Jumanne, 22 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Zanzibar Yahitaji Suluhisho la Kiislamu
Sio Serikali ya Mseto ya Kidemokrasia

Habari:

Mnamo tarehe 06/12/2020 chama kikuu cha upinzani cha Zanzibar Alliance for Change and Transparency-ACT-Wazalendo kilitangaza kujiunga na Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU). Halafu mnamo tarehe 07/12/2020, Rais Hussein Mwinyi alimteua Seif Sharrif Hamad wa ACT kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais na mnamo 08/12/2020 sherehe ya kuapishwa ilifanyika Ikulu ya Zanzibar.

Maoni:

Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU) huko Zanzibar iliundwa mnamo 2010 baada ya kura ya maoni ili kumaliza msuguano kati ya kambi kuu mbili za kisiasa. Matokeo ya kura hiyo ya maoni yalikuwa kwamba Wazanzibari wengi walipiga kura kuipendelea.

Kupitia hiyo (GNU) nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Rais iliundwa ambaye anapaswa kutoka chama kingine kisichokuwa kile cha Rais. Makamu wa 1 wa Rais anapaswa kuwa mtu kutoka kwa chama ambacho kilipata sio chini ya asilimia 10 ya kura katika uchaguzi wa rais.

Kufuatia uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020,  ACT Wazalendo, chama kikuu cha upinzani huko Zanzibar, pamoja na Chadema, chama kikuu cha upinzani Tanzania bara vilisusia matokeo vikitaja kasoro na vurugu dhidi ya wapiga kura na wagombea wa upinzani.

ACT ilikataa vikali matokeo ambayo yalimpa Hamad asilimia 19 ya kura na viti vinne pekee katika Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.

Lakini, licha ya msimamo wa awali wa kukataa wa ACT Wazalendo kufuatia kuuwawa kwa zaidi ya wanachama na wafuasi wao kumi wakati wa kile walichokiita uchaguzi usiokuwa wa haki, mwishowe walikubali kushiriki katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambayo Seif Sharrif anashikilia nafasi ya Makamu wa 1 wa Rais, cheo tasa bila ya mamlaka yoyote.

Hatua ya ACT-Wazalendo kujiunga na serikali ya mseto (Serikali ya Umoja wa Kitaifa) imefichua picha wazi kabisa kwamba, vyama vya kisiasa vya kidemokrasia na viongozi wao hawatumikii chochote isipokuwa maslahi yao binafsi na huu ndio msingi wa imani ya kirasilimali.

Licha ya mauaji, ubakaji na uchaguzi usiokuwa wa haki, ACT Wazalendo iliingia katika serikali ya mseto kwa lengo moja tu la kupata maslahi na manufaa ya kibinafsi. Hii ni mara ya pili kwa Sharrif (77) kushika wadhifa huo. Katika kipindi cha kwanza (miaka 5) ya urais wa Dkt Ali Mohammed Shein (2010-2015) alihudumu vivyo hivyo.

ACT-Wazalendo ilitangaza kuwa, uamuzi wao wa kujiunga na serikali ya mseto ulikuwa mahitaji ya katiba ya Zanzibar na vile vile kufanikisha maslahi mapana ya kijamii na kisiasa. Lakini kwa picha pana ilionekana ACT-Wazalendo iko katika kambi ya Amerika kama CCM, na Amerika ilisukuma na kuwezesha ushiriki wa ACT-Wazalendo serikalini kwa sababu kuu tatu:

  1. Kuondolea chama tawala cha CCM (iliyo upande wa Amerika) sura mbaya kufuatia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020 na kukipatia uhalali wa kisiasa.
  2. Kuwadanganya na kuwatuliza Waislamu wa Zanzibar wasisimame na suluhisho lao safi la Kiislamu, badala yake kuwaonyesha kuwa suluhisho la ukandamizaji wa kuuawa, kubakwa na kuteswa linaweza kushughulikiwa tu katika duru za kidemokrasia.
  3. Kupinga na kupunguza ushawishi wa kisiasa wa Ulaya nchini Tanzania kwa kuyeyusha na kupuuza kelele kubwa na shutuma kote ulimwenguni juu ya ukandamizaji wa CCM wa demokrasia zinazotolewa na chama cha upinzani cha Chadema (ambacho kiko upande wa Ulaya).

Amerika ilibariki na kuunga mkono ushiriki wa hivi karibuni wa ACT Wazalendo katika GNU, na balozi wa Amerika nchini Tanzania Donald Wright aliandika kwenye Twitter:

"Ninaipongeza serikali ya Zanzibar na ACT Wazalendo kwa kufuata maridhiano na serikali ya umoja wa kitaifa ambayo yatafanya kazi kwa pande zote za vyama kwa manufaa ya Wazanzibari wote."

Hali ya Zanzibar ni sawa na ardhi nyingine nyingi za Waislamu na maeneo yaliyo na Waislamu wengi ulimwenguni, kutoka Tunisia hadi Turkestan Mashariki.

Viongozi wa vyama vya kisiasa vya Kidemokrasia si chochote isipokuwa ni vibaraka wa wakoloni wa Kimagharibi, hawajali damu wala jasho la watu wao, na wanatumiwa tu kusema uongo kwa raia na kusaidia wakoloni kutumia rasilimali na kuimarisha ushawishi wao katika nchi zinazoendelea.

Kupitia Urasilimali na nidhamu yake ya kisiasa ya demokrasia haswa uchaguzi wa kidemokrasia; jamii isiyo na ulinzi hudhulumiwa, kuuawa na kuteswa kwa ajili ya hawa waangalizi ambao wanafanya kazi kwa ajili ya mabwana zao wa Kimagharibi.

Ni wakati mwafaka Ummah kutambua ujanja wa viongozi wa vyama hivi vya kisiasa na kutafuta suluhisho la matatizo yao kwa msingi wa Kiislamu ambao kwao ukoloni mamboleo utaondolewa katika nchi zetu na ulimwenguni kwa jumla.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Said Bitomwa
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Tanzania

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumamosi, 19 Disemba 2020 14:20

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu