Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mjomba Wetu (Mamo), Naveed Butt

Kila mmoja anamwita Mamo (Mjomba) na ndio maana kamwe haikuwa vizuri kumwita Naveed Butt. Jina hili limejenga hisia ya udugu, ingawa alishakuwa ni kama mtu wa familia yetu. Hakika, kila mmoja anajihisi kuwa anatokana na familia yao. Nimefanya kazi chini yake kama naibu msemaji (wa Hizb ut Tahrir Pakistan) amenikunjulia fadhila nyingi kwa muda wa miaka saba na kutokana na ukweli huu nimepokea mema mengi kutoka kwake. Amenikunjulia fadhila nyingi, kiasi kwamba familia yangu haiwezi kuzilipa. Daima yupo katika sehemu ya Dua za mke wangu na mimi. Pindi watoto wangu walipoanza kuongea tuliwafunza kuomba “Ewe Mwenyezi Mungu tusamehe sisi, Ewe Mwenyezi Mungu wasamehe wazazi wetu, Ewe Mwenyezi Mungu muokoe Mamo kutokana na kifungo.” Moyo wangu una huzuni na utabaki hivyo hadi atakapo tolewa. Wakati nafanya kazi katika Afisi Kuu ya habari ya Hizb ut Tahrir ndani ya Wilaya ya Pakistan chini ya uongozi wake, si tu nilipokea maarifa na kujifunza sanaa ya kufikisha Da'awa, lakini pia nimepokea muongozo wake katika kila sehemu ya maisha kama vile ndoa, kukuza watoto, dawa, matibabu, ushirikiano wa kibiashara, maadili na familia. Bado najutia kuwa sikunufaika zaidi kutoka kwake kwa sababu ya kasoro zangu mwenyewe.  

Nilimuona katika nyakati ambazo hakuwa vizuri kifedha. Hata katika kipindi hicho, hakuwahi kuniruhusu kulipia kitu. Hakutaka kujionesha kuwa ni dhaifu kifedha. Alipo pokea kiasi cha fedha kutoka kwenye mirathi, nyingi yazo alizigawanya kwa ndugu kama sadaka au mkopo. Sikufahamu kuwa alimtaka yeyote kulipa deni lake.

Nilikuwa na kawaida ya kuambatana naye pamoja kwenda kuonana na wanahabari. Kutokana na kufungiwa kwa chama, ni mara chache ndio tukipata fursa za mahojiano. Mara moja tulipata nafasi ya kuhojiwa na gazeti jijini Rawalpindi na ilikuwa ni mafanikio makubwa. Mamo na mimi tulikuwa tunasafiri kuelekea katika afisi za gazeti hilo. Tulipoiona gari imeharibika, na pembeni kuna dereva na familia yake wamesimama pambizoni, Mamo alisimama na kulikagua lile gari na kubaini kuwa tangi liliishiwa na gesi, hivyo gari ilihitajika kuvutwa hadi kituo cha karibu cha gesi (CNG). Nikamwambia Mamo kwamba mahojiano ni muhimu sana, na kwamba mtu mwengine atawasaidia. Hata hivyo, alilikokota gari lao kwa gari lake na kuwapeleka kituo cha CNG mwenyewe.

Mamo alikuwa mtendaji mzuri na mwenye shauku ya kupigania Khilafah. Alibaki katika msingi huu kwa saa 24, siku 7 za wiki, siku 365 za mwaka. Kamwe sikuwahi kumuona kushindwa kujibu maswali yao mbele ya vyombo vya habari. Kuhusiana na wale wanaojulikana leo kama watangazaji maarufu, Mamo alikuwa akijibu maswali yao magumu, ambayo viongozi wa Kiislamu huepuka kuyajibu waziwazi au kutoa udhuru. Hata hivyo, Mamo alikuwa akiwavutia ubora wa fikra ya Uislamu juu yao. Mtangazaji wa Runinga ya ARY alimuuliza Mamo, “Je, katika Khilafah mtawalazimisha wanawake kujisitiri wenyewe?” Mamo kwa utulivu akamjibu, “Niambie, kwani hakuna sheria ya kiwango cha chini mavazi katika maeneo ya ummah katika nchi kama Amerika, Uingereza na Ufaransa?

Kuna yeyote anaye weza kutoka nje akiwa uchi kabisa? Kama kuna kikomo, inamaanisha uhuru wa moja kwa moja hauwezekani. Hivyo basi, suala sio kuwepo kwa ukomo, kwa sababu upo kila mahali, wa aina mbalimbali na huwezi kupinga hilo. Swali ni kuwa, ni nani mwenye mamlaka ya kuamua ukomo huo. Demokrasia inazingatia kuwa mamlaka ya kuamua hilo yapo chini ya bunge, wakati sisi Waislamu tunaamini kuwa hiyo ni haki ya Muumba wa ulimwengu huu (swt) pekee.” Baada ya jibu hili mtangazaji hakuibua maswali mengine tena.

 Mtangazaji mwengine, ambaye amehamia katika YouTube, alivutiwa ndani ya dakika mbili tu pindi alipo mualika katika kipindi chake. Mamo alimuuliza, “Tafadhali nieleze hadi lini utazuia watu katika mjadala wa kulinganisha baina ya demokrasia na udikteta? Kwani zote hazina mfumo mmoja wa mahakama? Kwani zote hazina nidhamu moja ya mahakama? Kwani zote hazina polisi sawa, urasimu na nidhamu za kijamii zilizotokamana na fikra huru? Ikiwa Mujahidina waliuzwa kipindi cha Musharraf, je Aimal Kansi naye hakuuzwa kwa Amerika katika kipindi cha Nawaz? Kwani je wote hawalindi maslahi ya Amerika kwa jina la “maslahi ya taifa”? Kwani si wote hao hufanya kazi kwa amri ya wakoloni mamboleo? Hata hivyo, kipindi hicho hakikurushwa hewani, huenda ni kwa sababu ya simu moja ambayo ilimlazimisha kuibadilisha ofa yake.

Mtangazaji mwengine aliyekuwa akitarajia kustaafu katika idhaa yake alimpa fursa ya kutosha Mamo katika kipindi chake cha mwisho ili aweze kuwasilisha ulinganizi wake kwa uwazi. Hii ilionyesha mapenzi ya wanahabari juu ya Uislamu na pongezi zote bila shaka zinaenda kwa Mamo.

Mamo aliandika makala mingi kukanusha fikra zilizo athiriwa na wana mamboleo na wenye fikra za maridhiano. Hata leo, makala haya, ambayo yaliandikwa kwa Kiurdu chepesi, ndio bora zaidi ya kupinga fikra hizo. Aliandaa makala mwanana juu ya mada za nidhamu ya uchumi katika Uislamu, nidhamu ya utawala katika Uislamu, sheria katika Uislamu na sera za kigeni na elimu katika Uislamu, ili imani ya Ummah iweze kubakia katika Dini yake tukufu. Taarifa zake kwa vyombo vya habari ziliwachana vipande vipande madhalimu na haikuvumilika kwa watawala kukubali athari kali ya maneno yake.

Mamo na marafiki zake si tu waliwatengeneza wanachama kwa ajili ya Hizb ut Tahrir, bali walitengeneza viongozi kwa kiwango kikubwa. Bila shaka yeye ni mwalimu wa mashabab wengi na InshaAllah ataregea. Hatojutia kutekwa nyara na kupotezwa kwa nguvu, pindi atakapo tambua kuwa waliofuatia wametimiza jukumu la kubeba ulinganizi huu. Inawezekana pindi atakapo rejea hali itakuwa katika namna ambayo madhalimu watakuwa wamesha nyakuliwa shingo zao na mchezo wa wakoloni utakuwa umefikia mwisho. Siku hiyo, chini ya kishindo cha Takbira na kubebwa katika mabega ya ndugu zetu, Mamo ataanza kutimiza majukumu ya kutabikisha Dini ya Uislamu akiwa miongoni mwa watawala.

#MwacheniHuruNaveedButt
#MjueNaveedButt

                   Imeandikwa kwa ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na   

    Imran Yusufzai – Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu