Jumanne, 22 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Chini ya Urasilimali, Wanawake Waislamu Wanateseka Aina Nyingi za Unyanyasaji

Habari:

Nchini Canada, wanawake wawili wa Kiislamu wamejadili shambulizi kali lililofanywa dhidi yao na wanaume wawili. Wanaume hao walifoka maoni ya ubaguzi wa rangi na kuwatishia kifo. Waliachwa na kiwewe na wanaishi kwa hofu ya kila mara kwa usalama wao. Shambulizi hilo lilitokea mwezi mmoja uliopita lakini wamepata tu nguvu ya kulizungumzia hadharani kwenye habari za CBC mnamo 6 Januari 2021.

"Walichana udanganyifu wa usalama wetu," mwanafamilia mmoja alisema.

Maoni:

Mwaka jana, polisi wa Edmonton nchini Canada waliripoti uhalifu 64 uliochochewa na chuki kuonyesha kwamba utulivu na kutovumiliana ni sifa kuu za kudumaza za jamii za kiliberali za kidemokrasia. Mataifa yote ulimwenguni yana Waislamu wanaokabiliwa na tatizo hili la shambulizi kali na wanawake wa Kiislamu wakiwa walengwa haswa kwa kudhihirisha kwao Uislamu.

Mwanafamilia mmoja aliye na hofu sana kufichua jina lake alisema:

"Dada yangu aliniambia mshambuliaji wake alikuwa na chuki nyingi mno machoni mwake, kiasi kwamba sio tu kwamba alisema anataka kuwaua, lakini hasira zake za kimwili zilimfanya aamini kwamba atawaua wote wawili."

Wazo kwamba uhalifu huu dhidi ya wanawake wa Kiislamu ni jambo la kutarajiwa linaashiriwa kwa njia ya kienyeji ambayo kwayo hushughulikiwa na serikali na watekelezaji wa sheria. Katika ripoti rasmi, inasemekana kwamba polisi walimshtaki Richard Bradley Stevens mwenye umri wa miaka 41, na mashtaka mawili ya shambulizi na moja la ufisadi. Familia hiyo inatoa wito kwa polisi kumshtaki mtu wa pili ambaye wanasema alishiriki katika shambulizi hilo. Lakini, kwa kuwa hakuna madai yoyote yaliothibitishwa kortini hakujakuwa na mashtaka.

Wanawake hao wawili tangu wakati huo wamekuwa waking'ang'ana kutafuta ugumu wa huduma za wahasiriwa na msaada huko Alberta, mwanafamilia huyo alisema.

"Kukutana na mtu baada ya mtu ambaye amejihami vibaya kukabiliana na uhalifu wa chuki kumekuwa kwa kuvunja moyo," alisema. "Tunatumai utekelezaji wa sheria wa jiji utafanya kila wawezalo kuwafikisha wanaume wote wawili mahakamani."

Ukweli kwamba uhalifu wa chuki uliochochewa dhidi ya wanawake wa Kiislamu ni maalum katika hali ya kisiasa unaoweza kuonekana kwa kuwa wiki moja tu baadaye mwanamke mweusi wa Kiislamu mwenye umri wa miaka 23 alishambuliwa katika kituo hicho hicho cha karibu cha Southgate LRT.

Thamani ya wanawake Waislamu ulimwenguni ni sifuri kwani mashambulizi, mauaji ya kupangwa, kukamatwa na mateso yote yanazidi kuongezeka kwa uhalali kamili kutoka kwa kila kinachoitwa wakala wa haki za binadamu. Khilafah pekee kwa njia ya Utume ndiyo iliyochunga heshima ya wanawake wote bila ubaguzi. Tunajua mfano maarufu wa jinsi mwanamke mmoja wa Kiislamu alivyoshambuliwa sokoni na Mutasem mtawala alituma jeshi lote kutoa funzo la mara moja kwa tukio hilo bila kuuliza wala kuchelewa.

Mwenyezi Mungu (swt) hakubali mashambulizi kwa msingi wa jinsia, rangi au dini. Na kuna wanawake Waislamu ambao wanateseka katika viwango vyote hivi.

]يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُم مِّن ذَكَرٍ وَأُنثَى وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ اللَّهِ أَتْقَاكُمْ إِنَّ اللَّهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ]

“Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari.” [Al-Hujurat, 49:13]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu