Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mufti Samigullin Anajidhalilisha Mwenyewe

Mufti wa Tatarstan Kamil Samigullin ameeleza kuwa hakutoa kauli zozote dhidi ya marekebisho ya Katiba ya Urusi yaliyo jumuisha fahamu ya “watu wenye kuunda Serikali”, ila alionyesha tu shaka kuhusu maneno yake, Idara ya Usimamizi wa Masuala ya Kiroho ya Waislamu wa Tatarstan (SAM) imeripoti.

“Nikizungumzia kiujumla kuhusu mabadiliko ya katiba yaliyo fanywa na Raisi Vladimir Putin, ninachangia mengi yao na pia nitayaunga mkono. Zaidi ya hayo tunaona jinsi gani Vladimir Vladimirovich alivyo jizatiti katika kuhuisha mambo ya kiroho, akiunga mkono juhudi za imani za kiasili. Sasa, kuhusu “watu wenye kuunda Serikali”. Nilionyesha shaka kuhusu maneno yake. Bila shaka, kunapaswa kuwepo na hadhi maalum kwa lugha ya Kirusi kama lugha ya dola. Je, serikali inapaswa kueleza na kulinda maslahi ya watu wa Urusi – bila shaka inapaswa, kwani hawa ni sehemu kubwa ya watu waishio katika nchi yetu. Pia labda, ingekuwa vizuri kutumia tasnifu hii katika katiba: “Kuonyesha matakwa ya watu wa kimataifa wa Shirikisho la Urusi na watu wa Urusi”. Mtazamo kama huo unaweza kutilia mkazo utaifa wa kimataifa wa dola na dori yake maalum katika hatma ya watu wa Urusi” – Mufti alielezea msimamo wake.

Tunazungumzia kuhusu pendekezo la Putin la kurekebisha Katiba ya Urusi na kuiingizia ndani yake jukumu maalumu la raia wa Urusi kama la ujenzi wa taifa na kuendelea kwa Shirikisho la Urusi kuhusiana na USSR, pamoja na uaminifu na kutogawanyika kwa Urusi. Yaani, mamlaka za Urusi zinatangaza rasmi na wazi kuwa hii ni Urusi – “huu ni ulimwengu wa Urusi”, hii ni serikali kwa ajili ya watu wa Urusi, huku mataifa mengine yaliyo bakia yakitakiwa kukubaliana na hilo na kuridhia, Wakati huo huo, maafisa kama hao, wakiwakilishwa na viongozi rasmi wa kidini wa Kiislamu, kama vile Mufti wa Tatarstan Kamil Samigullin, mwenyekiti wa Idara Kuu ya Usimamizi wa Masuala ya Kiroho ya Waislamu wa Talgat Tadjeddin, akitoa wito wa kukubaliwa hili na kujisalimisha, akiwasihi Waislamu wajitambue kuwa ni sehemu ya huu “Ulimwengu wa Kirusi”, waitumikie na kujivunia. Yaani, wautambua uhalali wa mvamizi huyu, aliyezichukua ardhi za Waislamu na kusimamisha sheria za kikafiri huko, na pia kutii mamlaka ya Kanisa la Othodox la Urusi. 

Kwa bahati mbaya, tunasikia kauli kama hizi kutoka kwa wanaoitwa  “Viongozi wa Kiroho” wa Waislamu, ambao badala ya kuwa walinzi wa Uislamu na Waislamu,  kinyume chake, wako mbioni kuwalinda maadui wa Uislamu na Waislamu, wakipishana baina yao katika kuhalalisha  ukatili wao. Na hili ni moja tu ya matokeo ya takriban miaka 500 ya uvamizi dhidi ya Waislamu wa Tatarstan na Mkoloni wa Kirusi. Zaidi ya hayo, ndio uvamizi mrefu zaidi katika historia ya Ummah wa Kiislamu. Tangu 1552, kwa mujibu wa kalenda ya Miladia, kuanzia kipindi ambacho Kazan ilitekwa na vikosi vya Moscow Tsar Ivan the Terrible, Waislamu wa Kazan wamekuwa chini ya uvamizi, na hadithi ya majanga yao ilianzia: mauwaji ya halaiki, kufukuzwa nchi kwa lazima, kubatizwa kwa nguvu. Tokea hapo, uingizwaji wa lazima katika ukristo umekuwa ukifanyika, matokeo yake hata tabaka la kipekee lilizuka – Matatari waliobatizwa, ambao kwa badali ya kuritadi kwao waliokoa maisha yao, mali na hadhi zao.

Matatari Waislamu waligoma kutawaliwa na kubatizwa kwa nguvu, walianzisha uasi na harakati za kizalendo za mapambano zikiongozwa na Maimamu na Wanazuoni. Upinzani huu ulikandamizwa kikatili, lakini upinzani uliendelea. Matokeo yake, Malkia Catherine II aliandaa mbinu: aliwaruhusu Waislamu wabaki Waislamu, wafanye ibada ya swala na hata kujenga misikiti mipya na kuirekebisha ya zamani ilioharibiwa na Warusi, lakini wakati huo huo watambue uraia wa Urusi na kutambua sheria za Urusi. Alizuia ubatizwaji wao wa nguvu na hata kuunda “serikali ya kiroho ya Waislamu”, ambayo mfuasi wake ni Kamil Samigullin, ili kuwatawala, kuwadhibiti Waislamu na kuwatumia kwa maslahi yake kupitia viongozi wa kidini walio teuliwa naye.

Tangu 1917, baada ya Wakomunisti kushika hatamu, ambao hawakutambua uwepo wa Mwenyezi Mungu na kuichukulia imani kwa Mwenyezi Mungu kuwa ni “ulevi”, hatua ya pili ya ukandamizaji dhidi ya Waislamu ilianza kwa kutotambua kwao upagani. Ulikuwa ni mzunguko wa pili wa mauwaji ya halaiki, kuwafagia watu kuanzia waumini, wahubiri na wanasayansi, kwa kutotambua kwao sheria za mtu yeyote isipokuwa sheria za Mwenyezi Mungu. Kilikuwa ni kipindi cha uhamishwaji kwa nguvu, ufurushwaji nchi, na vifo vya polepole ndani ya kambi za Gulag.  Wote walio kataa walitangazwa kuwa ni “maadui wa watu”, “wapinzani wa Usovieti” na walipigwa risasi, au kuwekwa katika Gulag kwa miaka 25. Wakati huo huo misikiti ikageuzwa mazizi ya ng'ombe au mashamba ya nguruwe, au vilabu vya kitamaduni na burudani. Waislamu walificha imani zao, wakiswali kwa siri. Alfabeti ziligeuzwa kutoka Kiarabu hadi Kilatini, kisha ghafla hadi kugha ya Slavik, kwa hivyo vizazi vilivyo fuatia vikatengwa na turathi ya Uislamu wa Matatari na fasihi ya Kiarabu.

Lakini Waislamu, hata katika hali hii, walipinga kwa kadiri walivyo weza, mfano “mapinduzi ya pande mbili” yalio tokea mnamo 1920, au mapinduzi ya “mwewe mweusi”, ambayo yalizimwa kikatili.

Baada ya kuanguka kwa USSR, Waislamu hawakubaki bila ya maonevu kwa muda mrefu. Kuanzia mnamo 1995, mauaji ya halaiki ya wa Wachechen yalianza, na baadaye – maonevu dhidi ya Waislamu chini ya kisingizio cha “kupigana na ugaidi”. Na hadi hivi leo, chini ya miito ile ile ya “vita dhidi ya siasa kali na ugaidi”, maonevu dhidi ya Waislamu yameendelea na kuongezeka: sehemu nyengine wanauliwa chini ya kisingizio cha “kummaliza gaidi aliye jihami kwa silaha”, sehemu nyengine wanapelekwa gerezani, wanarushiwa silaha au hata kufunguliwa mashtaka batili ya kujaribu kufanya mapinduzi, kuchukua madaraka, na jaribio la shambulizi la kigaidi. Wasichana wanakatazwa kuvaa hijab shuleni na vyuo vikuu vikuu. Chini ya kisingizio cha “siasa kali”, vitabu vya Kiislamu vimepigwa marufuku, misikiti imefungwa kwa visingizio kadha wa kadha.

Hivyo, kuvunjwa heshima ya Waislamu wa Tatarstan na eneo zima la Volga na hali yake ya sasa ni kutokana na takriban miaka 500 ya kutawaliwa, mauaji ya halaiki, ufurushwaji, ufukuzwaji, kutenganishwa na Uislamu, kugeuzwa kuwa wakristo, na wakomunisti, licha ya hayo Waislamu hawakukata tamaa, walipinga,  wakijaribu kujiweka huru, kujihifadhi mwenyewe, dini yao, tamaduni zao, maadili na lugha yao. Licha ya kukaliwa huko, wakati Khilafah ilipo kuwa, Waislamu waliweka matumaini yao kwayo, wakiiomba na kutegemea msaada  kwayo, wakimzingatia Khalifah kuwa ni Imam na mtawala wao, wakiizingatia Istanbul kuwa ni mji wao mkuu, wakijizingatia kuwa wao ni raia wake, na mara nyingi  wakienda huko ili kuhifadhi dini yao.

Lakini kwa miaka 99 sasa, baada ya kuangamizwa Khilafah, Waislamu wa ardhi zetu, na sio wao tu, hawana sehemu ya kufanya hijra, hakuna yeyote wa kumtegemea kwa msaada na ulinzi. Na mamlaka za Urusi zinaweza kutufanyia chochote wanachotaka bila ya hofu kabisa. Wanajaribu kutushawishi kwamba sisi ni Warusi na hatupaswi kuutumikia Uislamu na Waislamu, bali tuitumikie Urusi. Na Mufti Samigullin, anajidhalilisha mwenyewe, yuko upande wa mkoloni na anamsaidia kuwabebesha watu wetu “fikra ya manku”.

Ni Khilafah pekee inayoweza kuwakomboa watu wetu kutokana na dhulma hizi zote na kuichukua dini yetu chini ya ulinzi wao. Hivyo, tunawasihi watawala na wanaomiliki nguvu katika hitajio la kutoa nusra ya kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa chama cha Hizb ut Tahrir, ambacho kimebeba jukumu hili kubwa kwa takriban miaka 70 sasa. Asema Mwenyezi Mungu mtukufu:

 (يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَنصُرُوا اللَّهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ)

 “Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu”. [47:7]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Shaikhetdin Abdullah 

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 26 Aprili 2020 09:10

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu