Ijumaa, 24 Rajab 1446 | 2025/01/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mashini ya Pesa - “Qu’ils mangent de la brioche”

(Imetafsiriwa)

Habari:

BP imeripoti faida yake kubwa zaidi ya robo mwaka kwa miaka 14 baada ya bei ya mafuta na gesi kupanda.

Kampuni hiyo kubwa ya nishati iliona faida ya msingi ikifikia $8.45bilioni (£6.9bilioni) kati ya Aprili na Juni - zaidi ya mara tatu ya kiasi ilichopata katika kipindi kama hicho mwaka jana.

Haya yanajiri huku bili za majumbani za nishati zikiwa zimetabiriwa kugonga zaidi ya £3,600 kwa mwaka msimu huu wa kipupwe.

Faida kubwa zimesababisha wito kwa serikali kuyatoza makampuni kodi zaidi ili kusaidia familia na bili zinazoongezeka.

Faida ya BP zilikuwa za pili kuwa juu kwa robo ya pili katika historia ya kampuni hiyo.

Inafuatia matangazo mengi ya faida kutoka kwa makampuni mengine yakiwemo Shell, Equinor, TotalEnergies na mmiliki wa British Gas Centrica, ambayo yamekuwa yakivuna manufaa ya bei ya juu ya gesi na mafuta. (BBC)

Maoni:

Mshtuko wa aibu. Kejeli kwa watu, huku wakijiinua baada ya janga baya la maambukizi, sasa wanakabiliwa na bei ya juu mno ya nishati na chakula, mfumko wa bei na mateso ambayo hayajaonekanapo hapa tangu Vita vya Pili vya Dunia. Afisi ya Takwimu za Kitaifa iliripoti mfumko wa bei wa Uingereza ulifikia 9.4% katika miezi 12 hadi Juni kutoka 9.1% mwezi Mei. Bili za kawaida za nishati zilipanda kwa £700 mwezi wa Aprili, na kutabiriwa kuongezeka tena kwa £1,200 mwezi Oktoba.

António Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, alilazimika kulaani ‘rekodi ya faida isiyo na maadili’ ya makampuni makubwa ya nishati ambayo yalipata faida ‘mgongoni mwa watu maskini zaidi’, jumla ya dolari bilioni 100 katika robo ya kwanza ya mwaka huu.

Je, bei za nishati zinawezaje, kuwa juu kikatili hivi katika taifa ambalo lina mafuta na gesi? Je, faida hizi ‘zisizo na maadili’ zimetoka wapi? Alok Sharma, aliyekuwa Waziri wa Biashara, Nishati na Mkakati wa Kiviwanda kwa serikali ya Uingereza alitoa maelezo ya kibepari kwenye Sky News, Januari 24 mwaka huu, "Tunakabiliwa na bei ya jumla ya gesi ya kimataifa. Unajua, hata kama tungekuwa tunachimba zaidi hivi sasa kutoka bonde la Bahari ya Kaskazini, hatimaye bei, ‘itakayotolewa’, itakuwa kwenye bei ya jumla ya gesi ya kimataifa.”

Ujumbe? Sio kosa la serikali. Hakuna kitu serikali inachoweza kufanya.

Kile wasichowaambia umma, ni kwamba marafiki zao matajiri wa kibepari wanakusanya kwenye ‘mashini ya pesa’ hii, kwa kuuza kwa bei ya juu zaidi wanaweza ‘kuzalisha’ kwenye soko la dunia, ili kuwasha moto kwa watu.

Na vyombo vyao vya habari vinashiriki kuendeleza masaibu haya. 'Vyombo vikuu vya habari' vinavyomilikiwa na wanahabari mabwenyenye wa kirasilimali, hufanya kazi kwa bidii kupotosha, kuvuruga na kueneza hasira na maumivu ya umma - simulizi ya kibepari ni: Kuna dosari katika kila kitu, janga la maambukizi, mwisho wa janga la maambukizi, mahitaji, ukosefu wa mahitaji, 'vita' vya Urusi nchini Ukraine, sio Brexit, - 'waungu watatu kwa jina fates', yaani, 'wao ndio wenye udhibiti, hakuna kitu kinachoweza kufanywa, na kwa taarifa yako, ulimwengu mzima una maumivu pia.' Vyombo vikuu vya habari, huhakikisha serikali zinazolinda, kuhalalisha, kuhifadhi faida zao chafu na maslahi ya kilafi, ya matajiri zinatawala.

Urasilimali huhujumu demokrasia na kuupindisha mfumo kuwanufaisha matajiri.

Hii ni makosa, sio haki.

Tatizo msingi ni urasilimali umefeli vibaya mno, unadhulumu vibaya sana pindi unaposhughulikia mahitaji muhimu na ya kimsingi.

Ukweli kwamba nishati ni hitajio muhimu sana, huifanya ‘hitaji lisilo nyumbuka’ - watu wanahitaji nishati kwa maisha ya kila siku, wanalazimika kulipa bila kujali bei gani. Kikweli ni aina ya ukiritimba. Ina maana, kila udhibiti wa uzalishaji wa nishati ukiwa mkubwa, ndivyo wanavyopata faida zaidi! Mabepari wanashikilia uhai wetu mikononi mwao.

Ni nyenzo msingi ya maisha ya kila siku, kuanzia usafiri, viwanda, afisi, shule, hospitali zote zinahitaji nishati. Bei ya nishati inapopanda athari huongezeka na kuathiri nyanja zote za maisha, na kuongeza mateso ya mfumko wa bei.

Makampuni makubwa ya nishati, yanageuza papatiko na taabu zetu, kuwa faida mwanana. Katika urasilimali, mafuta na gesi, utajiri wa madini wa taifa, sio kwa manufaa ya watu. Ni kwa manufaa ya matajiri wachache wa kibepari.

Msiba huu haungefikirika ndani ya Khilafah. Imepokewa kutoka kwa Ibn Majah kutoka kwa Abu Hurairah radhiallahu anhu, kwamba Mtume swallallahu alayhi wa sallam amesema:

«المسلمون شركاء في ثلاث: في الماء والكلأ والنار» Waislamu ni washirika katika vitu vitatu: katika maji, malisho na moto.”

Mfumo wa Uislamu (Shari’ah) unaainisha utajiri wote wa madini katika kundi maalum ‘al-milkiyyah al-ammah’ - mali ya umma, inayomilikiwa na wote. Haiwezi kumilikiwa na watu binafsi, wala haiwezi kumilikiwa na serikali (kutaifishwa). Kinyume na urasilimali na ujamaa/ukomunisti, utajiri wote wa madini, yakiwemo mafuta na gesi, ni kwa manufaa ya watu, unaosimamiwa na Dola kwa niaba ya watu.

Na tofauti na unyonge wa dhahiri wa serikali za mabepari zenye nguvu za ulimwengu, Khalifah (Khalifa) na magavana wake bila shaka watahesabiwa, binafsi, endapo raia ‘wataongezewa bei’ ya nishati, sembuse kuteseka wakati inapatikana kwa wingi. Shari’ah, mfumo wa Uislamu unawasimamia wote, haswa wale walio hatarini na wanyonge.

Baada ya kushika madaraka, Khalifa wa kwanza wa Uislamu, Abu Bakr (ra) aliwahutubia watu: “Nimepewa mamlaka juu yenu, na mimi si mbora wenu. Nikifanya vyema, nisaidieni; na nikikosea, niwekeni sawa. Kuheshimu ukweli ni uaminifu na kutojali ukweli ni usaliti. Mnyonge miongoni mwenu kwangu mimi ni mwenye nguvu mpaka nimpe haki yake, Mwenyezi Mungu akipenda; na mwenye nguvu miongoni mwenu kwangu ni dhaifu mpaka nimnyang'anye haki za wengine, Mwenyezi Mungu akipenda....” (Al-Bidayah wan-Nihayah 6:305, 306).

Sio kwa matajiri na wenye nguvu au maskini na mafukara, kuamua jema na baya. Ulimwengu haujawahi kuona mateso na misukosuko iliyoenea kama hii katika kumbukumbu hai. Katika kipindi chao kifupi cha utawala, urasilimali na ujamaa imeleta umaskini na taabu duniani. Uislamu ulitabikisha hadhara adilifu, yenye huruma, na angavu iliyowajali masikini na matajiri, kwa jamii zote na itikadi zote, kwa zaidi ya milenia moja.

Tunahitaji kwa haraka kurudi kwa Uislamu, kwa ajili ya Waumini na watu wote wema duniani.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammad Hamzah

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu