Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Athari za Ushawishi wa Kijamii juu y a Waislamu Leo Wanapojitahidi Kuwa Wachaji Mungu (Muttaqeen) Wakati Wa Ramadhan

(Imetafsiriwa)

Ramadhan ni mwezi ambao Mwenyezi Mungu (swt) huwawezesha Waislamu kujitafakari wenyewe kama wana wa Adam kwa kutafuta msamaha kutoka kwa Mola wao na kuweza kuwa mmoja wa Wachaji Mungu, kwani Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

[فَمَن تَابَ مِن بَعْدِ ظُلْمِهِ وَأَصْلَحَ فَإِنَّ اللّهَ يَتُوبُ عَلَيْهِ إِنَّ اللّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ]

“Lakini mwenye kutubia baada ya dhulma yake, na akatengenea, basi Mwenyezi Mungu atapokea toba yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira na Mwenye kurehemu.” [Al-Maida: 39]

Waislamu pia wanajua faida ambazo Mwenyezi Mungu (swt) amewezesha katika kufikia ukamilifu katika ibada zao katika mwezi huu mtukufu kama ilivyosimuliwa katika Hadith na Abu Hurairah (r.a) ambaye alisema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (saw) alisema:

إِذَا جَاءَ رَمَضَانُ فُتِّحَتْ أَبْوَابُ الْجَنَّةِ وَغُلِّقَتْ أَبْوَابُ النَّارِ وَصُفِّدَتْ الشَّيَاطِينُ»

“Pindi inapokuja Ramadhan, milango ya Pepo hufunguliwa na milango na milango ya Moto hufungwa na mashetani fungwa minyororo.” Walakini hali ya Waislamu kutafuta msamaha kutoka kwa Mola wao leo, ambapo Uislamu haupo maishani, inaweza kufupishwa kwa maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu aliyesema;

[وَاللّهُ يُرِيدُ أَن يَتُوبَ عَلَيْكُمْ وَيُرِيدُ الَّذِينَ يَتَّبِعُونَ الشَّهَوَاتِ أَن تَمِيلُواْ مَيْلاً عَظِيمًا]

“Na Mwenyezi Mungu anataka kukurejezeni kwenye ut'iifu wake, na wanao taka kufuata matamanio wanataka mkengeuke makengeuko makubwa.”  [An-Nisa: 27].

Umbali huu ambao Waislamu  wanajikuta nao kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) na Uislamu wao wakati na baada ya Ramadhan inahusiana moja kwa moja na hali isiyo ya Kiislamu ya jamii wanazoishi ambazo zinajulikana kwa sifa ya kufuata matamanio ya mifumo iliyobuniwa na wanadamu na sio matakwa ya Muumba wetu na mfumo wa Uislamu.

Wakati wa kuisoma jamii yoyote, inaeleweka kwa usahihi sio tu kuwa na idadi ya watu wanaoishi katika eneo fulani lakini pia kuwe na mlingano wa maadili na kanuni fulani. Hizi zinazalishwa mara kwa mara na kuimarishwa katika maisha ya kila siku kwa njia ya rai jumla, vyombo vya habari, uchumi, tamaduni, sheria, siasa na kadhalika. Watu binafsi wamo ndani ya eneo hili la nguvu za kijamii ambazo bila shaka zina athari kubwa juu ya jinsi wanavyoutazama ulimwengu na wao wenyewe, na matokeo yake kutamatisha namna wanavyoishi.  

Nidhamu ya kawaida tunayoiona katika jamii za Kimagharibi ni nidhamu ya kiliberali ya kisekula. Kutokana na nidhamu hii, watu binafsi na taasisi za kijamii (serikali) ndio wanaounda fikra na hamasa za kawaida. Fikra na hamasa hizi zinazotawala zina athari ya nguvu kwa watu wote katika jamii kiasi ya kuwa aghlabu wengi wao hatimaye huanza kuzibeba fikra hizi kama zao wenyewe.

Mapungufu katika elimu na utekelezaji wa Waislamu wa dini yao sio jambo la ajali.

Mara nyingi, tunaona Waislamu wakibuni upya mifumo ya tabia za kawaida zilizosawazishwa na kurahisishwa katika jamii. Fauka ya hayo, maswala ya kibinafsi yanaoneshwa mara kwa mara, inaonesha kana kwamba Waislamu wanatarajiwa kushinda vizuizi hivi vya kimuundo kati yao na Uislamu wao kwa kitendo tu cha chaguo huru lisilo na mipaka! Kwa hivyo, wanaangazia tu kasoro kwa watu binafsi kana kwamba mifano hii iko ndani ya ombwe, pasina pia kuwa na majadiliano ya kina juu ya muktadha wao wa kijamii ni usomaji juu juu kuhusu wa tatizo, na suluhisho lolote linalotegemea hali hiyo bila shaka halitakamilika.

Wale wanaosema haya kwa kweli wamechukua mtazamo wa kibepari juu ya jamii kwani wameiangalia jamii kama yenye kujumuisha pamoja tu watu binafsi. Kutokana na hili, wamebeba mtazamo kuwa: ‘Mrekebishe mtu binafsi na kisha jamii itabadilika’. Ukweli wa mambo hata hivyo ni kwamba mabadiliko au marekebisho ya mtu binafsi hupelekea marekebisho ya watu binafsi tu ambapo haina uhusiano wowote na mageuzi ya jamii. Hii ni kwa sababu jamii sio tu ni mkusanyiko wa watu binafsi bali ni watu ambao wana uhusiano wa kudumu ambao huwaunganisha pamoja. Kwa hivyo, kusahihisha mahusiano ndio hupelekea usahihishaji wa jamii. Mahusiano haya ni mkusanyiko wa fikra na hisia ambazo zinalindwa (na kudumishwa) na Nidhamu (serikali). Mwenyezi (swt) ameteremsha:

[إِنَّ اللَّهَ لاَ يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّى يُغَيِّرُوا مَا بِأَنفُسِهِمْ]

“Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo naf- sini mwao.” [Ar-Ra'd 13:11].

Maana ya aya hii sio, kama wengine wanavyoitumia, kuwa mabadiliko hayo hayatatokea katika jamii au kwa watu hadi watu wote wabadilike. Bali, ni kwamba mabadiliko hayatatokea hadi jamii ibadilishe yaliyomo ndani yake ambayo yanajumuisha watu binafsi lakini pia hujumuisha fikra zao, hisia zao na nidhamu yao ndani ya  jamii. Ndio sababu ni muhimu kwetu, ambao tunataka kubadilisha jamii, kuifafanua kwa usahihi.

Kwa hivyo, ikiwa Nidhamu ni ya Kiislamu inayolinda na kuhifadhi fikra na hisia za Kiislamu, itawakilisha jamii ya Kiislamu hata kama watu wake wengi hawakuwa Waislamu. Ikiwa, hata hivyo, nidhamu ni ya kikafiri inayolinda hisia na fikra zisizokuwa za Kiislamu, basi jamii hiyo itakuwa isiyokuwa ya Kiislamu na hata kama wengi wa watu wake walikuwa Waislamu!! Kwa hivyo, rangi muhimu zaidi ambayo hutofautisha jamii ni Nidhamu.

Kwa hivyo kutambua umuhimu ambao mifumo ya wanadamu inao juu ya Waislamu inapaswa kusababisha kwa Waislamu kutambua haja ya sio tu kujitahidi kibinafsi kutafuta radhi ya Mola wao ndani ya Ramadhan hii kwa kusoma maana ya ayat za Qur’an tukufu, kusoma juu ya maisha ya Mtume (saw) na masahaba zake (ra): jinsi walivyoishi maisha yao, jinsi walivyojitoa muhanga maisha yao na viungo vyao kuufanya ulimwengu wa Mwenyezi Mungu (swt) kuwa juu lakini pia kusoma juu ya sheria za mwingiliano katika Uislamu iwe katika biashara, fedha, kilimo au mengine. Hebu natutazame kile ambacho Uislamu unasema juu ya uhusiano kati ya wanaume na wanawake, familia na watoto. Uislamu ni mfumo kamili wa maisha na katika mwezi huu uliobarikiwa, hebu natuweke nia ya dhati kugusia sehemu zingine za Uislamu ambazo hatuna maarifa nazo tunapofanya kazi ya kuleta mabadiliko ya kijamii kutoka kwa nidhamu zilizotungwa na wanadamu hadi kwa nidhamu za Uislamu.

#رمضان_والإحسان

#Ramadan_And_Ihsan

#Ramazan_ve_İhsan
#Ramadhani_na_Ihisan

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Tsuroyya Amal Yasna

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu