Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Moyo wa Muislamu: Ni Ndege ambaye Mabawa yake ni Hofu na Matarajio

Si ajabu kwa kafiri kuishi katika dunia hii, akiwa amesahau kuhusu maisha ya Akhera, bila kukhofu nini kitatokea kwake. Amekanusha neema ya Mwenyezi Mungu ya kumuumba yeye, amepinga uwepo wa Mwenyezi Mungu, na amefanya matamanio yake mwenyewe kuwa ndio Mungu wake na akajipeana kwa Shetani, anaye mpambia dunia na anasa zake, na kumshawishi kwa matamanio ili kushibisha ghariza zake na mahitaji yake bila kizuizi au hofu.

Lakini ikiwa hii ndio hali ya Muislamu, kufuata njia ya kafiri mwenye kughafilika na Akhera na hatma yake katika hili, basi ni jambo la ajabu kama ilivyo ajabu ya maisha yake katika maisha haya ya dunia ambapo sheria za Mola wake na hukmu Zake hazipo ndani yake. Vipi Muislamu anaye muamini Mwenyezi Mungu kuwa ni Mola wake, Nabii Wake Muhammad (saw) kuwa ni Mtume, na Quran kuwa ni Kitabu na Katiba, vipi anaweza kuishi huku Uislamu umefutiliwa mbali maishani mwake, isipokuwa katika baadhi tu ya matendo ya ibada ambayo yamekuwa ni desturi mithili wafanyavyo Wakristo kanisani?!

Vipi anaweza kuishi chini ya mfumo wa kikafiri wa kirasilimali ambao umemuwekea maisha ya kujitenga na Mwenyezi Mungu na muongozo Wake na mwangaza; maisha ambayo anayakimbilia bila mazingatio ambapo wasiwasi wake wote ni kushibisha mahitaji yake, hivyo moyo wake umekufa na hauna hofu kwa Mwenyezi Mungu, isipokuwa kwa wale ambao juu yao Mola wangu amewarehemu? Kwa nini Waislamu wengi wameikimbia biashara bora na kushikamana na biashara hatari yenye hasara? Kwa nini wamekosa uoni wa Akhera na kushikwa na dunia yenye kumalizika? Kwa nini nyoyo za wengi zimekuwa ngumu kiasi cha kuwa hazihofii matokeo ya madhambi wanayofanya, na unawaona ima wamekuwa na kiburi kwa ushauri wanaopewa, na kujifakhiri katika kubeba dhambi, au kutegemea juu ya rehema za Mwenyezi Mungu, hivyo hawajali kwa madhambi yao, makubwa au madogo, na husema “Mwenyezi Mungu ni Msamehevu na Mrehemevu”?! Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayra (ra) kuwa Mtume (saw) amesema kuwa Mola wake Amesema:

«وَعِزَّتِي لَا أَجْمَعُ عَلَى عَبْدِي خَوْفَيْنِ وَأَمْنَيْنَ، وَإِنْ أَخَفْتُهُ فِي الدُّنْيَا أَمَّنْتُهُ فِي الْآخِرَةِ، وَإِنْ أَمَّنْتُهُ فِي الدُّنْيَا أَخَفْتُهُ فِي الْآخِرَةِ»

“Kwa Utukufu wangu, Sito changanya juu ya mja wangu hofu mbili na amani mbili; kama ataniogopa Mimi katika dunia hii Nitampa amani Akhera, na kama akijiweka katika amani kutokana na Mimi katika dunia nitampa hofu Akhera”

Hivi watu hawa hawaidiriki Hadith hii? Je, hawazingatii maneno yake? Je, kiapo cha Mola wao na Utukufu Wake haviwashtui? Vipi wanaishi ulimwengu wao kwa amani huku wakiwa na yakini kuwa wanafanya vizuri ndani yake na kuwa na mategemeo ya kuishi katika amani hii Akhera: je, amani ya mara mbili imepelekwa pamoja kwao? Ni vipi hilo?! Kwa hakika hii haiwezekani, na Mwenyezi Mungu Mtukufu ameapa kwa Utukufu Wake kutoviweka pamoja kwa mja wake!

Muislamu lazima ategemee mazuri kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kama ambavyo lazima ahofie adhabu Zake. Ili aweze kwenda kwa uzuri katika dunia, ni lazima ayaunganishe haya mawili hadi akutane na Mwenyezi Mungu. Aweze kwenda katika ardhi, akitafuta Halali katika matendo yake na aepuke ya Haram, akimuogopa Mola wake, akiomba malipo Yake, na hatodanganywa na kazi yake, akifikiria kuwa ni muokozi wake na kusahau rehema na neema. Imepokewa kutoka kwa Anas bin Malik, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, kuwa Mtume (saw) aliingia kwa kijana mmoja akikata roho na kusema:

     «أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم دَخَلَ عَلَى شَابٍّ وَهُوَ فِي الْمَوْتِ فَقَالَ لَهُ: كَيْفَ تَجِدُكَ؟ فَقَالَ أَرْجُو اللَّهَ وَأَخَافُ ذُنُوبِي، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: لَا يَجْتَمِعَانِ فِي قَلْبِ عَبْدٍ فِي هَذَا الْمَوْطِنِ إِلَّا أَعْطَاهُ اللَّهُ مَا يَرْجُو وَآمَنَهُ مِمَّا يَخَافُ»

“Vipi unajihisi?” Akasema: “Nina matumaini kwa Mwenyezi Mungu, lakini ninahofia dhambi zangu.” Mtume wa Mwenyezi Mungu, (saw) akasema: “Vitu hivi viwili (matarajio na hofu) haviwi pamoja katika moyo wa mja katika hali kama hii, isipokuwa Mwenyezi Mungu atampatia kile anacho kitumainia na kumpa amani kutokana na kile anacho kihofia.”

Hivi ndivyo Muislamu hutakiwa awe, mwenye hofu na matumaini. Kwa kuwa hofu na matumaini kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu humsukuma mtu katika matendo mazuri na kutegemea mazuri kutoka kwa Mwenyezi Mungu na rehema zake, kwa kuwa ni njia ya kuepuka Moto na kuingia Peponi. Hichi ndicho Mtume (saw) alichokitoa kwa Ummah wake na ndicho alichokitaka kukiingiza ndani ya nyoyo za Masahaba wake na Waislamu wote. Amewaaminisha kuwa wamhofu Mwenyezi Mungu na wasijihisi salama kutokana na utenganishaji wao na kujiweka mbali kwao na uongozi wa Mola wao. Wamuombe Yeye, na kumtaka awathubutishe kama Mtume (saw) alivyo kuwa akifanya. Alikuwa akimuomba Mola wake siku zote kuuweka moyo wake imara juu ya Dini yake na utiifu Kwake! Huyu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Mpendwa Wake, ambaye Mwenyezi Mungu amemsamehe madhambi yake yaliopita na yajayo, na ambaye ameshaahidiwa Pepo, basi vipi kuhusu sisi?!

Tuko wapi sisi kutokana na mpendwa Mustafa, aliye kusanya hofu na matumaini, akitamani na akihofia na akielewa ukubwa wa jambo hili, basi akienda katika dunia hii na kumuabudu Mwenyezi Mungu kama anavyo stahiki kuabudiwa hadi alipokutana Naye bila ya kubadilika au kufitinika, na hali amepokea thawabu za Mwenyezi Mungu na radhi Zake na kuipata Pepo?

Muislamu lazima awe mwenye huzuni pindi akitenda dhambi, akipuuza wajibu au akipuuza jambo lolote la dini yake, na lazima ahofie katika maisha yake yote ghadhabu na kisasi cha Mwenyezi Mungu na hofu ya adhabu ya Moto. Hofu hii ni taa inayo angaza moyo wake, hivyo kama itatengana naye, moyo huu utaharibika, na mwenyewe atapotea, na matendo yake yatafisidika. Namna gani Muislamu leo ataridhika na Mola wake na kuishi katika dunia hii bila ya hofu ya hatima yake ya Akhera, kana kwamba ana hakika ataipata?! Vipi anaweza kuendelea mbele katika dunia hii wakati amepuuza jambo hili kubwa linalomkinga na uovu wa madhambi na kumzuia kutokana na kufuata matamanio, ili aepuke kuingia kwenye dhambi na kufanya matendo yaliokatazwa? Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

(إِنَّ عَذَابَ رَبِّكَ كَانَ مَحْذُوراً)

“Hakika adhabu ya Mola wako Mlezi yafaa kutahadhari nayo.” [Al-Israa: 57[.

Hofu inamsukuma kutenda matendo mema na kuacha makatazo, lakini bila ya kuelekea katika hofu inayokataliwa ambayo inampelekea kufa moyo na kukata tamaa kutokana na rehema za Mwenyezi Mungu na

(إِنَّهُ لَا يَيْأَسُ مِن رَّوْحِ اللَّهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْكَافِرُون)

 “Hakika hawakati tamaa na faraja ya Mwenyezi Mungu isipokuwa watu makafiri” [Yusuf: 87].

Muislamu hutamani kupata radhi za Mwenyezi Mungu, mapenzi, na malipo, na kuwa katika watu wa Peponi na kupata rehema zake. Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

إِنَّ الَّذِينَ آَمَنُوا وَالَّذِينَ هَاجَرُوا وَجَاهَدُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ أُولَئِكَ يَرْجُونَ رَحْمَةَ اللَّهِ وَاللَّهُ غَفُورٌ رَحِيمٌ)

“Hakika wale walio amini na wale walio hama na wakapigania Njia ya Mwenyezi Mungu, hao ndio wanaotaraji rehema za Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu” [Al-Baqara: 218].

Hamu ya Muislamu ni mategemeo yake kwa yatokayo kwa Mola wake, ambayo yanamsukuma kuendelea katika matendo mema, hivyo anashindana katika matendo mema na kujitahidi kuongeza utiifu wake, na moyo wake kujifunga na Pepo na neema zake, na kufanya bidii kwa nafsi yake na kutamania yale ambayo Mwenyezi Mungu amewaahidi watu mema katika Akhera, kutumia muda wake kwa kila kitu ambacho ni kizuri kwake na chenye kunufaisha. Lazima awe na moyo ulio hai uliobeba mapenzi ya Mwenyezi Mungu, na kuruka kama ndege kwa mbawa zake! Ibn al-Qayyim amesema: “Moyo katika njia yake kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kama ndege, ambapo mapenzi ndio kichwa chake, na hofu na matarajio ni mbawa zake.” Hofu na matarajio ni mbawa za moyo wa Muislamu, na hatoweza kupaa au kuelea hewani na kufikia lengo lake kama atapoteza moja ya mbawa zake. Pindi Muislamu anapo shikana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kusoma aya zake, hujawa na hofu na kutishika kwa aya hizo ambazo Mwenyezi Mungu amewaahidi makafiri na wanafiki na kuwa na wasiwasi kwa hofu ya kuwa yeye ni mmoja wao, na anapo soma aya ambazo Mwenyezi Mungu anawaahidi waumini hujawa na furaha na kujikurubisha kwa Mtume (saw), huwa na furaha kwa hilo na hutamani kupata daraja ya watu hao na humuomba Mola wake asimnyime hayo na kuwa ni miongoni mwao.

Hivyo, utambuzi wa muumini wa adhabu kubwa humpelekea kuogopa na utambuzi wake wa uwezo na rehema za Mwenyezi Mungu humfanya atamani na kuwa na matarajio kwa Mola wake. Mtume (saw) amesema:

«لَوْ يَعْلَمُ الْمُؤْمِنُ مَا عِنْدَ اللَّهِ مِنْ الْعُقُوبَةِ مَا طَمِعَ بِجَنَّتِهِ أَحَدٌ، وَلَوْ يَعْلَمُ الْكَافِرُ مَا عِنْدَ اللَّهِ مِنْ الرَّحْمَةِ مَا قَنَطَ مِنْ جَنَّتِهِ أَحَدٌ»

“Lau angejua muumini kile kilichoko kwa Mwenyezi Mungu katika adhabu, asingetumainia yeyote (kuipata) Pepo yake, na lau angejua kafiri kile kilichoko kwa Mwenyezi Mungu katika rehma zake, asingekata tamaa yeyote (kuipata) Pepo yake.”  

Kwa hayo, Muislamu lazima awe baina ya hali mbili: hali ya hofu na hali ya matumaini, na ziwe katika uzani ambapo hali moja asiifanye kuishinda nyengine. Kama nafsi yake itamshinda na kumpelekea katika dhambi, lazima akumbuke kumhofu Mwenyezi Mungu na adhabu Zake. Na kama itamshawishi kujitenga na mambo mema, lazima arejee katika kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kuomba rehema Zake na msamaha. Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

(أُولَئِكَ الَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَى رَبِّهِمُ الْوَسِيلَةَ أَيُّهُمْ أَقْرَبُ وَيَرْجُونَ رَحْمَتَهُ وَيَخَافُونَ عَذَابَهُ)

“Hao wanaowaomba, wao wenyewe wanatafuta njia ya kwendea kwa Mola wao Mlezi - hata miongoni mwao walio karibu mno – na wanataraji rehema zake na wanaikhofu adhabu yake.” [Al-Israa: 57]. Anafuata muongozo wa Mtume wake, rehema na amani ziwe juu yake, na Mitume wengine wote waliomuabudu Mola wao kwa hofu na matumaini.

(إِنَّهُمْ كَانُوا يُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَيَدْعُونَنَا رَغَباً وَرَهَباً وَكَانُوا لَنَا خَاشِعِينَ)

“Hakika wao walikuwa wepesi wa kutenda mema, na wakituomba kwa shauku na khofu. Nao walikuwa wakitunyenyekea.” [Al-Anbiya: 90].

Hivi leo, Waislamu wanaishi chini ya mfumo wa kirasilimali unaoitenganisha dini na maisha! Mfumo wa Kikafiri ambao haumuogopi Mwenyezi Mungu, wala kuwa na matarajio ya rehema zake! Mfumo usio wa kiadilifu wenye chuki kwa dini hii na watu wake, basi vipi Muislamu huweza kukubali haya? Vipi hukubali kuishi bila sheria za Mola wake kutekelezwa juu yake? Vipi huweza kubakia bila Imam anaye tekeleza vifungu vya Uislamu na kumhifadhi kutokana na uovu wa kuingia kwenye matamanio ya dunia? Vipi anaweza kujihisi yuko salama kutokana na adhabu za Mola wake wakati ameridhika na batili hii? Vipi haogopi hasira za Mola wake, ambaye sheria zake zimevurugwa na wanaadamu wameregea kizani na kwenye ujinga?!

Moyo wa muumini lazima upume kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu na uelee angani kama ndege akipiga mbawa zake, kutokana na hofu ya Mwenyezi Mungu na matarajio ya rehema zake, hivyo atafika angani na kuishi maisha ambayo Mola wake ameyakubali kwake, na hivyo atakuwa, Mwenyezi Mungu akipenda, miongoni mwa washindi. Lazima aharakishe kueneza kheri na kuregesha mwanga wa Mwenyezi Mungu na kufanya kazi na watendaji walio waaminifu kuinusuru Dini ya Mwenyezi Mungu na kuinyanyua juu bendera ya Al-Uqab kwa kuhofia kuwa Mola wake hatombebesha lawama kwa kile walichotenda wajinga na kutumai kupata radhi na kuandikwa miongoni mwa watendao mema na warekebishaji.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Zeinah As-Samit

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu