Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Hawajaridhika na Uharibifu wa Gaza, Wazayuni Sasa Wanaendeleza Uhalifu Wao hadi Lebanon

Baada ya mwaka mmoja wa kampeni ya wazi ya mauaji ya halaiki dhidi ya watu wa Palestina, iliyofanywa mchana kweupe kwa ushirikiano wa dola za kimataifa na watawala wa Waislamu wanaowazunguka, Wazayuni hivi sasa wameendeleza jinai zao hadi Lebanon kwa kulipua mabomu kiholela katika makaazi yenye wakaazi wengi, na kuua maelfu ya watu tayari, kwa matumaini wanaweza kurekebisha sura yao iliyoshindwa baada ya kampeni yake angamivu mjini Gaza.

Soma zaidi...

Kama Umma Mmoja: Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa Kuangamizwa kwa Dhalimu Hasina na Tunawaombea Kuporomoka Madhalimu Wote Wanaoukandamiza Ummah

Baada ya majuma kadhaa ya ukandamizaji wa kikatili dhidi ya watu wa Bangladesh na dhalimu Hasina, genge la serikali yake, na wachungaji wake wa kigeni, alilazimishwa kidhalilifu kuikimbia nchi. Waislamu shupavu wa Bangladesh, wakiongozwa na wanafunzi jasiri, walivumilia ukatili usio na kifani na hatimaye kulazimisha kuondolewa kwake kupitia wimbi lisilozuilika la maandamano ambayo yalimshinda dikteta huyo.

Soma zaidi...

Kama Umma Mmoja: Waislamu Wanasimama pamoja na Watu wa Bangladesh Dhidi ya Dhalimu Sheikh Hasina

Watu wa Bangladesh—zaidi ya 92% yao ni Waislamu na sehemu ya mojawapo ya Waislamu wengi zaidi duniani—wamejitokeza katika maandamano ya amani yanayoongozwa na wanafunzi dhidi ya dhalimu Sheikh Hasina. Maandamano ya hivi punde yalizuka baada ya serikali inayoongozwa na Hasina kujaribu kuongeza mgawo wa nafasi za kazi serikalini kwa kuwapendelea wafuasi watiifu wa serikali badala ya wagombea wenye sifa stahiki. Sera hii ni ya hivi punde tu katika mfululizo wa vitendo vya rushwa na uonevu vinavyofanywa na serikali ya Awami League tangu iingie mamlakani mwaka wa 2009.

Soma zaidi...

Kujadili Yasiyoweza Kujihami

Baada ya juhudi zilizoratibiwa za Wazayuni zenye lengo la kukashifu sauti zinazoiunga mkono Palestina, zilizoundwa na mfululizo wa makala ya magazeti ya udaku na vipindi vya TV vinavyofafanuliwa kwa batili na dosari, ilidhihirika kwamba wengi wao hawakustahili jibu la heshima hata kidogo.

Soma zaidi...

Domo Tupu la Serikali ya Australia juu ya 'Maeneo ya Wapalestina Yanayokaliwa Kimabavu' Linaficha Uhalifu wake katika Kuwezesha Ukaliaji Kimabavu wa Palestina Yote

Serikali ya Kifederali la Labor jana iliongeza mazungumzo yake mtupu juu ya Palestina kwa kuthibitisha Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza kama 'maeneo yaliyokaliwa kimabavu', na makaazi yoyote kwenye ardhi hizi kama 'yasiyo uhalali wa kisheria' na hufanya kuwa 'ukiukaji wa sheria za kimataifa'.

Soma zaidi...

Serikali ya Australia Yatafuta Kupiga Marufuku Nembo za Uislamu kwa Kisingizio cha Ugaidi

Serikali ya Australia leo imeashiria kuanzishwa kwa sheria inayolenga kuharamisha nembo za chuki.

Mark Dreyfus, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Majimbo, alisema hivi leo katika taarifa yake kwa vyombo vya habari: “Serikali ya Albanese leo imeanzisha mageuzi ya kina ili kulinda jamii dhidi ya wale wanaotaka kueneza chuki na kuwachochea wengine kufanya vitendo vya ugaidi.”

Soma zaidi...

Uhalifu wa Kivita wa Mkongwe wa Vita Aliyepambwa Zaidi wa Australia ni Akisi ya Sera ya Vita ya Serikali

Madai ya uhalifu wa kivita dhidi ya mkongwe wa vita aliye hai nchini Australia, Ben Roberts-Smith, yalipatikana kuwa "kweli kabisa" na jaji wa Mahakama ya Shirikisho. Jaji huyo alihitimisha kuwa madai ya kuwashambulia na kuwaua Waafghani wasio na hatia na wasio na silaha yalithibitishwa, na kwamba alileta fedheha kwa nchi yake na jeshi la Australia kwa kuvunja 'kanuni za maadili na kisheria' za ushiriki wa kijeshi.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu