Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mpango wa Salahudin wa Kuikomboa Palestina

(Imetafsiriwa)

Salahudin aliyezaliwa 1137 nchini Iraq, aliibuka kuwa maarufu kipindi cha zahama wakati ardhi za Waislamu zilipokuwa zimesambaratika na kuwa chini ya mwavuli wa Makruseda wavamizi. Alipochukua uongozi Misri mnamo 1169, alianzisha misheni ya kuimarisha Dola ya Khilafah na kuunganisha maeneo kadhaa ya Kiarabu. Kwa kutambua umuhimu wa umoja wa Waislamu, Salahudin kwa mkakati maalum, aliviunganisha vijinchi vidogo vidogo vilivyo izunguka Palestina, akiweka maandalizi ya medani iliyoungana dhidi ya Makruseda. Kipindi muhimu katika kampeni ya kijeshi ya Salahudin ilikuwa ni 1187 kwa shambulizi baya dhidi ya msafara wa Waislamu alilofanya Reynold de Chatillon, Mfalme wa Kikristo wa Kerak, aliyekuwa Jordan ya sasa. Tukio hili lilivunja amani iliyopo kwa muda na kumpatia Salahudin fursa ya kutimiliza ndoto yake ya muda mrefu ya kuikomboa Al-Qudsi.

Jitihada za Salahudin za kuunganisha safu za Waislamu zilikumbana na changamoto kubwa kutokana na Makruseda kudhibiti miji ya pwani ya Syria na ngome muhimu kama Kerak na Crac de Montreal, katika eneo la Jordan ya sasa. Ngome hizi zilizuia mawasiliano baina ya Misri, Syria Kuu (maeneo ya Sham), na sehemu za Iraq, mhimili muhimu kwa dola ya Salahudin. Mwanzoni, Imad ad-Deen Zangi [Zenki] aliweka msingi kwa ajili ya umoja kwa kuunganisha Syria Kuu. Urithi huu uliendelezwa na Nur ad-Din aliyeiunganisha Misri na Syria.

Vita vya Hattin vilitanguliwa na msururu wa matukio, ikianzia na kifo cha Mfalme Baldwin V mnamo 582 H. Mivutano ya ndani ilizuka miongoni mwa watoto wa Makruseda wakigombania utawala wa Al-Qudsi. Salahudin alitumia fursa hii ya kukosekana utulivu, akaingilia masuala ya Makruseda. Ndoa ya Guy wa Lusignan kwa Sybille, Mama wa Mfalme Baldwin V, ilimpatia yeye ufalme, jambo lililozusha mivutano baina ya Guy de Lusignan na Raymond III, mgombea mwengine wa ufalme.

Suluhu ya Salahudin na Raymond III, Kiongozi wa Tripoli, eneo la Lebanon ya sasa, na suluhu nyengine na Bohemond III, Kiongozi wa Antioch, eneo la Uturuki ya sasa, ilimuwezesha kuzidhibiti siasa za Mvamizi. Kwa kuufanya upya ushirikiano pamoja na Raymond III na Bohemond III kwa lengo la kimkakati kuzidhoofisha himaya za Tripoli na Antioch. Hili lilimghadhibisha Reynald de Chatillon, Kiongozi wa Kerak, ambaye licha ya suluhu ya awali, alivunja mkataba wake kwa kuingilia msafara wa wafanyibiashara. Muelekeo wa kistratejia ya kidiplomasia ya Salahudin kukabiliana na uvunjaji huu wa mkataba ulizusha kutoaminiana na mgawanyiko baina ya Mfalme Guy na Reynald, na kuweka maandalizi kwa ajili ya Vita vya Hattin.

Salahudin aliitumia fursa hiyo kwa kuunganisha safu za Waislamu na kutayarisha majeshi kutokea Misri, Mesopotamia, Mosul Kusini ya Iraq na Syria. Akiyaelekeza kutoka Damascus mnamo 583 H, na kimkakati akiyapeleka Kerak kuficha lengo lake hasa la kuelekea kwenye Mamlaka ya Al-Qudsi. Hatua hii sio tu ilimtisha Reynald de Chatillon lakini pia ilionyesha ushujaa wa kijeshi na mkakati wa Salahudin. Salahudin al-Ayyubi alitengeneza hatua kadhaa zilizopelekea hatua ya maana zaidi ya Vita vya Hattin.

Ikiwa ni utangulizi wa makabiliano haya, kikosi chake cha upelelezi kilifanikisha ushindi muhimu eneo la Sepphoris linalojulikana leo Galilee, ikitia hofu Makruseda. Salahudin katika kuonyesha kuona mbele kwake, alichagua vita vikali licha ya kutafautiana rai miongoni mwa makamanda wake. Mpango wake ulikusudiwa kutumia migawanyiko katika safu za Makruseda na kutumia kwa faida yake juu ya kifo cha Mfalme Baldwin V kudhoofisha uthabiti wao. Mgawanyiko wa ndani wa Makruseda, muozo wa maadili, na ukosefu wa umoja vilichangia kuanguka kwao. Wakiwa wamekabiliana na kikosi cha Waislamu kilichoungana, Makruseda, wapatao takriban alfu hamsini, walijitahidi kuvumilia.

Salahudin alitumia udhaifu huo, akipata faida ya kistratejia na kuweka mitego ambayo Makruseda walinaswa. Kwa kufahamu umuhimu wa mandhari ya eneo, Salahudin kimkakati aliwasukuma Makruseda kuelekea Tiberias, Galilee ya hivi leo, ikizusha hali mbaya kwao. Makruseda walichoka na kuwa na kiu, waliangukia kwenye mtego wa Salahudin. Kimkakati Salahudin aliyashinda majeshi ya Kikristo, akiepuka makabiliano ya moja kwa moja hadi pale hali ilipokuwa muafaka kwa Waislamu.

Hatimaye, Vita vya Hattin vilipiganwa katika joto kali, ikapatilizwa udhaifu wa Makruseda katika wingi wa silaha na ukosefu wa maji, na kupelekea ushindi mkubwa sana kwa Waislamu. Vita vilivyofuata vya Hattin vilionyesha makabiliano makali, huku vita vya kisaikolojia, mzingiro, na kushikwa kwa Msalaba wa Kweli kuliongeza athari.

Ushindi wa Salahudin katika Hattin ulionyesha Nusra ya Mwenyezi Mungu (swt) aliyowaahidi wale walioshikamana na njia yake. Vita hivi vilidhihirisha mgeuko katika vita vya baina ya Khilafah na Makruseda, iliyopelekea ushindi wa kweli na juhudi zinazofuata kuunganisha Syria Kuu. Mji wa Al-Qudsi, baada ya miaka 88 ya ukaliwaji na Makruseda, ukawa ni mlengwa mkuu wa mpango wa mkakati wa Salahudin. Lengo la mwisho la Salahudin ni kuikomboa Al-Quds (Jerusalem).

Kabla ya kuweka mzingiro wa mji mtakatifu, aliikata Jerusalem kutoka Bahari ya Mediterania, akaitenga. Salahudin alishirikiana na jeshi la majini la Misri kuzuia jeshi la majini la Wakristo kukaribia, akionyesha mbinu yake ya kina ya mkakati wa kijeshi.

Kipaji cha kimkakati cha Salahudin kilichofichuliwa baada ya Vita vya Hattin, kilidhihirishwa kwa kuzingatia kwake miji ya pwani ya Makruseda. Kwa kuyakomboa maeneo ya Tiberias, Akka, Jaffa, Ascalon, Sidon, Beirut, Jubayl na mengineyo, alivunja uwepo wa Makruseda katika maeneo hayo. Ngome hizi za maeneo ya pwani zilizotaabisha tawala za Waislamu kwa muda mrefu zilianguka moja baada ya moja, na kuvunjika ngome za Makruseda. Kwa kuidhibiti miji ya pwani mwanzoni, aliweza kuwanyima Makruseda kambi za majeshi ya majini na hivyo kudhoofisha vikosi vyao, na kuzuia misaada ya Ulaya. Juhudi za nje za kidiplomasia ikiwemo miungano na Konstantinopoli na mikataba ya kimkakati na manuari za Italia, zilizuia uingiliaji wao kwenye himaya za Makruseda.

Mbinu yake ya kimahesabu, kuokoa maisha na mali iliwepesisha wimbi lisilotegemewa la ushindi. Mfululizo huu wa kukomboa uliiweka upya mandhari ya kisiasa na kuwadhoofisha Makruseda, hatimaye ulifikia kilele chake katika kuikomboa Al-Qudsi. Uongozi wa Salahudin ulianzisha zama mpya, ukitoa changamoto za hatua za wakoloni na kuweka msingi kwa ajili ya hatimaye kuwafurusha Makruseda kutoka maeneo hayo.

Wakati Salahudin akisonga mbele kuelekea Al-Qudsi, walinzi Makruseda wa mji walikabiliana na changamoto. Huku kukiwa na wapiganaji Makruseda zaidi ya 60,000 katika Al-Qudsi, matayarisho yalipamba moto wakati vikosi vya Salahudin vikijikusanya. Ngome za mji ziliimarishwa, mangoneli (mashine za kurushia makombora) ziliwekwa kwenye kila mlima, na mahandaki yalichimbwa kujilinda dhidi ya uzingiaji unaotarajiwa wa Waislamu. Umahiri wa kimkakati wa Salahudin ulikuwa wazi katika mpango wake wa kijeshi alioubuni kitaalamu. Alitaka kuunganisha vikosi vya Waislamu, kuwadhoofisha Makruseda katika ardhi yao, na kuitenga Jerusalem katika kupata msaada. Salahudin alikuza kampeni ya uenezaji habari kuwashajiisha Waislamu kwa Jihad. Ukombozi wa maeneo ya pwani na ushindi yaliangazia kukusanya msaada kutoka maeneo yote ya ulimwengu wa Kiislamu. Salahudin aliizingira Jerusalem, mzingiro uliochukua siku 12, wakiushambulia mji hadi Wakristo wakasalimu amri mnamo Oktoba 2, 1187. Silaha bora za Salahudin zilichukua dori muhimu katika kuvunja kuta. Baada ya mapambano makali, Salahudin alikubali kupatana na Balian de Ibelin, Aka Balian wa Jerusalem, kiongozi maarufu wa kijeshi wa Makruseda. Makruseda katika Jerusalem wakakubali kusalimu amri, ikapelekea kuwepo masharti maalum na malipo ya fidia.

Kuingia kwa Salahudin Jerusalem kukadhihirisha ukombozi wa mji. Salahudin akaonyesha huruma kwa kuweka fidia muafaka kwa Makruseda. Alipoingia Jerusalem, Salahudin aliamrisha kujengwa upya kwa mji na kuwa katika hali yake ya awali, akigeuza mabadiliko yaliofanywa na Makruseda. Wakristo waliruhusiwa kukaa, kulipa jizya, na kuishi chini ya hifadhi ya sheria za Uislamu. Alikataa kabisa ushauri wa kuyavunja makanisa. Huruma ya Salahudin ilienea kwa mateka wa Makruseda. Aliwaachilia huru wafungwa na kuonyesha wema, hata kwa familia za wapiganaji walioshindwa wa Makruseda. Vyanzo vya Kikristo na wanahistoria vinakiri juu ya uvumilivu wake wa ajabu na ubinadamu, uliotafautiana sana na uovu uliotendwa na Makruseda hapo nyuma.

Siku nane baada ya kukombolewa, msikiti mtukufu ulitwahirishwa, na swala ya mwanzo ya Ijumaa iliswaliwa. Al Qadhi Muhyi ad-Diin ibn az-Zaki alitoa khutba nzito, akimshukuru Mwenyezi Mungu (swt) kwa ushindi juu ya ukafiri, akasisitiza umiliki Wake (swt) juu ya mambo yote, na kushukuru juu ya neema walizopewa waumini. Khutba ilisisitiza umuhimu wa ukombozi, utukufu wa msikiti, na umuhimu wa kihistoria wa Masjid al-Aqsa. Alihimiza kufuatwa maamrisho ya Mwenyezi Mungu (swt), na kuendeleza jihad kwa ajili ya kuzikomboa ardhi za Waislamu.

Salahudin alitanua ukombozi hadi nje ya Al-Qudsi, akayafika maeneo ya kusini na kaskazini ya Syria Kuu. Ngome za Kerak na Crac de Montreal zilitoa upinzani, na kupelekea mzingiro kwa mwaka mzima. Kusalimu amri kwa ngome hizi kulionyesha hatua muhimu katika juhudi za Salahudin kuimarisha udhibiti wa Khilafah katika eneo. Salahudin baadaye akahamishia nguvu zake kaskazini, akilenga maeneo ya miji ya Tripoli na Antioch. Kukombolewa kwa Tripoli na Antioch kulidhoofisha ngome za Makruseda, na kupelekea suluhu na kutambuliwa mafanikio ya Salahudin kwa maeneo hayo.

Salahudin alionyesha ukomavu usio na kifani wa kisiasa. Alitambua muunganiko wa kuunganisha vikosi vya Kiislamu na kupigana jihad dhidi ya Makruseda. Mikataba ya muda na baadhi ya vikosi vya Makruseda ilimuwezesha kulenga katika kukusanya nguvu zake na kuepuka mapambano yasio na lengo, akionyesha uoni wake wa mbali. Vikosi vya Salahudin vilionyesha uvumilivu usioyumba katika mapambano ya jihad yao, wasiotishwa na upinzani au vizuizi.

Wanazuoni walibeba jukumu muhimu katika kuutayarisha Ummah kwa ajili ya jihad, wakiongeza ari na kutoa msaada wa kifikra. Salahudin alijenga mahusiano ya karibu na wanazuoni, akiwashauri kuhusiana na vita na masuala ya usimamizi wa mambo. Al-Qadhi al-Fadhil, mwanachuoni maarufu, alichukua jukumu muhimu, akitoa nasaha na ushauri wa busara.

Baada ya matayarisho makini, Salahudin alimgeukia Mwenyezi Mungu (swt) kwa maombi ya unyenyekevu, akitambua utegemezi kwa Mwenyezi Mungu (swt). Uaminifu na ukweli wake kwa Mwenyezi Mungu (swt) ulikuwa wazi katika maombi yake na dua, akiomba ushindi kwa Yule Aliye Mkuu zaidi. Heshima na utukufu wake vilihusishwa na kujitolea kwake na kujifunga na Sharia. Kama Umar ibn al-Khattab alivyosisitiza kuwa Uislamu ni chanzo cha izza (utukufu) wa Ummah, akikazia katika mahusiano yasiotengana baina ya hadhi ya Ummah na kuwajibika kwake kwa Sharia.

“Sisi tumeumbwa kwa ajili ya Ibada na kwa Jihad tu.” yalikuwa maneno ya Salahudin wakati anaingia Damascus akitilia mkazo dhamira yake isiyoyumba kwa iman. Ushindi wa Salahudin haukuwa tu wa kijeshi; ulitokana na kuikumbatia iman, kujifunga na misingi ya Kiislamu na kufuata njia ya Mtume (saw). Mafanikio yake yalionyesha uwezo wa lugha ya Quran Tukufu katika kuwahamasisha waumini wanyenyekevu, wakitilia mkazo umuhimu wa iman na jihad katika kuunganisha ulimwengu wa Waislamu. Mafanikio yake katika Hattin na ukombozi wa mfuatano wa Al-Qudsi ilikuwa ni matokeo ya mkakati mpana unaojumuisha umoja, werevu wa kisiasa, utawala, diplomasia na dhamira ya dhati kwa jihad iliyotokana na misingi ya Kiislamu. Urithi wake hutumika kama kinara kwa uongozi wa kimkakati na ufuasi imara kwa misingi ya Kiislamu.

Hivi leo Ummah unakabiliana na hali sawia. Wavulana na wasichana wa Ummah wanauliwa kikatili mjini Gaza. Wakoloni walowezi wa Kiyahudi wameikalia kimabavu ardhi takatifu na yametokea haya mara tu baada ya kuanguka Khilafah na kugawanywa ardhi za Waislamu katika mgawanyo bandia usio wa kimaumbile wa dola za kitaifa, huku watawala vibaraka Waislamu wakihudumia maslahi ya wakoloni. Ardhi ambayo Salahudin ameiwacha huru kutoka kwa Makruseda, ardhi ambayo Khalifah Abdul Hamid II aliihifadhi, imeangukia kirahisi kwa Mayahudi kwa maagano ya dola za Kikoloni. Ummah unamsubiri tena Salahudin mwengine. Unamsubiri shujaa mwengine mwenye kipawa cha Salahudin, mwenye uadilifu, aliyejifunga na imani ya Uislamu na kupenda Jihad.

Mjumuiko wa hivi karibuni wa watawala Waislamu jijini Riyadh ulikuwa ni tafauti kabisa na matendo ya Salahudin Ayyubi. Wakati watawala hawa wakishutumu maovu yanayotendwa Gaza kwa kauli na matamshi, maneno yao yanakosa nguvu ya mabadiliko inayotokana na kuoanisha vitendo na maadili ya Kiislamu. Ushindi katika vita unahitaji matendo na sio ufasaha tu. Mfano aliouonyesha Salahudin unatufunza kuwa ufasaha wa kauli pekee bila matendo thabiti hupunguza kushughulikia udharura wa hali ilivyo. Viongozi wa Waislamu wanaotetea suluhisho la dola mbili wanasaliti dhati ya Uislamu. Palestina, ardhi iliobarikiwa ya Al-Masjid Al-Aqsa, haiwezi kugawanywa baina ya watu wake na maadui zake. Badala yake ni kuwa, suluhisho lake ni kama Mwenyezi Mungu Al-Aziz, Al-Jabbar, alivyosema, na kauli yake ndio suluhisho la kweli,

[وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ وَأَخْرِجُوهُمْ مِنْ حَيْثُ أَخْرَجُوكُمْ]

“Na wauweni popote muwakutapo na muwatoe popote walipo kutoeni.” [Surah Al-Baqarah 2:191].

Wito wa matendo sio tu ni wajibu wa pamoja lakini pia ni kielelezo cha kujifunga kwetu na Aqida ya Kiislamu. Maamrisho ya Quran ya kupigana na udhalimu na kuwanusuru wale wanaohitajia msaada kwa ajili ya dini lazima yasikike ndani ya nyoyo za Waislamu. Kama ambavyo Salahudin alivyoyashajiisha majeshi kuyalinda matukufu ya Al-Aqsa, majeshi ya hivi sasa lazima yaitike wito wa Gaza. Majeshi haya yanaungana na Aqida sawa na ile ya Salahudin, ambayo ni Aqida yenye nguvu zaidi ya Uislamu. Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[وَإِنِ اسْتَنْصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ]

“Na wakiomba msaada kwenu katika Dini basi ni juu yenu kuwasaidia.” [Surah Al-Anfal 8:72].

Enyi Majeshi ya Waislamu! Enyi Watoto wa Salahudin! Ni Uislamu pekee unaoweza kutuhuisha sisi. Ni Uislamu pekee unaoweza kutusukuma sisi. Unatufanya kumuogopa Mwenyezi Mungu (swt). Unatufanya tuelewe juu ya wajibu wetu juu ya Siku Kubwa ya Mwisho ya Hesabu. Inatusukuma kupanga matendo yetu kwa mujibu wa maamrisho ya Mwenyezi Mungu (swt), ima tukiwa wepesi au wazito.

Enyi Makamanda wa Kiislamu! Kwa mkabala wa uvamizi usizokoma dhidi ya ndugu zenu na dada zenu mjini Gaza, ni wajibu juu yenu kutafakari kwa undani juu ya wajibu wenu wa kuwahami madhlum na kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa. Tafakari hii lazima ijengwe juu ya misingi ya Aqida ya Kiislamu na ufahamu juu ya kuhisabiwa Siku ya Kiyama. Je, hamtamani moja ya neema mbili, ushindi au kufa shahidi? Je, hamtamani heshima katika maisha haya na ya Akhera? Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

 

يَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَيُدْخِلْكُمْ جَنَّـٰتٍۢ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ وَمَسَـٰكِنَ طَيِّبَةًۭ فِى جَنَّـٰتِ عَدْنٍۢ ۚ ذَٰلِكَ ٱلْفَوْزُ ٱلْعَظِيمُ * وَأُخْرَى تُحِبُّونَهَا نَصْرٌ مِنَ اللهِ وَفَتْحٌ قَرِيبٌ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ

“Atakusameheni dhambi zenu, na atakutieni katika mabustani yapitiwayo na mito kati yake, na maskani nzuri katika bustani za milele. Huko ndio kufuzu kukubwa. Na kinginecho mkipendacho, nacho ni Nusra itokayo kwa Mwenyezi Mungu, na ushindi ulio karibu! Na wabashirie Waumini!” [Surah As-Saf 61:12-13].

Enyi makamanda Waislamu mlio na ikhlasi! Hivi leo, wito wa matendo unajirudia kila tunaposhuhudia hali mbaya ya ndugu zetu katika Gaza. Wakati Ummah ukikabiliana na msiba huu, Aqida ya Kiislamu na mpango mtukufu wa Salahudin al-Ayyubi lazima ukuongozeni kwenye mwitiko wa maana wenye kuathiri. Ni jambo muhimu sana kwenda sambamba baina ya zama za Salahudin na hali ya sasa katika Gaza, wakati uongozi wake ukionyesha uimara unaotokana na Aqida ya Kiislamu. Ni muhimu kuigiza werevu wa kisiasa, mikakati na umahiri wa kijeshi wa Salahudin. Wakati wa vitendo ni sasa. Shikamaneni na mafundisho ya Uislamu na fuateni nyayo za Salahudin. Changamkeni kuwanusuru ndugu zenu katika Gaza, simameni dhidi ya uvamizi wa wale waliolaaniwa na Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ انْفِرُوا فِي سَبِيلِ اللهِ اثَّاقَلْتُمْ إِلَى الْأَرْضِ أَرَضِيتُمْ بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَنْيَا مِنَ الْآخِرَةِ فَمَا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فِي الْآخِرَةِ إِلَّا قَلِيلٌ * إِلَّا تَنْفِرُوا يُعَذِّبْكُمْ عَذَاباً أَلِيماً وَيَسْتَبْدِلْ قَوْماً غَيْرَكُمْ وَلَا تَضُرُّوهُ شَيْئاً وَاللهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ

“Enyi mlioamini! Mna nini mnapoambiwa: Nendeni katika njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya Akhera ni chache. Kama hamwendi atakuadhibuni adhabu chungu, na atawaleta watu wengine, wala nyinyi hamtamdhuru chochote. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.” [Surah at-Tawbah 9:38-39].

Uimara wa Waislamu Gaza dhidi ya tabia chafu kabisa ni ushahidi wa nguvu inayotokana na imani isiyoyumba. Vikosi vilivyoungana haviwezi kuvunja azma ya wale waliosimama imara katika njia ya Mwenyezi Mungu (swt). Kinyume chake, madhalimu, wanajikuta hawawezi kukabiliana na ari ya waumini. Vikosi vilivyoungana vya makafiri na Mayahudi waliojizatiti kwa teknolojia ya kisasa na silaha, wameshindwa kuwapunguza nguvu Waislamu katika Gaza. Hakika, Mayahudi kama alivyosema Mwenyezi Mungu (swt),

[لَنْ يَضُرُّوكُمْ إِلَّا أَذًى وَإِنْ يُقَاتِلُوكُمْ يُوَلُّوكُمُ الْأَدْبَارَ ثُمَّ لَا يُنْصَرُونَ]

“Maadui hawatakudhuruni ila ni maudhi tu. Na wakipigana nanyi watakupeni mgongo, na tena hawatanusuriwa.” [Surah Aali Imran 3:111].

Makafiri, waliojifungia ndani ya ngome imara, wamebakia wamegawanyika katika nyoyo zao, hawawezi kukabiliana na uthabiti wa waumini. Mgawanyo wa sasa uliopo miongoni mwa safu za Wakoloni unaakisi hali ya nyuma ya Makrusea kabla ya Vita vya Hattin. Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[لَا يُقَـٰتِلُونَكُمْ جَمِيعًا إِلَّا فِى قُرًۭى مُّحَصَّنَةٍ أَوْ مِن وَرَآءِ جُدُرٍۭ ۚ بَأْسُهُم بَيْنَهُمْ شَدِيدٌۭ ۚ تَحْسَبُهُمْ جَمِيعًۭا وَقُلُوبُهُمْ شَتَّىٰ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَووْمٌۭ لَّا يَعْقِلُونَ]

“Hawatapigana nanyi kwa mkusanyiko isipokuwa katika vijiji vilivyo zatitiwa kwa ngome au nyuma ya kuta. Wao kwa wao vita vyao ni vikali. Utawadhania kuwa wako pamoja, kumbe nyoyo zao ni mbali mbali. Hayo ni kwa kuwa wao ni watu wasio na akili.” [Surah Al-Hashr 59:14].

Sisi kama Waislamu, tunakumbushwa kuwa matendo yetu yatahesabiwa siku ya Kiyama. Watawala na makamanda wanaobaki wametulia tuli, huku wakishuhudia maovu na wakiwa upande wa madhalimu, watahesabiwa kwa khiyana yao kwa Ummah. Wito wa kuhamasisha, ima katika hali ya wepesi au uzito, imekita katika Aqida ya Kiislamu na hadithi za Mtume (saw). Kushindwa kuitika kunaweza kupelekea kubadilishwa kwa majeshi wengine wanaompenda Mwenyezi Mungu (swt) na njia Yake. Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

هَـٰٓأَنتُمْ هَـٰٓؤُلَآءِ تُدْعَوْنَ لِتُنفِقُوا۟ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ فَمِنكُم مَّن يَبْخَلُ ۖ وَمَن يَبْخَلْ فَإِنَّمَا يَبْخَلُ عَن نَّفْسِهِۦ ۚ وَٱللَّهُ ٱلْغَنِىُّ وَأَنتُمُ ٱلْفُقَرَآءُ ۚ وَإِن تَتَوَلَّوْا۟ يَسْتَبْدِلْ قَوْمًا غَيْرَكُمْ ثُمَّ لَا يَكُونُوٓا۟ أَمْثَـٰلَكُم

“Angalieni! Nyinyi mnaitwa mtumie katika njia ya Mwenyezi Mungu, na wapo katika nyinyi wanaofanya ubakhili. Na anayefanya ubakhili basi anajifanyia ubakhili mwenyewe. Na Mwenyezi Mungu si mhitaji, na nyinyi ndio wahitaji. Na mkigeuka atawaleta watu wengine badala yenu, nao hawatakuwa kama nyinyi.” [Surah Muhammad 47:38].

Enyi Watoto wa Ummah katika Majeshi ya Waislamu! Mwisho, kumbukeni kuwa Ushindi kwa ajili ya Uislamu na Waislamu hautegemei juu ya uwezo wa mwanadamu pekee. Bali unatoka kwa Mwenyezi Mungu (swt), ukiwasubiri wale walio wakweli na wenye kustahiki ambao wapo tayari kujitoa muhanga kwa ajili ya Dini yao. Wito wa kuhamasisha ni wito wa biashara ya dunia ipitayo kwa maisha ya milele. Kuisimamisha Khilafah, kwa njia ya Utume, kutahakikisha uunganishaji wa vikosi vya Waislamu na ni njia ya kupata heshima na utu wa Ummah. Ni wito uliokita katika Aqida ya Kiislamu na utambuzi wa kuwa tutaulizwa na Mwenyezi Mungu (swt) katika siku ya Kiyama. Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ تَنْصُرُوا اللهَ يَنْصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ * وَالَّذِينَ كَفَرُوا فَتَعْساً لَهُمْ وَأَضَلَّ أَعْمَالَهُمْ * ذَلِكَ بِأَنَّهُمْ كَرِهُوا مَا أَنْزَلَ اللهُ فَأَحْبَطَ أَعْمَالَهُمْ

“Enyi mlioamini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu. Na waliokufuru basi kwao ni maangamivu, na atavipoteza vitendo vyao. Hayo ni kwa sababu waliyachukia aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, basi akaviangusha vitendo vyao.” [Surah Muhammad 47:7-9].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Abdur Rahman Qutuz – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu