Jumatano, 25 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Hakuna Uamuzi wa Kisiasa wa Mahakama Utakaositisha Wito wa: “Israel” Lazima Iondolewe na Palestina Yote Ikombolewe

Mnamo siku ya Jumanne tarehe 25/6/2024, nilihukumiwa kifungo cha nje siku 60 katika Mahakama ya Jiji la Copenhagen kwa kutoa wito wa ukombozi wa Palestina. Jaji anayeendesha kesi aliamua wakati wa kutoa hukumu kwamba hotuba yangu ya 2021 katika suala hilo haikuelekezwa kwa Mayahudi kama kundi la kidini, lakini alitoa wito wa kuondolewa kwa umbile haramu la Kizayuni linaloitwa “Israel” kupitia uingiliaji wa kijeshi. Wito huu ulitangazwa na mahakama ya jiji kuwa sio halali!

Soma zaidi...

Jitihada Zinazorudiwa rudiwa, za Kutapatapa za Kuinasibisha Hizb ut Tahrir na Uanamgambo, ni Kwa sababu Magharibi Inaogopa Kuporomoka kwa Mfumo Wake Fisadi wa Kilimwengu, katika Ulimwengu wa Kiislamu

Ni dhahiri kwamba mfumo wa Hizb, Uislamu, ni tishio la kuwepo kwa mfumo wa kilimwengu wa Magharibi. Uislamu unakataa ubwana wa akili ya mwanadamu, na haki ya wanadamu kutunga sheria. Uislamu unatangaza ubwana pekee ni wa Mwenyezi Mungu (swt), na utabikishaji hukmu za Shariah. Uislamu unaamuru kuunganisha Ummah kama Umma mmoja, na unakataa mipaka ya kitaifa ambayo iliwekwa na wakoloni makafiri, ili kuwagawanya Waislamu katika zaidi ya dola hamsini.

Soma zaidi...

Ubinafsishaji Tayari Umeharibu Sekta ya Kawi, Ilhali Watawala Wangali Wanafuata Maagizo ya Angamivu ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF)

Katika Khilafah, chanzo kikubwa cha utajiri katika uchumi, nishati, kinagawiwa watu, kwa pamoja. Kutokana na mtazamo wake wa kipekee wa umiliki, Uislamu unahakikisha mzunguko wa mali katika jamii. Uislamu unazuia mali kujilimbikiza mikononi mwa wawekezaji wachache.

Soma zaidi...

Mtazamo wa Serikali Tawala katika Uchimbaji Migodi Unaziimarisha Dola Adui (Muharib) na Kuwadhoofisha Waislamu wa Afghanistan

Wizara ya Madini na Petroli ya Afghanistan imetangaza kuwa katika kipindi cha miaka miwili na nusu iliyopita, zaidi ya dolari bilioni saba zimewekezwa katika sekta ya madini nchini Afghanistan. Katika mchakato huu, kando na makampuni ya ndani, makampuni kutoka Qatar, Uturuki, Urusi, Iran, China na Uingereza pia yamechukua dori kubwa. Huu unachukuliwa kuwa uwekezaji mkubwa zaidi katika uchimbaji madini katika historia ya Afghanistan.

Soma zaidi...

Kesi ya Kisiasa Inafichua Uungaji Mkono wa Denmark kwa Uvamizi wa Mauaji ya Halaiki

Serikali ya Denmark inaendelea na uungaji mkono wake wa dhati kwa uvamizi wa Kizayuni wa Palestina na mauaji ya halaiki yanayoendelea huko Gaza, ambayo yameitia hofu kila nafsi adhimu katika sayari hii, na kuwaamsha watu kuona kwamba vima vinavyodaiwa vya dola za Magharibi vimezikwa na maiti hizo za maelfu ya wanawake na watoto chini ya magofu ya Gaza. Haki za binadamu, haki ya kuishi na kujiamulia, haki za wanawake na ustawi wa mtoto - yote haya yanatupwa chini ya tingatinga la Uzayuni na wanasiasa na mamlaka, ambao kwa hivyo wanaonyesha unafiki wao wa hali ya juu na kufichua jinsi gani "vima" hivi kivitendo ni ala tu za kisiasa.

Soma zaidi...

Kuwekwa Kizuizini kwa Sababu ya Majadiliano Tu ya Hadhara kuhusu Kanuni za Shariah ya Kiislamu katika Demokrasia Kubwa Zaidi Duniani

Mamlaka za polisi kutoka jimbo la Tamil Nadu nchini India zimeripoti kuzuiliwa kwa Waislamu sita kwa kufanya amali za Hizb ut Tahrir (HT). Watu hao waliokamatwa ni pamoja na Dkt Hameed Hussain, ambaye ana shahada ya uzamifu ya Uhandisi Mitambo, Baba yake Hussain Ahmed Mansoor na kaka yake Abdul Rehman ambaye ni Msomi wa Kiislamu na wengine watatu, Mohammed Maurice, Khader Nawaz Sherif na Ahmed Ali.

Soma zaidi...

Pongezi za Idd Al-Adha Iliyobarikiwa 1445 H

Hizb ut Tahrir inatoa pongezi na baraka zake za dhati kwa Umma wa Kiislamu, wenye kulemewa na majeraha na kustahamili shinikizo la moja kwa moja na lisilo la moja kwa moja la kikoloni. Kwa mnasaba huu, tunawataja makhsusi watu wetu wenye subira mjini Gaza Hashim na kwa jumla katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, tukimuomba Mwenyezi Mungu azifanye siku za Idd hii kuwa chanzo cha utulivu wa nyoyo zao.

Soma zaidi...

Mauaji ya Nuseirat Yanafichua Dini ya Ukafiri Na Yanafichua Ufadhili na Uungaji Mkono wa Marekani kwa Umbile la Uhalifu

Mnamo tarehe 8 Juni 2024, umbile la Kiyahudi lilifanya mauaji ya kutisha katika kambi ya Nuseirat katika Ukanda wa Gaza kwa usaidizi wa Marekani kwa kisingizio cha “kuwaokoa wafungwa 4” wanaozuiliwa na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu (Hamas) na kuwakomboa kutoka mikononi mwake.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu