Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kura ya Maoni nchini Uzbekistan: Operesheni “Raisi wa Milele”

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo Aprili 30, 2023, Uzbekistan ilipiga kura katika kura ya maoni ya katiba ambayo inaweza kumruhusu Rais Shavkat Mirziyoyev kuongeza muda wake wa uongozi kwa miaka 14, kwa mujibu wa tovuti ya Idhaa ya Televisheni ya Aljazeera. Iwapo kura ya maoni ya Jumapili itapita, muhula wa urais utaongezwa kutoka miaka mitano hadi saba. Mabadiliko hayo yatamruhusu Mirziyoyev, 65, kuhudumu mihula miwili zaidi na kuongeza muda wake wa kukaa madarakani hadi 2040.

Mamlaka katika jamhuri ya zamani ya Usovieti yenye watu wengi zaidi ya Asia ya Kati zimesema marekebisho hayo ya katiba yataboresha utawala na ubora wa maisha katika nchi hiyo yenye Waislamu milioni 35. Serikali pia ilisema kura hiyo ya maoni itaanzisha mageuzi ya haki za binadamu.

Tangu aingie madarakani mwaka 2016 baada ya kifo cha mtangulizi wake Islam Karimov, Mirziyoyev ameongoza mageuzi kadhaa nchini Uzbekistan, ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku kazi ya kulazimishwa katika mashamba ya pamba. Lakini wanaharakati walisema ukiukaji wa haki unaendelea na mamlaka hazionyeshi dalili za kuruhusu upinzani wa kisiasa kuibuka. Mnamo 2022, watu wasiopungua 21 waliuawa wakati wa maandamano katika jimbo linalojitawala wenyewe la Karakalpakstan. Wanaharakati wa haki za binadamu walizituhumu mamlaka kwa kutumia silaha dhidi ya waandamanaji. (Aljazeera.com)

Maoni:

Uzbekistan ni moja ya lulu za thamani za Umma wa Kiislamu. Katika eneo la nchi hii walizaliwa maimamu-muhaddithina kama al-Bukhari na at-Tirmidhi, mienge ya sayansi ya ulimwengu kama vile al-Khwarizmi, al-Biruni, Ibn Sina, na wengineo. Lakini thamani hii si tu kutokana na historia yake ya kale, eneo la kijiografia na maliasili tajiri zaidi. Hazina muhimu zaidi ya Uzbekistan, pamoja na nchi zingine za eneo hili, ni Waislamu wanaokaa humo, ambao wamedumisha mshikamano mkubwa wa Uislamu, licha ya ukoloni wa Urusi na ugaidi wa Kikomunisti.

Serikali tawala ya Uzbekistan, kama nchi zingine za baada ya zama za Usovieti za Asia ya Kati, ni mgawanyiko wa nomenklatura ya chama cha kikomunisti. Wakati wa enzi ya Usovieti, jukumu lake kuu lilikuwa kupigana dhidi ya Uislamu, kupitia ukandamizaji na elimu ya kipagani, na pia kugawanyika kwa umoja wa Waislamu kulingana na sera ya kitaifa ya Kistalini. Urusi ilitaka kuwafinyanga Waislamu pamoja na watu wengine wote wa USSR kuwa "watu wa Kisovieti", kuipiga vita dini, kubadilisha maandishi ya Kiarabu kwa ya Kirusi, na kuanzisha kanuni za maadili zilizo ngeni kwa Uislamu.

Kwa madhumuni haya, wakomunisti walichagua watu duni kabisa kutoka kwa Waislamu na kuwaweka kama wakuu wa jamhuri zilizoundwa kwa msingi wa kitaifa. Waliolelewa katika roho ya ushabiki wa vyama, wanaojali tu ustawi wa kibinafsi na utajiri, na, baada ya kuwa kama wafalme, walianza kuwakandamiza watu wao, wakijizungusha pambizoni mwa maafisa wapambe na wafisadi. Kila moja ya satrap hizi za ndani zilisimamiwa na mkomunisti aliyeteuliwa maalum kutoka Moscow, aliyetumika kama katibu wa pili wa vyombo vya chama cha kijamhuri.

Baada ya kuondolewa kwa mfumo ya kikomunisti katika mkesha wa kuanguka kwa Muungano wa Kisovieti, walibakisha mamlaka mikononi mwa koo zao, wakijigeuza kuwa wanademokrasia na wanamageuzi. Kwa kubadilishana na ushawishi dhaifu wa Urusi, walikimbilia kutafuta ufadhili wa Magharibi na China, na wakati huo huo wakivunja polepole mafungamano ya kisiasa, kijeshi, kiuchumi na wengine na Urusi ambayo yaliendelea wakati wa utawala wake usiogawanyika katika eneo hilo. Wanaendelea kufanya biashara kwa maslahi ya watu wao, kama ilivyokuwa hapo awali, sasa tu chini ya viapo vya kujitolea kwa demokrasia na haki za binadamu, na si kwa ukomunisti.

Serikali ya sasa ya Uzbek, inaoongozwa na Mirziyoyev, ingawa haionekani kuwa ya kuchekesha kama, kwa mfano, serikali ya nchi jirani ya Turkmen au Tajik, ni mbaya tu, yenye ujanja na ukatili. Yeye hajali kabisa mahitaji na shida za raia wa kawaida, na anajishughulisha na maslahi yake ya kibinafsi na kiburi. Kwa hivyo, hata na akiba tajiri ya gesi asilia, mafuta, dhahabu, urani, metali zisizo na feri na madini mengine, watu wengi wa Uzbekistan wanaishi katika umaskini wa kupitiliza, wakikosa umeme na joto. Ili kulisha familia zao, mamilioni ya wanaume na wanawake wanalazimika kwenda kufanya kazi nchini Urusi, Kazakhstan na nchi zengine, wakikabiliwa na udhalilishaji, ubaguzi na tishio kwa afya zao na hata maisha yao.

Licha ya ukweli kwamba Mirziyoyev anataka kujitenga na "mchinjaji wa Andijan" Karimov, yeye ndiye mrithi wake. Baada ya kuwasafisha makada wa zamani katika vyombo vya sheria, badala yake aliwaweka watu ambao kuanzia sasa watakuwa na deni kwa "mafanikio ya kitaaluma" yao binafsi kutoka kwake. Akitangaza msamaha kwa kisingizio cha ukombozi, aliwaachilia kutoka gerezani idadi ya wafungwa wa kisiasa ambao umri na hali yao ya afya ilikuwa karibu kifo. Wakati huo huo, maelfu ya Waislamu, waliokamatwa kwa jinai na kutupwa gerezani na Karimov kwa sababu tu walikuwa na bidii katika njia ya Mwenyezi Mungu, wanaendelea kutumikia vifungo virefu na vya maisha, wakikabiliwa na unyanyasaji na mateso makali zaidi. Zaidi ya hayo, idadi yao inaongezeka kutokana na mapambano yanayoendelea ya utawala wa Uzbekistan kwa kufufua kitambulisho cha Kiislamu.

Ni vita dhidi ya Uislamu na Waislamu wenye fahamu ambavyo vinaupa uhalali utawala wa Uzbekistan mbele ya nchi za Magharibi, ambayo iko tayari kumsamehe kwa hili na ufisadi wa mfumo huo, na mateso ya upinzani wowote, na ukiukaji wowote wa haki za binadamu. Baada ya yote, hakuna mtu anayetilia shaka kwamba lengo kuu la kubadilisha Katiba katika kura ya maoni ya sasa, iliyopewa jina la utani na waandishi wa habari wa Magharibi kama "Operesheni ya Raisi wa Milele", ni kupanua mamlaka ya urais ya Mirziyoyev. Na kauli zote kuhusu ukombozi na demokrasia ni vazi tu la ahadi tupu zinazofinika dhati ya kimabavu ya utawala wa Uzbekistan. Lakini hata kama ataweza kuwa na angalau moja kati ya hizo, hii itakuwa ni nyongeza ya kupendeza kwao - hatua iliyo mbali na Uislamu kuelekea kwenye mfumo wa kisekula.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Mustafa Amin
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Ukraine

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu