutoka nchi nyingi ambazo vyenginevyo zimethibitisha kuwa ni changamoto kubwa kwa chumi chache zilizo jihusisha na huduma za afya na bidhaa za madawa.

2. Zoezi la kiwango cha juu la kukabiliana na majanga lilifanywa na Kituo cha Johns Hopkins kwa ushirikiano na Jukwaa la Uchumi la Ulimwengu na Taasisi ya Bill na Melinda Gates mnamo Oktoba 2019 jijini New York. Zoezi hili lilikusudiwa kuelezea ushirikiano unaohitajika baina ya serikali, taasisi za kimataifa na sekta binafsi mbali mbali wakati wa kukabili ueneaji wa maambukizi. Mandhari ilitumia janga lililoibuka nchini Brazil (katika nusu ya Kusini ya Dunia) na kuenea kote ulimwenguni na kuathiri mamilioni ya watu. Zaidi ya hayo, Mkutano wa Jukwaa la Takwimu wa Hazina ya Fedha ya Kimataifa (IMF) mnamo Novemba 2019 uliitishwa ili kutathmini Uchumi Usio rasmi wa nchi zinazo endelea ambapo baadhi ya wakati huwa zaidi ya asilimia 90. David Lipton katika tamko lake la ufunguzi alitaja moja ya malengo kwa ajili ya kupima uchumi usio rasmi kama kutathmini uhimili wa deni na kutumia kanuni za kodi [5]. Zuwio la dharura kwa watu majumbani ni miongoni mwa hatua muhimu zinazo tumika kudhibiti maambukizi ya COVID-19 na ilitazamiwa kusukuma uchumi rasmi kwenye mdororo na kuumiza uchumi usio rasmi kwa kiasi kikubwa kote duniani. Pia ilimaanisha kuchangamsha mipango ya kuhuisha uchumi wa nchi zilizo athirika na ni lazima ukadiriwe na upimwe kudhibiti mporomoko, hasa katika mataifa yaliyo chini ya jangwa la sahara na Asia. Inaweza kuelezwa kuwa tathmini ya warsha ya Kituo cha Johns Hopkins ilitoa muongozo juu ya kudhibiti COVID-19, huku kongamano la Jukwaa la Takwimu la IMF likitoa sababu za kupelekea zuwio la dharura la watu majumbani na kuchangamsha usimamizi uliosukumwa na COVID-19. Ingawa tofauti ni kuwa COVID-19 iliibuka kutoka China (katika nusu ya kaskazini ya dunia) na kuenea kote ulimwenguni. 

3. Mfumo wa Dunia uliopo kwa sasa umeitumia COVID-19 kutabikisha mipangilio yake iliyopo kwa sasa ya mipangilio mipya iliyo pangwa ya udhibiti. Kifurushi cha kusisimua uchumi cha dolari trilioni 5 kinategemewa kurithi sera mpya za hatua za udhibiti kwa kuzingatia biashara na uchumi mbali na huduma za afya. Pia kuna msukumo katika kutekeleza upelelezi wa kidijitali kudhibiti COVID-19. Aina mbali mbali za matumizi ya programu za kompyuta zimetolewa na serikali ambazo zimeingilia faragha za raia wao kupitia kuhalalisha ukusanyaji wa data ili kudhibiti COVID-19. Ni suala linalotarajiwa kuwa teknolojia hizi zitadumishwa matumizi yake baada ya COVID-19.

4. Hata kabla ya mashambulizi ya chombo cha habari chenye hasira za chuki na Uislamu cha India dhidi ya kundi la Jamaat Tabligh, kulikuwa na jaribio la kuhusisha ueneaji wa COVID-19 na Uislamu. Ripoti huru ya Machi 19 katika makala ilitaja kuwa tabia za kitamaduni katika jamii za Waislamu, kama sehemu ya Uislamu, ni zenye kwenda kinyume na kile ambacho serikali inashauri ili kuzuia ueneaji wa COVID-19. Matendo mengi ya Kiislamu kama kupeana mikono, kukumbatiana, swala za jamaa, familia pana na maziko ya Waislamu yenye mikusanyiko yanahusishwa na ueneaji wa COVID-19 [6]. Hii inaelekea kuwa ni kwa makusudi ili msemo uliopo wa Vita dhidi ya Ugaidi udumishwe na sio kuuliwa na COVID-19.

5. Vifo vya hali ya juu milioni 9 vya njaa huenda vikawa ndio janga baya zaidi na kwa kweli ndio inayodhaniwa kuwa sababu halisi ya kuzingatiwa kote ulimwenguni [7]. Watetezi wanaopigana na COVID-19 kama UM, Amerika, Ulaya, India, China wote wameangazia kuhusu kuokoa kila nafsi kutokana na COVID-19, takriban wote wamekuwa viziwi juu ya njaa na umasikini vinavyo uwa kiasi cha watu 25,000 kwa siku! Unafiki uliofungamana na mataifa haya unahakikisha tu silaha ya maambukizi waliojipamba nayo huku wakificha nia zao mbaya.

6. Kichocheo cha dolari trilioni 5 kinachoongozwa na Amerika kina uhakika wa kuweka muundo wa matumizi yake katika miaka inayokuja kote duniani. Inatarajiwa sana kuwa kuinuka kwa uchumi baada ya COVID-19 kutavisongeza mbele vita vya kibiashara pamoja na China kuwa vikubwa zaidi. Hata hivyo, tokea mwanzoni mwa Machi 2020, China imejitoa mtoaji mkubwa wa madawa duniani kwa kiasi cha dolari bilioni 1.4 [16]. Lakini iwapo msimamo utabadilika karibuni kwa China itaonekana.    

7. Utafiti wa PEW uliofanywa mnamo Februari 2020 unaonyesha kuwa kuna ongezeko la watu kutoridhika na demokrasia katika muongo uliopita na liko katika kiwango cha chini zaidi ya 50% [13]. Mwaka wa 2019 ulishuhudia idadi kubwa ya maandamano eneo la Mashariki ya Kati, Afrika, Asia, na nchi za Ulaya. Uzuiaji rasmi wa watu majumbani umezipa serikali hizi afueni katika kukabiliana na maandamano na kurefusha umri wa Demokrasia kama nidhamu ya serikali juu ya watu.

Hivyo, imethibitishwa kuwa homa ya mafua ya kawaida na Maradhi Yanayo pelekea Homa ya Mafua yanayo tokea kila mwaka kote duniani, huja chini ya uchunguzi mkali na uangalizi wa serikali na vyombo vya habari kama Covid-19 ili kuendeleza malengo kadha wa kadha na kudhibiti utawala kiulimwengu.

Hitimisho

Muundo wa kiuchumi na kisiasa wa dola ya Khilafah utahakikisha yafuatayo:

1] Dola ya Khilafah haitawali kwa udanganyifu. Mtume (saw) amesema:

«مَا مِنْ وَالٍ يَلِي رَعِيَّةً مِنْ الْمُسْلِمِينَ فَيَمُوتُ وَهُوَ غَاشٌّ لَهُمْ إِلَّا حَرَّمَ اللَّهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ»

“Pindi mtawala yeyote atakapokuwa na mamlaka kuwatala raia na akafa hali akiwa mwenye kuwadanganya, Mwenyezi Mungu ataiharamisha Pepo juu yake” Nafasi ya utawala ni amana, hivyo watawala humuogopa Mwenyezi Mungu (swt) katika kutekeleza majukumu yao kwa watu.

2. Dola ya Khilafah huchunga mambo ya watu na hulenga katika huduma sahihi za afya. Dola hii haitoliangalia janga la maradhi ya maambukizi kama fursa ya kiuchumi, lakini badala yake italenga mara moja juu ya hatua za kujikinga. Dola hii itatenga fedha moja kwa moja kwa lengo la kutafuta matibabu halisi na sio kama uwekezaji unao ahidi mapato mazuri.

3. Ni wazi kuwa njaa ni “janga” baya zaidi kuliko COVID-19 au maradhi mengine yoyote. Ikiwa ndio sababu inyo ongoza ya vifo duniani, hii itakuwa ndio kipaumbele cha dola ya Khilafah. Muundo wa kiuchumi wa Dola ya Khilafah utazingatia zaidi juu ya usambazaji kuliko uzalishaji, utawezesha kufikia vifo sifuri vitokanavyo na njaa kwa urahisi zaidi. Uthman ibn Affan ameripoti: Mtume, rehma na amani zimshukie, amesema,

«لَيْسَ لِابْنِ آدَمَ حَقٌّ فِي سِوَى هَذِهِ الْخِصَالِ بَيْتٌ يَسْكُنُهُ وَثَوْبٌ يُوَارِي عَوْرَتَهُ وَجِلْفُ الْخُبْزِ وَالْمَاءِ»

“Hakuna haki kwa mwanadamu isiokuwa katika vitu hivi: nyumba anayoishi, na nguo ya kuhifadhi uchi wake na kipande cha mkate na maji.” [Tirmidhi]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Abdul Fattaah ibn Faruuq

#كورونا             #Covid19    |        #Korona

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumanne, 21 Aprili 2020 11:52

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu