Jumatatu, 27 Rajab 1446 | 2025/01/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Anayechukua maagizo kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Hutawala kwa Mujibu wa Uislamu,

Sio kwa Mujibu wa Usekula na Demokrasia, Ewe Erdogan!

(Imetafsiriwa)

Habari:

Je, Bw Kemal na wafuasi wake wanapata wapi maagizo yao? Kutoka kwa magaidi huko Kandil. Na sisi tunapokea maagizo kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Je, mnamo tarehe 14 Mei, tuko tayari kuwazika wale wanaochukua maagizo kutoka mlimani? Sina shaka na hilo. (Haber7, 03/05/2023)

Maoni:

Erdoğan, ambaye hana simulizi iliyobaki kuwasilisha na kuelezea kwa umma, kando na kusambaza fikra nyingi na kufanya ufunguzi baada ya ufunguzi ili kushinda uchaguzi ujao wa Mei 14, pia anacheza na hisia za Kiislamu za Waislamu, anatumia hisia zao na kuutaja uchaguzi kuwa ni pambano baina ya haki na batili, baina ya wanywaji mvinyo na wanaosujudu, baina ya wanaokanyaga zulia la swala na viatu vyao na wale wanaoweka vipaji vyao juu yake. Anasema kwamba wapinzani wanawakilisha Magharibi na kuchukua maagizo kutoka kwa shetani, huku yeye akiwakilisha haki na kuchukua maagizo kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Kwa kweli, wanasiasa na vyama vya kisiasa vya kisekula nchini Uturuki ni wawakilishi wa batili, sio haki, na wanachukua maagizo kutoka Uingereza au Marekani, sio kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Kwa sababu muelekeo na kauli mbiu ya wale wanaochukua maagizo kutoka kwa Mwenyezi Mungu ingekuwa ni Qur’an na Sunnah, lakini mwelekeo na kauli mbiu ya wanasiasa na vyama vya kisekula nchini Uturuki ni usekula na demokrasia, na kibla chao ni Marekani au Uingereza. Kwa hivyo, mapambano ya vyama vya kisekula na kidemokrasia nchini Uturuki ni mapambano ya batili, sio ya haki na batili, kwa maana nyengine, mapambano ya kafiri mkoloni Marekani na Uingereza. Tofauti pekee kati yao ni kwamba wahafidhina, wale wanaojiita Waislamu laini na wanaukoo, ambao uti wa mgongo wao unaundwa na AKP inayounga mkono Marekani na MHP (Muungano wa Republican), wanaficha kitambulisho chao cha kisekula wa "Kiislamu" kwa kujifanya Waislamu, na kutumia Uislamu kama chombo cha malengo ya kisiasa ya Amerika. Kwa upande mwingine, wana Kemal laini na wasanii, ambao uti wa mgongo wao unaundwa na CHP inayounga mkono Uingereza na IYI Party (Muuangani wa Taifa), wanajaribu kusahau historia yao chafu iliyopita kwa mijadala ya Kiislamu ambayo haiendani na vinywa vyao kwa sababu maisha yao ya nyuma yamejaa chuki ya Uislamu, na wanajaribu kuutumia Uislamu kama chombo cha malengo ya kisiasa ya Uingereza kwa kujigeuza kuwa Waislamu ili kuficha kitambulisho chao cha kisekula chenye chuki na Uislamu. Kwa maana nyengine, mmoja wao ni gwiji na mtaalamu wa mauzauza ya “Kiislamu” huku mwengine akijitahidi kuwa mcheshi wa “Kiislamu” lakini wote wawili wana lengo moja: kuhakikisha uendelevu wa mfumo wa Kishetani na muovu wa kisekula na kidemokrasia na kuzuia mfumo wa Kiislamu (Khilafah) kuingia madarakani.

Kwa hakika, Erdoğan kwa kauli "Bwana Kemal anachukua maagizo kutoka kwa magaidi huko Kandil. Tunapokea maagizo kutoka kwa Mwenyezi Mungu", anakiri kwa lugha ya ustadi sana kwamba hakuna mtu anayeweza kuelewa kwamba mzozo wa kisiasa nchini Uturuki ni kati ya wafuasi wa Marekani "Wafuasi wa Mwenyezi Mungu" ambao, kama nilivyotaja hapo juu, wamebobea katika kuutumia Uislamu kama nyenzo ya matamanio yao ya kisiasa na wana Kandil wanaounga mkono Uingereza.

Kwa upande mwingine, matamshi ya Erdoğan hayaendani na hali halisi ya Uturuki. Erdoğan hachukui maagizo kutoka kwa Mwenyezi Mungu katika uchumi, siasa, sera za kigeni, maisha ya kijamii, elimu, kwa ufupi, katika nyanja zote za maisha. Lau angechukua maagizo kutoka kwa Mwenyezi Mungu, angeifuta riba badala ya kuipunguza kwa mujibu wa amri ya Mwenyezi Mungu, asingejifungamanisha na maadui wa Uislamu na Waislamu, Urusi na Marekani katika siasa za nje, asingetabikisha usekula. katika elimu na demokrasia katika utawala, na asingetoa uhuru kwa pombe na uasherati. Ni dhahiri kwamba Erdoğan anatawala kulingana na usekula na demokrasia katika kila nyanja ya maisha. Hatutaelezea hili kwa urefu hapa, hii ni mifano tu.

Mtu anayechukua amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu atatabikisha Uislamu katika kila kipengee cha maisha, si kwa maneno bali kwa vitendo, kama Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na Makhalifa Rashid baada yake. Njia ya kufanya hivi sio demokrasia bali ni Khilafah. Maadamu hakuna Khilafah, hakuna uhalisia katika ukweli wa kuchukua maagizo kutoka kwa Mwenyezi Mungu au kutabikisha Uislamu katika maisha, ni udanganyifu tu. Waislamu hawapaswi kuanguka katika mtego huu. Wanapaswa kukaa mbali na wale wanaotumia mazungumzo ya Kiislamu tu na wale wanaojaribu kutumia mazungumzo ya Kiislamu. Wanapaswa kususia miungano yote miwili katika uchaguzi. Hakuna kitu kinachoitwa la hafifu katika madhara mawili, yote ni maovu, hakuna kheri inayotarajiwa kutoka kwa uovu.

[وَمَنْ أَحْسَنُ قَوْلًا مِّمَّن دَعَا إِلَى اللَّهِ وَعَمِلَ صَالِحًا وَقَالَ إِنَّنِي مِنَ الْمُسْلِمِينَ]

“Na ni nani mbora wa kusema kuliko aitaye kwa Mwenyezi Mungu na akatenda mema, na akasema: Hakika mimi ni katika Waislamu?” [Fussilat: 33]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Ercan Tekinbaş

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu