Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Kwa Nini Serikali za Kisekula Zimepagawa Sana na Hijab?

Vazi la mwanamke wa Kiislamu, ima Khimar, jilbab au Niqab kamwe huwa haliko mbali na vyombo vya habari au kurunzi ya kisiasa ndani ya dola za kisekula. Tuhma kadha wa kadha zimerushiwa vazi hili na waandishi habari wa kisekula, wanaharakati wa wanawake, wanasiasa na serikali – mashariki na magharibi – ambao wamelibandika "nembo ya unyanyasaji". Matokeo yake, marufuku ya hijab na niqab imelazimishwa katika dola kadhaa za kisekula. Mwezi uliopita, vazi la Kiislamu kwa mara nyengine tena liligonga vichwa vya habari wakati ambapo Mbunge wa Ufaransa aliondoka katika kikao cha uchunguzi kilichokuwa kikifanywa ndani ya bunge la Ufaransa kupinga mwanamke mmoja wa Kiislamu aliyekuwa amevaa Khimar huku akitoa ushahidi katika kikao hicho.

Majadiliano haya ya paneli yatachunguza ni kwa nini wanasiasa na serikali za kisekula wanabeba chuki kama hii kwa vazi la Kiislamu la mwanamke, kuchunguza uhalali wa tuhma hizo zilizotolewa dhidi yake, na kueleza namna Waislamu wanapaswa kujibu mashambulizi dhidi ya vazi la mwanamke wa Kiislamu."

3 Oktoba 2020

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatano, 07 Oktoba 2020 11:09

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu