Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Uislamu ni Fikra na Njia (Twariqa) 

Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا]

“Leo nimekukamilishieni Dini yenu na nimekutimizieni neema zangu, na nimekutimizieni Uislamu uwe ndio Dini.” [Surah al-Maida 5:3]. Katika kipindi cha kuanguka kwa Waislamu, fikra ya Dini miongoni mwa Waislamu ilichukua ufahamu wa Wamagharibi, ambao ni ukasisi. Hii ni kwa sababu usekula ulioletwa na wanafalsafa wa Kimagharibi waliasi dhidi ya makasisi, hasa hasa viongozi wa dini ya Kikristo. Baada ya suluhisho la muwafaka baina ya viongozi wa dini na wanafalsafa, walikuja kutenganisha baina ya ukasisi au watu wa dini na na maisha. Hivyo, walitenganisha sheria, ambazo viongozi wa dini walizichukua kwa jina la Mungu kutokana na kushughulikia mambo ya watu. Kwa hivyo, usekula ulitenganisha sheria za kikasisi kutokana na maisha ya watu. Hata hivyo, fikra ya Dini katika Uislamu ni tofauti kabisa na zilivyo katika dini nyengine, ambazo zimechafuliwa na makasisi kwa maslahi ya wafalme, waliokuwa wakiwadhulumu watu kwa jina la dini. Hivyo Dini ya Uislamu haina ukasisi; bila shaka, iko mbali nao. Uislamu ni mfumo iliojengwa juu ya itikadi (Aqida) ambayo inaikinaisha akili na inakubaliana na umbile la mwanaadamu (Fitra). Umejengwa juu ya mkusanyiko wa Hukmu za kisharia ambazo zinatatua matatizo ya wanaadamu kwa nafasi yao kama wanadamu. Hukmu hizi za Kisharia ni Kiislamu ni kamilifu, zenye kuenea nyanja zote za kimaisha, ambazo ndio utatuzi na suluhisho sahihi kwa matatizo yote ya wanadamu, bila ya kuzingatia mahala au zama.

Maana ya kuwa Uislamu ni mfumo iliojengwa juu ya Aqida ambayo kwayo inachipuza nidhamu ya maisha humaanisha kuwa Uislamu ni Fikra na Twariqa. Uislamu sio mkusanyiko wa sheria zisizo nyumbuka, fanya na usifanye, unaotangulia zama au kuwa nyuma yake. Bali, Uislamu una hukmu za kivitendo zinazo weza kutekelezeka katika zama na sehemu zote na juu ya kila kizazi cha wanaadamu, awe Muarabu au asiye Muarabu, mweusi au mweupe, maji ya kunde au mwekundu. Kwa hivyo, Uislamu umeteremshwa kwa wanaadamu katika sifa yao ya ubinaadamu na mfumo huu imeteremshwa na Muumba (swt) wa wanaadamu, Mwenyezi Mungu (swt). Mwenyezi Mungu (swt) (swt) anajuwa yote yenye kufaa na pamoja na yasiyofaa kwa wanaadamu. Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[أَلَا يَعْلَمُ مَنْ خَلَقَ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ]

“Asijue aliyeumba, naye ndiye Mjua siri, Mwenye khabari? [Surah al-Mulk 67:14]

Hivyo Uislamu ni Fikra, Aqida na Hukmu za Kisharia. Na Uislamu ni Twariqa, inayokusanya hukmu za kisharia ambazo zinafafanua namna ya kutekeleza Aqida na Hukmu za kisharia. Hivyo, Mwenyezi Mungu (swt) ameamrisha juu ya imani ya Ulazima wa Kuwepo Kwake na katika Utume wa Muhammad (saw), ambazo ni Hukmu kutokana na Fikra. Yeye (swt) ameharamisha mtu kutoka katika Uislamu na akaamrisha kubeba ulinganizi wa Uislamu duniani. Hivyo hukmu zenye kuonyesha Namna ya utekelezaji wa Maamrisho na Makatazo ni Njia (Twariqa), kama hukmu za Anayeritadi, Hukmu za Jihad na Hukmu zinazo husiana na Washirikina Waarabu na wasiokuwa Waarabu. Mwenyezi Mungu (swt) ameamrisha kujihifadhi na amekataza zinaa, Yeye (swt) ameamrisha kuhifadhi mali ya kibinafsi na kukataza wizi na Yeye (swt) ameamrisha kuhifadhi nafsi na kukataza mauaji, ambazo ni Hukmu za Kifikra. Hata hivyo Hukmu  zinazo fafanua Namna ya Utekelezaji wa Maamrisho na Makatazo ni zinazohusu Twariqa, kama adhabu kwa Zinaa, adhabu kwa wizi na kuuliwa kwa muuaji. Mwenyezi Mungu (swt) ameamrisha usimamishaji Khilafah na kuwakataza Waislamu kubakia bila ya kuisimamisha Khilafah kwa zaidi ya siku tatu. Yeye (swt) ameamrisha kuweka makadhi wanao hukumu mizozo. Yeye (swt) ameamrisha kusimamia mambo ya Waislamu na kuharamisha dhulma, udanganyifu katika biashara, ukiritimba na unyanyasaji. Hivyo Hukmu za Twariqa, ambazo zinafafanua Namna ya Utekelezaji wa Maamrisho na Makatazo ni Hukmu za biashara, sheria, Baytul-Mal, Dhulma katika Hukmu na Hisba (Kuondosha udanganyifu wa kibiashara kwa watu). Mwenyezi Mungu (swt) ameamrisha kuwalisha maskini na wahitaji na kukataza kumuacha yeyote kubakia na njaa kwa sababu ya hitajio, ambazo ni hukmu kutokana na fikra. Hivyo Hukmu za Twariqa ni zile Hukmu ambazo hutoa mali kwa masikini na kumlinda kila mmoja kutokana na njaa kutokana na umasikini, kama Hukmu za Nafaqa (matumizi ya lazima nyumbani), Hukmu za Zaka na Hukmu zinazo husiana na Bayt ul-Mal. Hii ni namna ambapo kila Hukmu inayo fafanua Utekelezaji wa kila Amri katika Maamrisho ya Mwenyezi Mungu (swt), pamoja na kukataza yaliyo haramishwa na Mwenyezi Mungu (swt), ni katika Twariqa.

Hivyo, Twariqa hukusanya Hukmu za Kisharia. Haipaswi kusemwa kuwa hakuna dalili maalumu ya ombi (Talab) la kukatikiwa kutoka kwa Mtunga sheria kuhusiana na Wajibu wa kujifunga na Twariqa. Dalili ya hili ni Ushahidi unao onyesha wajibu wa kujifunga na Hukmu za Kisharia. Dalili hizi zinajumuisha tamko la Mwenyezi Mungu (swt),

[فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا]

“La! Naapa kwa Mola wako Mlezi! Hawatakuamini mpaka wakufanye wewe ndiye muamuzi katika yale wanayokhitalifiana, kisha wasione uzito katika nyoyo zao juu ya hukumu utakayotoa, na wanyenyekee kabisa” [Surah an-Nisa’a 4:65]. Na kauli Yake,

[وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا]

“Na anacho kupeni Mtume chukueni, na anacho kukatazeni jiepusheni nacho.” [Surah Hashr 59:7] miongoni mwa dalili nyengine maarufu zinazo julikana.

Mwenyezi Mungu (swt) hakuweka Hukmu za Kisharia kutatua matatizo kwa ajili tu ya mtu kuweza kutekeleza hukmu hizi apendavyo yeye. Mwenyezi Mungu (swt) hakuamrisha, ‘Usiibe’, ‘Usizini’, Usile chakula cha wengine’, Usinywe mvinyo’, bila kuainisha namna ya kuyatekeleza hayo. Hivyo, Mwenyezi Mungu (swt) ameamrisha kutokuiba na pia akaweka Hukmu zinazo fafanua namna ya kutekeleza katazo hili, ambalo ni Hukmu inayohusiana na wizi, unyanganyi, ujambazi na uporaji. Hivyo Mwenyezi Mungu (swt) sio tu amefafanua Hukmu zote ambazo ni muhimu kwa mwanaadamu katika maisha yake, lakini pia amefafanua Hukmu zote ambazo ni muhimu katika kutekeleza hukmu hizi. Mwenyezi Mungu (swt) hakuweka Hukmu yoyote, ima ya kutatua matatizo au namna ya kutekeleza utatuzi huu, isipokuwa Yeye (swt) amezifafanua zote. Kwa hiyo, Uislamu ni Fikra na Twariqa; Fikra zake zinajumuisha Aqida na Hukmu ambazo hutatua matatizo ya maisha, kama katika kuamini uhalali wa Uislamu, Quran na Sunnah, na ukanushaji wa Ukafiri, pamoja na hukmu za biashara, ndoa, kukodisha na Swala. Ama kwa upande wa Twariqa, hukusanya Hukmu ambazo zinafafanua juu ya namna ya kutekeleza Fikra hii, yaani namna ya kutekeleza Aqida na Hukmu za Kisheria, kama hukmu za Jihad, Ngawira za vita, al-Fay-i na kuritadi, hukmu za adhabu kama Hudud, Janayat na Ta’zir, na hukmu za Da’wah, kumhisabu mtawala, kuamrisha mema na kukataza maovu.

Kujifunga na Twariqa ni Wajibu na kutokujifunga nayo ni dhambi. Na yeyote asiye jifunga na Twariqa na kuchukua Twariqa nyengine, huku akiamini kutosihi kwake Twariqa hiyo, tendo hili ni tendo la ukafiri, (Mwenyezi Mungu atulinde). Hivyo, yeyote asiye jifunga na hukmu za Uislamu katika sifa yake kuwa ni Twariqa inayo stahili kutekelezwa, huku akiamini haifai kuacha kujifunga kwake, kama kukatwa mwizi mkono, kwa mfano, basi huwa amekufuru. Kama hakujifunga nayo kutokana na uvivu au tamaa au mfano wake, basi tendo lake hilo ni uasi. Na kutoka hapa hukmu kwa watawala na makadhi huja kwa namna ya ima ni Ukafiri au Uasi, kwa sababu hukmu na mahakama ni katika Twariqa. Kadhi anayetoa hukmu ya kumfunga mwizi na sio kumkata mkono anapaswa kuangaliwa. Ikiwa anatoa hukmu hiyo bila ya kuamini usahihi wa ukataji mwizi mkono na kusihi kwake, hutenda ukafiri na hutoka katika Uislamu. Ikiwa atatoa hukmu hiyo kutokana na kutenzwa nguvu juu ya matakwa ya mtawala, huku akiamini usahihi wa kukata mwizi mkono na kufaa kwake, basi huwa ametenda dhambi. Katika hali zote mbili, ametenda dhambi. Hali hiyo pia ni sawa kwa watawala. Hivyo, Kujifunga na Twariqa yaani Hukmu zinazo fafanua namna ya utekelezaji Hukmu hufikia kiwango cha ukali kutokana na kauli ya Mwenyezi Mungu (swt),

[فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ]

La! Naapa kwa Mola wako Mlezi! Hawatakuamini mpaka wakufanye wewe ndiye muamuzi” [TMQ 4:65]. Hufikia kiwango kibaya zaidi kiasi cha kuwa yeyote asiye amini, hutenda ukafiri (Mwenyezi Mungu atuhifadhi).

Ulinganizi wa Uislamu katika kiwango cha dola kupitia Twariqa maalum ni Jihad, kuwatiisha watu kwa utumiaji wa nguvu ili washikamane na Sharia za Uislamu baada ya ardhi hiyo kuwa chini ya Utawala wa Kiislamu. Kwa hiyo huu ni mvutano wa Waislamu na mataifa mengine ambao uko ndani ya maumbile ya Uislamu na hatimaye kuwa ni katika maumbile ya Waislamu. Zaidi ya hayo, uwepo wa Sultan (Mamlaka) au dola huwakilisha roho ya mwili, katika kadhia ya Uislamu. Kadhia ya Uislamu haipatikani wala haisalii bila ya utawala. Bila ya utawala, nuru ya Uislamu haitoangaza maisha, wala Uislamu hautakuwepo. Mvutano ambao Waislamu wanaingia na mataifa mengine ni mvutano wa kifikra, ambapo zana yake ni mada, ima iwe ni katika Jihad au kuwatiisha watu kwenye Sharia. Bila shaka, watu watalinganiwa kwenye Uislamu kwa uwazi wakati wa Jihad kabla mapambano hayajaanza. Katika kuwatiisha watu kwenye Sharia za Uislamu, adhabu zitatolewa tu kwa kuachwa maamrisho na kutendwa kwa makatazo, na ni tu baada ya tamko la Hukmu kwa watu na kuzoeana kwao na Sharia. Katika hali yoyote, utawala kwa nafsi yake huongoza Ummah kwa ajili ya Jihad na kutekeleza Huduud za Mwenyezi Mungu kwa kuwa utawala umejengwa juu ya Fikra na unaendelea kwa mujibu wa Fikra. Utawala huu unaendelea kwa kuchanganywa na Fikra, kiasi cha kuwa tofauti yoyote au mtengano kutokana na Fikra huwa ni makosa. Kwa hivyo, sio rahisi kwa wale wanaokabiliana na utawala wa Kiislamu kusimama dhidi yake, kwa kuwa makabiliano yao ni ya kimada halisi na utawala wao ni utawala wa kimada, ambapo mapambano ya Kiislamu ni mapambano ya kifikra na ala yake ni mada na utawala wake ni utawala uliojengwa juu ya Fikra ya Kiislamu. Hii ndio sababu kwa nini Waislamu wakati wote wameshinda vita, japokuwa wamepoteza mapambano mengi. Huenda, hii inafichua siri ya Waislamu kuamrishwa kusimama dhidi ya nguvu ambayo ni mara kumi zaidi ya nguvu zao, ambapo waliwepesishwa kwao kwa kuamrishwa kusimama dhidi ya jeshi ambalo ni mara mbili ya nguvu zao. Kwa hakika, hairuhusiki kwa Waislamu kukimbizwa na jeshi lililo na nguvu mara mbili yao. Hii ni kwa sababu nguvu za Fikra, ambazo utawala umejengwa nazo ni mara kumi zaidi na imara zaidi ya nguvu za kimada. Hivyo jambo muhimu zaidi katika mvutano huu wa Waislamu, ambao lazima wauingie na watu (wengine), ni jambo la kifikra ambalo nguvu za kimada zimejengwa juu yake, au kwa maneno mengine, ujengaji wa nguvu za kimada juu ya Fikra.

Watu wanaoingia katika mapambano ya kumwaga damu na Waislamu hawakutanabahi kiwango cha nguvu za Aqida ya Kiislam yaani Fikra katika nguvu ya mada. Hivyo walitegemea juu ya kuongeza nguvu zao za kimada dhidi ya jeshi la Waislamu ili kuwashinda Waislamu. Hata hivyo, licha ya kuongeza nguvu zao, Waislamu walikuwa washindi dhidi yao japokuwa walikuwa dhaifu na idadi ndogo. Ongezeko la nguvu za kimada halikuwanufaisha watu hawa katika uwanja wa mapambano, na ushindi ulibakia kwa Waislamu pekee. Hali hii ndio iliyo kuwa kwa Washirikina kwa Mtume (saw) na Masahaba wake (ra). Hii ilikuwa ndio hali ya Warumi na Wafursi kwa Masahaba wa Mtume (saw). Hii ndio hali ya makafiri wote walioinga katika vita na Waislamu katika zama zote za utawala wa Kiislamu. Waislamu wamepoteza si zaidi ya mara mbili wakati wa zama za Uislamu. Mara moja ilikuwa wakati wa vita vya msalaba, ambapo Waislamu walipoteza, japokuwa waliregea vitani, wakaanzisha mapambano na hatimaye wakawa washindi. Tukio la pili lilikuwa katika kipindi cha karne ya kumi na tisa, ambapo hatimaye walishindwa kabisa katika Vita vya Kwanza vya Dunia.

Hivi leo dunia yote inajaribu kujiengua kutoka kwenye utawala wa Kimagharibi. Ni jambo la kimaumbile kwa Waislamu kutaka kuun’goa utawala wa Kimagharibi na kupambana na maslahi ya Wamagharibi katika ardhi zao. Hata hivyo, je dunia itafanikiwa kumaliza utawala wa Wamagharibi? Je, Waislamu wataun’goa ushawishi wa Wamagharibi? Kile kinacho wafanya Waislamu kuendelea katika njia ya sawa ni kubaini kwao kuwa jambo la msingi kwao sio kujitoa kutoka kwenye utawala wa Wamagharibi pekee. Hilo lenyewe, ni muitiko wa kimaumbile tu, kwa mwanaadamu kupinga kutawaliwa na kamwe hawezi kuridhia utumwa. Kadhia ya Waislamu ni kadhia ya Uislamu pekee, ambao ni ulinganizi wa Uislam kupitia Jihad na kuwatiisha watu kwa nguvu kwenye Hukmu za Sharia. Twariqa sahihi ni kuingia katika mivutano na mataifa yote kwa upande wa mapambano ya kimada, mapambano ya damu, kwa ajili ya kueneza Uislamu na kuwatiisha watu kwenye Sharia zake. Hii ndio Twariqa sahihi na hakuna Twariqa kwa Waislamu isiokuwa hii. Hakupatikani Twariqa kwa Waislamu mbali ya hii, wakiwa wao ni Waislamu. Kwa hivyo, hakuna khiari kwa Waislamu katika muendelezo huu. Waislamu wanalazimika kuendelea katika hili endapo wanataka kubakia kuwa Waislamu na kubakia kuwa kama Ummah wa Kiislamu. Hii ni kwa sababu mvutano huu hauko tu katika maumbile ya Waislamu pekee; ni maumbile ya Uislamu wenyewe.

Hata hivyo, kuingia katika mvutano huu kwa ajili ya maslahi ya jambo la Waislamu litafanyika tu kupitia mamlaka na sio kila mamlaka, bali ni mamlaka ya Kiislam pekee. Hivyo, utawala wa Kiislamu lazima uwepo kwanza ufuatiwe mara moja na mapambano ya kimada na mataifa. Hivyo kazi ya kusimamisha utawala wa Kiislamu ni tendo ambalo jitihada hupaswa zitumike juu yake. Hii ni kwa sababu hakuna suala la Waislamu kabla ya kuwepo kwake. Hakuna njia ya kufanya kazi kwa ajili ya jambo hili au ndani ya suala hili kabla ya kuwepo kwake. Ili tuanze kufanya kazi, bali kuweza kufanya kazi, ni lazima kuzifunga jitihada zote katika kusimamisha mamlaka haya maalum, mamlaka ya Kiislamu. Uhalisia ni kuwa kusimamisha mamlaka ya Uislamu katika Ulimwengu wa Kiislamu ni rahisi zaidi kuliko kusimamisha mamlaka mengine yoyote, ima iwe ni maumbile ya mamlaka kama ni mamlaka, au maumbile ya mamlaka ya Kiislamu kama mamlaka ya Kiislamu. Ama maumbile ya mamlaka, mamlaka yako kwa Ummah au kwa kundi lenye nguvu ndani yake. Wengi wa watu katika ardhi ya Kiislamu ni Waislamu, hivyo kusimamisha mamlaka ya Kiislamu miongoni mwao ni rahisi zaidi kuliko kusimamisha mamlaka mengine yoyote. Ama maumbile ya mamlaka ya Kiislamu, ni wajibu kwa Muislamu kukabiliana na jeshi kubwa mara kumi yake mwanzoni mwa mamlaka, na kisha kukabiliana na jeshi kubwa lililo mara mbili zaidi yake katika hali nyengine za kawaida. Ikiwa wale wanaosimamisha mamlaka ni wachache katika ardhi, basi wana uwezo wa kuwashinda walio mara kumi ya idadi yao. Wana uwezo mkubwa zaidi kusimamisha mamlaka ya Kiislamu, kuliko wengine wanaotaka kusimamisha utawala mwengine wowote. Bila shaka, kusimamisha mamlaka ya Kiislamu katika ulimwengu wa Kiislamu ni jambo la karibu sana kuliko kusimamisha mamlaka mengine. Kwa hivyo, tukumbuke kauli ya Mwenyezi Mungu (swt),

[وَإِن يَكُن مِّنكُم مِّائَةٌ يَغْلِبُوا أَلْفًا]

“Na wakiwapo kati yenu mia watawashinda elfu moja”. [Surah al-Anfaal 8:65].

Na kauli Yake (swt),

[إِن يَكُن مِّنكُمْ عِشْرُونَ صَابِرُونَ يَغْلِبُوا مِائَتَيْنِ]

“Na wakiwapo kati yenu ishirini wanaosubiri watawashinda mia mbili” [Surah al-Anfaal 8:65].

Kwa njia hii, Uislamu umejengwa juu ya Aqida, ambayo kwayo unachipuza mfumo kamili wa kipekee unaoleta furaha kwa wanaadamu na kusuluhisha matatizo yao. Uislamu mtukufu una Twariqa ya utekelezaji, ambayo ni Dola ya Kiislamu inayo tawala kwa Uislamu. Uislamu huu mtukufu utabakia tu kuwa ni mfumo mkuu, hadi utakapo tekelezwa kama dola na Ummah wa Kiislamu, unao ongozwa na chama cha kisiasa ambacho kina ufahamu wa Sharia za Uislamu. Hata hivyo, chama hiki kinahitaji nguvu za kimada kufikia nafasi ya utawala. Watu wenye nguvu hizi ni watu wa Nussrah kutoka miongoni mwa majeshi ya Ulimwengu wa Kiislamu. Hawa ni wale wanaotambua kuwa kadhia ya Uislamu ni utekelezaji wa Uislamu katika mambo ya watu na kuulingania Uislamu kupitia Twariqa maalum ambayo ni Jihad na kuwatiisha watu kwa nguvu kujifunga na hukmu zake. Mapambano ya kimada na watu ni kupitia mamlaka ya Uislam. Bila ya Twarika hii, Waislamu hawatoweza kujikomboa kutokana na utawala wa Wamagharibi wala kung'oa maslahi yao miongoni mwao. Fauka ya hayo, hawatobakia kuwa ni Ummah wa Kiislamu. Watu wenye msemo/nguvu hawana haki ya kudai kuwa wao ndio nguvu/jeshi la Uislamu, huku wanawatelekeza Ummah na hawainusuru Dini ya Mwenyezi Mungu (swt) kwa kutoa Nussrah kwa chama ambacho kinabeba jukumu la kuuhuisha Ummah. Wanapo wapa migongo, watakuwa wamekanusha sababu ya kuwepo kwao katika maisha haya kama watumishi wa Mwenyezi Mungu (swt). Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنْسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ]

“Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi” [Surah adh-Dhariyaat 51:56]. Kumuabudu Mwenyezi Mungu (swt) hakugawanyiki na hivyo hairuhusiki kwa afisa na mwanajeshi kumuabudu Mwenyezi Mungu (swt) kwa kutekeleza Swala, Funga, Umrah, Hajj na Zakah pekee, wakati hatekelezi kilicho cha wajibu zaidi ya haya, ambacho ni kutoa Nussrah kwa Uislamu, kunyanyua bendera za Uislamu na kuukabili uso wa Dunia kupitia Jihad katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, jukumu limewekwa kwenye mabega ya watu wa Nussrah, hadi watekeleze Jihad katika Njia ya Mwenyezi Mungu (swt), kwa kusimamisha Uislamu katika utawala na kubeba Uislamu kama ujumbe, uongofu na rehma kwa wanadamu wote. Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ تَنْصُرُوا اللَّهَ يَنْصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ]

“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu” [Surah Muhammad 47:7]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Bilal Al-Muhajir – Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu