Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mitandao ya Kijamii Imefichua Kufeli kwa Nidhamu ya Kisekula ya Kidemokrasia na Wafuasi Wake!

Habari:

         Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed alizima mitandao mnamo Jumatano, 4 Novemba 2020 wakati alipozindua mashambulizi katika eneo la kaskazini la Tigray. Rais wa Amerika, Donald Trump ananung’unika baada ya kupigwa marufuku na mitandao ya kijamii mikuu kutokana na madai kuwa ndiye mchochezi wa tukio la Jumatano, 6 Januari 2021 wafuasi wake kuvamia Jengo la Capitol Hill. Rais wa Uganda, Yoweri Museveni mnamo Jumanne, 12 Januari 2021 alizima mitandao siku mbili kabla Uchugazi wa Alhamisi, 14 Januari 2021!

Maoni:

Mitandao ya kijamii imepenya na kuwa takribani kila mahali na kusababisha kukosa usingizi kwa hali iliyoko sasa. Kipote cha mabwenyenye kilipanga mchoro wenye sura mbili kwa wamiliki na watumiaji mitandao ya kijamii. Ama kwa wamiliki ambao ni sehemu ya kipote hicho kama vile Facebook, Twitter, YouTube n.k. Wapo kwa ajili ya kufikia malengo mawili makuu: kwanza –kutia faida kwa kuifanya mitandao yao kuwa ya kibiashara na pili –kupenyeza ajenda ovu za kipote hicho kwa maana ya kutoa jukwaa ili kueneza mfumo wa kisekula wa kirasilimali duniani kote kwa njia zote.

Kuhusiana na watumizi wanayo malengo mawili makuu: kwanza –kutia faida kupitia matumizi yao na pili –kuwa ni ngazi-nyenzo ya pili ya upenyezaji wa ajenda ovu ya kisekula ya kirasilimali! Mpango huu wenye sura mbili haujafaulu namna walivyopangilia. Hilo linafichuliwa na matukio ya hivi majuzi kama yalivyotajwa hapo juu yakijumuisha na sio tu kwa kampeni za mitandaoni kama #EndSARS na #BlackLivesMatter. Mitandao ya kijamii imekuwa ni kikombe chenye sumu dhidi ya nidhamu ya kisekula ya kidemokrasia na wafuasi wake na kuharakisha kudondoka kwao hivi karibuni.

Mitandao ya kijamii haikufichua tu upuzi unaojulikana kama uhuru wa kibinafsi na uhuru wa kujieleza; lakini, pia imefichua undumakuwili unaotumiwa kuwadhibiti na kuwakejeli wengine ambao hawafuati sheria na sera msingi zilizopo na zenye kusimamia dola za kisekula. Kwa kuongezea, imethibitisha kuwa ni zana muafaka ambayo imetoa jukwaa kwa wale ambao wametambua kufeli kusikokuwa na shaka kwa mfumo batili wa kisekula wa kirasilimali na kutokuwa ni suluhisho kwa matatizo ya wanadamu na hivyo kutoa hasira zao dhidi yake na wanaoupigia debe.

Inatambulika kuwa mamlaka ya Amerika yako katika hatua za mwisho kabla kuanguka kwake kusipoepukika. Kila mtu mwenye akili na kujiuliza maswali ya kisiasa duniani kote na ambaye alifuatilia safari ya hatari ya kuelekea kuanguka kwa mamlaka ya UK. Ataona kuwa inajirudia tena kupitia Amerika na mitandao ya kijamii inapeperusha matukio hayo kwa njia ya moja kwa moja. Ama kuhusiana na marufuku zinazotolewa na wamiliki wa mitandao hiyo pamoja na tawala zilizo feli ni sehemu tu ya njama kubwa ya kuziba kufeli kukubwa na majanga yaliyo sababishwa na nidhamu ya kisekula ya kidemokrasia na wanaoipigia debe. Ni wafa maji wanaojaribu kuinusuru ilhali wamekata tamaa!

Hatimaye, marufuku hizo zinazidisha madhara zaidi kwa hali iliyoko kwa sababu mfumo wao wa kisekula wa kirasilimali una kasoro na kattu hauwezi kunusurika. Hata vipofu na viziwi wameweza kuona na kusikia machungu mtawalia yanayochipuza kutokana na nidhamu ya kisekula ya kidemokrasia inayougua. Hivyo basi, yale yanayotokea nchini Amerika, inayojiita kinara na ngome ya demokrasia ni uthibitisho wa wazi kwamba demokrasia sio chochote bali ni uongo uliojazwa katika akili za watu na kuwahadaa kwamba wao ni wakuu kuliko Muumba, Allah (swt).

Sasa ni wakati wa nidhamu mbadala ya Khilafah. Nidhamu ambayo imechipuza kutoka kwa Muumba wa ulimwengu, mwanadamu na uhai- Allah (swt). Sio nidhamu ya kubahatisha kama zilizotangulia- awali ujamaa / ukomunisti na sasa urasilimali.  Zote asili yake ni akili iliyo na kikomo ya mwanadamu ambayo haiwezi kutambua dhati ya Muumba wake, Allah (swt) pasina kupata uongofu Wake kupitia Manabii na Mitume wake aliowachagua!  Hivyo basi, nidhamu ya Khilafah msingi wake ni Shari’ah ya Kiislamu (Qur’an, Sunnah, Ijma’ Sahaba na Qiyas). Ni muhimu kwa kila mtafutaji mabadiliko ya kweli awe mmiliki au mtumiaji wa mitandao ya kijamii aliye hai na mwenye kulingania kurudisha tena maisha ya Kiislamu kupitia njia ya kusimamisha nidhamu ya Khilafah kwa njia ya Utume. Sema LA kwa mabadiliko feki!

Imeandikwa kwa ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Ali Nassoro Ali

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 17 Januari 2021 23:27

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu