- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Dhalimu wa Uzbekistan Ajaribu Kukandamiza Madhihirisho ya Uislamu katika Jamii
(Imetafsiriwa)
Habari:
Mnamo tarehe 16 Septemba Radio Liberty iliripoti: "Kampeni dhidi ya ufugaji ndevu na uvaaji hijab kwa mara nyingine tena imepamba moto nchini Uzbekistan. Picha za video zilizotumwa kwa Ozodlik mnamo tarehe 13 Septemba zinaonyesha wanafunzi wa kike katika Chuo cha Benki huko Andijan, waliovaa hijab, wakiambiwa wafunge hijab zao tofauti, mafundo yakiwa mgongoni. Wanafunzi wanaokataa kufuata kanuni hizo hawaruhusiwi kuingia chuoni. Marufuku ya hijab miongoni mwa wanafunzi pia imezingatiwa katika majimbo mingine ya Uzbekistan.
Kampeni ya kupinga ufugaji ndevu na uvaaji hijab inajiri huku bunge la Uzbekistan likipitisha marekebisho ya Kanuni za Maadili Maeneo ya Umma. Kulingana na vyanzo, katika mkutano maalum wa serikali uliofanyika mnamo tarehe 10 Septemba, Waziri Mkuu Abdulla Aripov "aliwaonya" watumishi wa umma juu ya matokeo ya kutembelea misikiti".
Maoni:
Mamlaka za Uzbek mara kwa mara hushambulia Uislamu na Waislamu kwa njia tofauti tofauti. Hivi majuzi, Bunge lilipitisha mswada unaopeana jukumu la kiutawala kwa ndoa za wake wengi, na maimamu mafisadi waliunga mkono uamuzi huo wa mamlaka.
Sasa kuna uvamizi kwenye masoko na maeneo ya umma katika kutafuta Waislamu wenye ndevu. Wanaume wamefungwa na kutakwa kunyoa ndevu zao papo hapo. Mikahawa iliyopewa chapa ya Halal imesakwa, baada ya hapo mingi ikafungwa.
Mamlaka za kihalifu zinajaribu kufuta dhihirisho lolote la Uislamu katika jamii. Mtu anaweza kusema kuwa Waislamu wanaingizwa kwenye barabara, lakini Waislamu wa Uzbekistan ni kama matawi ya miti ambayo huvunja barabara na kwa mara nyingine tena wanafurahisha macho na moyo kwa nguvu zao na uthabiti wao katika mapambano dhidi ya Taghut.
Uislamu ulikuja Asia ya Kati katika zama za Maswahaba. Tangu wakati huo, Waislamu wa ardhi hizi wamepitia panda shuka. Kwa kuanguka Khilafah, kwa Waislamu wa ardhi hizi, kama kwa Waislamu wote wa ulimwengu, hasara imekuwa kali zaidi kuliko hapo awali. Lakini licha ya mateso, hasara na majaribu haya yote, Uislamu umetulia makini nyoyoni mwa watu hawa. Na kwa neema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, Khilafah Rashida, itasimamishwa tena hivi karibuni, na Waislamu wa Uzbekistan watapumua afueni na kufurahi katika ushindi wao! Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema katika Kitabu chake Kitukufu:
(وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُم فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَلِكَ فَأُوْلَئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ)
“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [24:55].
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Eldar Khamzin
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir