Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Njia ya Kufikia Viwango vya Juu vya Iman:

“Tumuabudu Mwenyezi Mungu kama Ambaye Tunamuona”

(Imetafsiriwa)

Mwenyezi Mungu amewaneemesha waja wake kwa neema nyingi zisizohesabika, kubwa zaidi ni neema ya Uislamu ambayo kwayo aliukirimu Umma wa Mtume wake mpendwa Muhammad (saw), na ambayo alimteremshia ili kuieneza katika walimwengu kwa uongofu na rehma. Yeye, (saw), alitimiza amana na kuuacha Ummah wake taifa bora zaidi linaloongoza watu kwa wema na kueneza rehma kwao, lakini hali yake ilibadilika na kuwa mkia wa mataifa; ambao eneo lake linaporwa, utajiri wake kufujwa, na heshima yake kukiukwa, baada ya dola ya Khilafah ambayo iliulinda na kuuhami dhidi ya maadui kuvunjwa.

Karne imepita tangu kubomolewa kwa ngome hii, miaka mia moja imepita tangu Uislamu kutengwa kutoka katika maisha ya Waislamu. Miaka mia moja na Waisilamu wanaishi kama "wafu", kama vile Mtume wao (saw) alivyowaita, iliondolewa kutoka kwa maisha yao.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَجِيبُواْ لِلّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُم لِمَا يُحْيِيكُمْ﴿

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal: 24]. Na zililazimishwa juu yao sheria zilizotungwa na wanadamu ambazo zilitawala maisha yao kulingana na mfumo wa kiulimwengu wa kirasilimali ambao ulibadilisha na kuuondoa mfumo wa Kiislamu. Je! Waislamu wataridhika na maisha ambayo dini yao imetengwa na hukmu zake zimevurugwa?!

Mfumo wa kirasilimali umefanya kazi kuwaeka mbali Waislamu na Mola wao, kumwabudu katika sehemu na misimu, na kujikaribisha Kwake katika hukmu fulani pekee. Kwa fahamu zake fisidifu zilizojengwa juu ya maslahi na manufaa, uliweza kuiunda ibada yao kwa njia inavyotaka na kulingana na yale ambayo hadhara yake ya Kimagharibi unayoeleza: kutenganisha dini na maisha, kwa hivyo Waislamu wanaomwabudu Mola wao walifungwa katika swala, kufunga, na Hajj, na walianza kuishi kwa hukmu zingine zisizokuwa hukmu Zake ambazo zinatawala maisha yao ya kisiasa, kiuchumi, na hata kijamii na wakatii amri za mfumo huu wa kirasilimali.

Ikiongezewa na mahusiano ambayo yamekuwa ni mafungamano yaliyojengwa kufikia kiwango ambacho yataleta manufaa na maslahi, wakati ambapo vipimo vya Muislamu vya sheria yake, "Halali na Haramu", viliondolewa kutoka kwake, alimuabudu Mwenyezi Mungu bila kumkumbuka maishani mwake na bila kurudi kwenye masuluhisho yaliyotokana na sheria Yake ili kutatua matatizo anayokumbana nayo. Badala yake, alianza kuziona tu sheria zilizowekwa na mfumo wa kirasilimali, ambao umejiweka kama mfumo pekee unaoweza kuendesha maisha, na ulimwengu wote na Waislamu pia wanapaswa kutembea pamoja nao kulingana na fahamu za hadhara yake hadi wajiunga na msafara, au vinginevyo, hawataweza - bila shaka - kutatua kurudi nyuma kwao. Kwa hivyo ilikuuza hilo na kutumia mbinu zake zote, ikiwemo vyombo vya habari na vibaraka kujitokeza kama mkombozi, mrekebishaji, na mwenye fadhili zaidi, ilhali ni kinyume chake! Unawashambulia wao na dini yao na unajitahidi kuwamaliza wao na hadhara yao ya jadi, na kuleta ni tishio kwa uwepo wake  endapo itarudi tena katika maisha.

Magharibi imeanzisha vita vya kimfumo ambavyo kwavyo imehujumu imani ya Umma wa Uislamu katika hukmu za dini yake, vita ambavyo imeuvua ukamilifu wa hukmu hizi ili kuzifunga tu ziwe vitendo vya ibada pekee bila ya mahusiano wala miamala. Ilipanda fahamu zake zenye sumu na kukomesha hukmu zenye harufu nzuri na njema za Uislamu. Ili Ummah ugejeshe ustawi wake na kupona maradhi yake, lazima ichomoe miiba hii na urudi kwenye mti mwema ambao huzaa matunda mazuri. Lazima itupilie mbali fahamu hizi fisidifu na kurudi kwenye fahamu safi za dini yake.

Kumwabudu Mwenyezi Mungu kunamaanisha kutii amri na makatazo yake katika kila kubwa na dogo la maisha yetu: katika uhusiano wetu na Mwenyezi Mungu, nafsi zetu na wengine; Katika swala yetu, kufunga na kusimama, katika kula kwetu, kunywa, na mavazi, katika wema wetu kwa wazazi wetu na kuunganisha kizazi na ujamaa zetu, katika kuamiliana kwetu na majirani zetu, katika kununua na kuuza kwetu, katika biashara zetu na mahusiano yetu, bila kujali anuwai na tofauti zake; tunazunguka mahali ambapo hukmu Zake zinazunguka na kushikamana nazo. Uumbaji na amri zote ni za Mwenyezi Mungu, na Yeye ndiye Mola wetu Mlezi, Muumba wetu na Mlinzi wetu:

آمَنَ الرَّسُولُ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مِن رَّبِّهِ وَالْمُؤْمِنُونَ كُلٌّ آمَنَ بِاللَّهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّن رُّسُلِهِ وَقَالُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ﴿

“Mtume ameamini yaliyo teremshwa kwake kutoka kwa Mola Mlezi wake, na Waumini vile vile. Wote wamemuamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake na Mitume wake. Hatutafautishi baina ya yeyote katika Mitume wake, na (Waumini) husema: Tumesikia na tumet'ii. Tunakutaka maghfira Mola Mlezi wetu! Na marejeo ni kwako.” [Al-Baqara: 285].

Kumuabudu Mwenyezi Mungu ni kumuamini Yeye, kukiri Upweke Wake, na kujitahidi kutomuasi. Tunamuabudu na kushindana kufikia viwango vya juu kabisa vya Iman, kufikia kiwango cha Ihsan. Hivyo basi, Ihsan ni nini? «أَنْ تَعْبُدَ اللَّهَ كَأَنَّكَ تَرَاهُ فَإِنْ لَمْ تَكُنْ تَرَاهُ فَإِنَّهُ يَرَاكَ» “Ihsan ni kumuabudu Mwenyezi Mungu kama ambaye wamuona, na ikiwa basi humuoni hakika Yeye yuakuona.” Hili ndilo lililokuwa jibu la Mtume (saw) wakati Jibreel (as) alipomuuliza juu ya Ihsan. Kwa hivyo Ihsan ni kwa Muislamu kufanya kazi kana kwamba anamuona Mola wake, akisimama mbele ya mikono Yake, akijitahidi katika matendo yake na kuyafanya vizuri na kwa ukamilifu. Muislamu lazima aufunge uhusiano wake na Mola wake wakati wote na kwa kila hali na usikosane kutoka kwake, hata kwa sekunde, kwa kule kwamba Mwenyezi Mungu anamwona na anayatazama matendo yake.

وَتَوَكَّلْ عَلَى الْعَزِيزِ الرَّحِيمِ * الَّذِي يَرَاكَ حِينَ تَقُومُ * وَتَقَلُّبَكَ فِي السَّاجِدِينَ * إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ﴿

“Na umtegemee Mtukufu Mwenye nguvu Mwenye kurehemu, * Ambaye anakuona unapo simamama, * Na mageuko yako kati ya wanao sujudu,*  Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua.” [Ash-Shu’ara: 217-220].

Watafiti wengi na wanachuoni wa Kiislamu wa zamani wameizungumzia mada ya Al-Ihsan, na kuieleza kwa ufafanuzi juu yake na kuifanya kuwa ni jambo la Iman.

Kumuabudu Mwenyezi Mungu kana kwamba unamuona inamaanisha kuwa umuone katika ibada na faragha; umuone katika bishara zako na mahusiano yako; umuone katika kila kubwa na dogo la maisha yako. Hiki ni kiwango cha Iman ikiwa Muislamu atakifikia, basi atakuwa ameinuka kwa nafasi ya juu

هَلْ جَزَاء الْإِحْسَانِ إِلَّا الْإِحْسَانُ﴿

“Ati yaweza kuwa malipo ya ihsani ila ihsani?” [Ar-Rahman: 60].

Kwa hivyo, ikiwa mtu anafanya kwa bora zaidi na anamwabudu Mola wake kwa njia inayomridhisha, basi malipo yake yatakuwa ni radhi ya Mwenyezi Mungu na Pepo Yake, na ni malipo makubwa yalioje! Ni uzuri ulioje kwa mtu kupata kukubalika na kibali kutoka kwa Mola wake kama matokeo ya matendo mema aliyoyatenda! Ni wema ulioje kwa mtu kufanya matendo yake huku akikumbuka hofu ya Mola wake, kumcha Yeye na kutafuta kuridhika kwake! Ni hisia tamu ilioje wakati Muislamu anapofikia safu ya juu kabisa na bora ya waja, na kupokea ujira mzuri kutoka kwa Mola wake!  

فَآتَاهُمُ اللّهُ ثَوَابَ الدُّنْيَا وَحُسْنَ ثَوَابِ الآخِرَةِ وَاللّهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ﴿

“Basi Mwenyezi Mungu akawapa malipo ya duniani na bora ya malipo ya Akhera. Na Mwenyezi Mungu anawapenda wafanyao mema.” [Aal-i-Imran: 148]. Kwa hivyo, hongereni Muhsineen (watendao mema), hongera kwao, mapenzi ya Mwenyezi Mungu kwao, na tunamuomba Mwenyezi Mungu atusajili miongoni mwao na atuongoze kwa kile Anachokipenda na kukiridhia na atufanya tuwe na msimamo katika utiifu kwake.

Je! Ummah wa Uislamu uko wapi leo katika dini yake? Je! Unaishi ndani ya mipaka ya hukmu zake? Je! Ulikubali vipi maisha bila ya kuongozwa na hukmu za Mola wake? Je! Unaishi vipi na sheria za wanadamu na kuachana na sheria za Muumba wake?!

Wako wapi Waislamu kwa kile kinachotendeka leo katika maisha yao? Je! Wanamwabudu Mwenyezi Mungu kama alivyowaamuru? Je! Wanatambua kuwa radhi ya Mola wao na sheria yake imevunjwa na kuondolewa? Je! Wanamcha Mwenyezi Mungu na kumtambua, na huku maadui wanazitusi hukmu za Mwenyezi Mungu na wanamdhihaki Mtume wake? Je! Hawatarajii na kushindania heshima ya kiwango cha juu, na hivyo kufanya kazi kuwa katika Muhsineen?

Uhalisia wa Umma wa Uislamu hufanya iwe muhimu kwa wana na binti zake kufanya kazi ili kutoka katika giza lililowatesa maisha yao na kujikomboa kutoka kwa pingu za mfumo wa kirasilimali ambao uliwaonjesha, na wanadamu wote, huzuni kubwa na dhiki ya maisha. Lazima wamwabudu Mwenyezi Mungu kana kwamba wanamuona, na watambue kuridhika kwake juu yao ikiwa watafanya kazi ya kurudisha sheria na hukmu zake kwa maisha yao na kuzieneza kwa watu wote. Lazima waharakishe mwendo wa kufikia lengo hili tukufu, ili wapate kutoka kwa Mola wao kitakachowafurahisha hapa duniani na Akhera.

Mwenyezi Mungu (swt) asema: ﴾إِنَّ اللَّهَ مَعَ الَّذِينَ اتَّقَوْا وَالَّذِينَ هُمْ مُحْسِنُونَ﴿  “Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kumcha, na watendao mema.” [An-Nahl: 128[. Ibn Katheer asema katika kutafsiri Ayah hii: ﴾إِنَّ اللَّهَ مَعَ الَّذِينَ اتَّقَوْا وَالَّذِينَ هُمْ مُحْسِنُونَ﴿ “Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kumcha, na watendao mema.” Yamaanisha; Yuko pamoja nao kwa maana ya kuwaunga mkono, kuwasaidia na kuwaongoza. Hii ni aina maalum ya "kuwa nao". (Wale walio na Taqwa) maana yake, wanajiepusha na yale yaliyoharamishwa. (na watendao mema.) inamaanisha wanafanya vitendo vya kumtii Mwenyezi Mungu. Hawa ndio wale ambao Mwenyezi Mungu huwatunza, Anawaunga mkono, na kuwasaidia kuwashinda maadui na wapinzani wao.) Je! Kuna uharamu mkubwa zaidi kuliko kuishi bila ya sheria ya Mwenyezi Mungu na hukmu zake kutekelewa katika maisha ya Muislamu? Je! Kuna utiifu mkubwa zaidi kuliko kuhukumu kwa sheria ya Mwenyezi Mungu hapa duniani?

Ili muumini atembee katika njia ya Ihsan katika amali, maneno, na vitendo vyake vyote, ni lazima amuabudu Mwenyezi Mungu (swt), kama Apendavyo na Kuridhia:

وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَمْراً أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ وَمَن يَعْصِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالاً مُّبِيناً﴿

“Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na khiari katika jambo, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapo kata shauri katika jambo lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi hakika amepotea upotofu ulio wazi.” [Al-Ahzab: 36]. Na lazima akumbuke kuonekana na Mwenyezi Mungu Mtukufu katika hali zote, na kuwa na hakika kwamba Mwenyezi Mungu yuko juu ya kila kitu, mtazamaji na Shahidi, na usiokosekana katika elimu Yake uzito wa chembe ndani ya mbingu au ndani ya ardhi. Ikiwa Muislamu atakumbuka hilo, basi atatafuta kuongeza kazi yake na kuinua matakwa na malengo yake na kufanya kusimamishwa kwa dola ya Khilafah itakayotabikisha sheria ya Mwenyezi Mungu kuwa ndio hamu yake kubwa na shughuli yake kuu, kwa hivyo atajitahidi na kufanya kazi na wafanyikazi ili kufikia lengo hilo na kukumbuka kuonekana na Mwenyezi Mungu Mtukufu katika vitendo, harakati na makaazi yake yote.

Muisilamu anapaswa kumwabudu Mwenyezi Mungu kama Yeye Apendavyo, sio kama atakavyo na kutafute hoja dhaifu ili kuhalalisha ukiukaji wake wa hukmu za Mola wake na kupindisha shingo ya nususi za Sharia ili kuafikiana na uhalisi anayoishi ndani yake. Hizi ni athari za hadhara chafu iliyojengwa na kutawala maisha ya Muislamu, na ikawa inayumba kati ya hukmu za dini yake na uhalisia fisidifu wa kimada; ufisadi wa hadhara inayoyaendesha, kwa hivyo anajaribu kuikubali hali halisi. Anawezaje kubadilisha kilicho bora kwa kile kilicho duni? Je! Anawezaje kutoshikamana imara na hukmu za dini yake na kuishika dini yake kama aliyeshikilia makaa ya moto na kutopotoka kwake kwa urefu wa hata ukucha?! Yuko njiani kufikia kiwango cha Al-Muhsineen, bila ya kujali kile kitakachomgharimu.

Yakini ya Muislamu kwamba Mwenyezi Mungu atamuangalia katika matendo yake yote humkinga asiangukie katika vitu vilivyo haramishwa na kumsukuma kujitahidi kuendelea kupata radhi ya Mwenyezi Mungu bila kufanya chochote chengine ila matendo ya utiifu, kuepukana na madhambi na kuyashinda yale ambayo nafsi yake ilimpotosha na yale ambayo Shetani hushawishi. Huushinda uhalisia unaotawaliwa na hadhara ambayo ni adui wa hadhara yake, kwa hivyo anapambana na kupigana na kufanya kazi ili misukumo yake na kushikamana na Kitabu cha Mola wake na Sunnah za Mtume wake (saw):

«يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنِّي قَدْ تَرَكْتُ فِيكُمْ مَا إِنِ اعْتَصَمْتُمْ بِهِ فَلَنْ تَضِلُّوا أَبَداً»

"Enyi watu, hakika mimi nimekuachieni yale ambayo mkishikamana nayo kamwe hamtapotea”. Ili Muislamu awe pamoja na Mola wake katika harakati zake zote, na hukmu za Mwenyezi Mungu ziwe ndio ngome yake isiyoweza kuingiliwa mbele ya vishawishi vya uhalisia, starehe za maisha, na matamanio ya nafsi na ziwe ndio silaha katika vita yake dhidi ya "adui" hadhara ya kirasilimali.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Zeinah As-Samit

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu