Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Barua ya Wazi kwa Naveed Butt, Mashahidi na Wakandamizaji Wake

(Imetafsiriwa)

Ndugu Naveed Butt, msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan hivi sasa ana umri wa miaka 52, ametekwa nyara na mawakala wa utawala wa Pakistan mnamo 11 Mei 2012 kutoka barabara za Lahore mbele ya watoto wake wakati akiwarudisha kutoka shule. Hakuonekana au kusikilikana tokea muda huo wala kushitakiwa kwa kosa lolote au kupelekwa katika mahakama yoyote. Amepotea tu na imebakia hivyo hadi kufikia mwaka wake wa kumi kifungoni.

Ninaandika barua hii ya wazi kwanza kwa kumtukuza Muumba wetu Mwenyezi Mungu (swt) na kujua kuwa Mwenyezi Mungu (swt), Aliye Juu zaidi, Mtukufu, na mstahiki wa shukrani zote hakika Yeye ndiye msimamizi wa mambo yote na kwa hekima zake zisizo na kikomo ni mwenye kujua kwa nini mambo yamekuwa hivi.

Naveed Butt ni msomi na ni mtu mahiri mno. Alikuwa ni mwanafunzi wa uhandisi mwenye kipawa kutoka Lahore aliyetunukiwa msaada wa masomo nje ya nchi katika chuo miongoni mwa vyuo bora zaidi, ambapo hatimaye alianza kwa mafanikio masomo katika tasnia yenye pato kubwa ya teknolojia ya mashirika. Lakini ni katika wakati huu ambapo Naveet Butt alikutana na amali ya kiulimwengu ya kusimamisha Khilafah – mfumo wa utawala wa Kiislamu ambao kupitia kwake sheria zote za Mwenyezi Mungu (swt), ima ziwe za kiuchumi, kijamii, hukmu, sheria, sera za ndani na nje nk., zinazohusiana na jamii huwa zinatekelezwa, hivyo kutimiza maamrisho ya Mwenyezi Mungu (swt) katika Quran:

[فَاحْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللّهُ]

“Basi hukumu baina yao kwa aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu” [Al-Maida: 48].

Huo ulikuwa ni ukweli wa Naveed Butt kwa Uislamu na shauku yake ya kuona ukandamizaji na dhulma – ambazo huja kimaumbile wakati kunapotawalishwa kile kisichoteremshwa na Mwenyezi Mungu (swt) – zitaondoka kutoka Pakistan na nje yake, ndipo alipowacha shughuli yake ya ustawi nje ya nchi na kurudi Pakistan kufanya kazi ya kurejesha mfumo wa Kiislamu wa Khilafah kwa amani, harakati zilizojifunga na siasa bila utumiaji nguvu kama ilivyo Sunnah ya Mtume Muhammad (saw), ambaye mwenyewe alisimamisha dola ya mwanzo ya Kiislamu mjini Madina baada ya miaka kumi na tatu ya mapambano ya amani ya kisiasa mjini Makkah.

Ninatumai na kuomba kwa Mwenyezi Mungu (swt) kuwa ujumbe wa barua hii umfikie Ndugu Naveed Butt, kwani matabaka ya ukandamizaji yanamtenga na familia yake, marafiki na ndugu zake wanaharakati wa kisiasa wanaomheshimu kwa kiwango kikubwa. Ujumbe huu aujaalie uende hadi umfikie Naveed bhai mwenyewe.

Mpendwa Ndugu Naveed, tunakuzingatia kwa mapenzi makubwa na tumeukosa uwepo wako kwetu, hasa katika jitihada zako katika njia ya Mwenyezi Mungu (swt) na hekima zako ulizotuachia, yote haya yakiwa katika shughuli hii kubwa. Tunajua kuwa hujaiona familia yako. Kwa zaidi ya miaka kumi ya maisha yako yamekuwa kifungoni katika gereza la chini ya ardhi tusilolielewa. Huko nao watoto wako. Hawajaona tabasamu lako wala kumbatio la mapenzi ambalo kila mtoto hutamani kuliona na kulihisi. Miaka hii yote hakuna awezaye kuirejesha. Hakuna mtu awezaye kuurejesha muda au kuweka mbadala kwa kile ambacho wewe na familia yako wamekikosa. Unakumbana na kama yale yaliyompata Nabii Yusuf (as) wakati alipofungwa gerezani kwa makosa ya uongo. Malipo yako inshaAllah, yatakuwa katika maisha haya na yajayo.

Kwa wakandamizaji wake – kwa wale waliomteka, kwa wale ambao bila shaka walimtesa, kwa wale ambao bado wamemuweka ndani mbali na familia yake bila huruma yoyote, kwa wale waliosimama kupinga maamrisho ya Mwenyezi Mungu (swt) – endeleeni na uovu wenu wa kumshikilia kifungoni Naveed bhai kwa muda wote mnaoweza kuvumilia kuweka mikono yenu juu ya moto. Tambueni kuwa hiki ndicho mtachokabiliana nacho katika maisha yajayo kwa uovu wenu, bali ukali wake ni mkubwa mara nyingi zaidi. Na kama hamkhofii Akhera, wala adhabu za Mwenyezi Mungu (swt), basi juweni kuwa dola ya Khilafah ijayo itakushikeni na kukuhisabuni kwa maovu yenu. Basi tumieni fursa hii kumuacha huru hivi sasa.

Kwa wale walioshuhudia ambao walimfahamu Naveed bhai au kwa wale wanaojua kifungo chake na bado wakanyamaza kimya juu ya hilo na wasinyanyue hata kidole dhidi ya dhulma hii wala kusema chochote cha haki kudhihirisha hili. Juweni kuwa Mwenyezi Mungu (swt) ameweka juu yenu mtihani huu ili abainishe mko upande gani; wa haki au batili, kwa sababu katika Uislamu hakuna nafasi ya katikati. Wale wanaoona uovu na wasifanye chochote kuupinga, na wana uwezo wa kufanya hivyo, bila shaka wapo machoni mwa Mwenyezi Mungu (swt) wakijikuta wapo katika ushirikiano mmoja kama madhalimu wenyewe na wanastahiki adhabu sawa.

Ujumbe wa mwisho kwa Naveed Butt bhai. Tumekukosa kwa kipindi kirefu. Tunaomba na kukusudia kufungua mlango uliofungiwa – kwani tunajitahidi mchana na usiku kuisimamisha tena dola ya Kiislamu ya Khilafah kwa njia ya Utume (saw) kwa haraka kadiri iwezekanavyo ambayo itatimiza hukmu za Mwenyezi Mungu (swt) na katika mchakato huo kuwakomboa watu wa Pakistan kutokana na ukandamizaji ulioshitadi wanaokumbana nao.

Mwenyezi Mungu (swt) akipenda tunategemea kukuona tena sio tu ukiwa ni mwanaharakati wa kisiasa, bali mara hii ukiwa mwenye heshima na kiongozi muadhamu wa Ummah wa Waislamu katika nafasi ya Amil (Meya) au Wazir (Gavana) wa jimbo la Hind au siku moja pengine kuwa Khalifah mwenyewe. Tunakusudia kwa hili tukiwa Waislamu, tunaweka mategemeo yetu kwa Mwenyezi Mungu (swt) na tukiamini Ahadi yake ya ushindi na kutoa uongozi kwa wale walio na Iman na kufanya matendo mema, kama alivyowapatia walio kabla yetu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Mohamed Asif

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu