Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  25 Rabi' II 1444 Na: 1444 H / 11
M.  Jumamosi, 19 Novemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Jaribio la ATU la Kuwabandika Majina Wanachama wa Hizb ut Tahrir waliokuwa Wazungumzaji wa Makongamano ya Kisiasa ya Mtandaoni kuwa ni Wanamgambo ni Kitendo cha Ugaidi na Ukandamizaji

(Imetafsiriwa)

Serikali ya Hasina ilifanya jaribio jengine lililofeli la kusitisha dawah ya Hizb ut Tahrir katika kurudisha Mfumo kamili wa Maisha wa Kiislamu kupitia kusimamisha tena Khilafah Rashida kwa kuwahangaisha na kuwakandamiza wanachama wake kupitia kikosi chake maarufu cha kigaidi kinachojulikana kama "Kitengo cha Kupambana na Ugaidi (ATU)”. Kitengo cha Kupambana na Ugaidi (ATU) cha Polisi wa Bangladesh katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa mnamo Jumatano kwa vyombo vya habari kiliwataja baadhi ya watoto shupavu wa Umma ambao waliokuwa ni wazungumzaji wa makongamano ya mtandaoni yaliyoandaliwa na Hizb ut Tahrir kuwa ni magaidi na wanamgambo na kutaka msaada wa umma wa kuwakamata.

Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh inalaani vikali kitendo hiki cha kiovu, kilichoshindwa, na cha kutapa tapa cha serikali. Hizb ut Tahrir inajulikana vyema kama chama cha kifikra kisicho na vurugu na tayari kimejikita vyema katika jamii na kinakumbatiwa na matabaka yote ya watu. Hizb ut Tahrir inawalingania watu kwenye mapambano yake ya kisiasa na mvutano wa kifikra ili kuregesha dola ya Khilafah kwa sababu ni faradhi juu ya Waislamu wote na sio juu ya Hizb ut Tahrir peke yake. Hizb ut Tahrir imekuwa ikifanya kazi ya kujenga ufahamu jumla na rai jumla kwa ajili ya Khilafah kwa kufanya amali za kifikra na kisiasa kama vile kujihusisha kwa wingi katika maeneo ya umma kwa kutoa vipeperushi na visimamo pamoja na kuandaa makongamano ya mtandaoni.

Hizb ut-Tahrir pia inawakumbusha maafisa waaminifu katika jeshi kuhusu wajibu wao wa Shariah wa kutoa nussrah (msaada wa kimada) ili kusimamisha tena Khilafah kama vile Swahaba mkubwa Sa'd bin Muadh (ra), mkuu wa kabila la Ansari, alivyotoa nussrah, katika kusimamisha dola ya kwanza ya Kiislamu mjini Madina. Ili kuukomboa Umma wa Kiislamu kutoka katika makucha ya ukoloni, Hizb ut Tahrir imekuwa ikifichua njama za Marekani-Uingereza na washirika wao wa kieneo katika siasa na uchumi wetu. Kwa ujasiri na ikhlasi, imekuwa ikifichua mipango miovu ya nchi hizi za kikoloni na ushirikiano wa mawakala wao kuhusiana na ubwana wa Umma na jeshi lake. Makongamano mbalimbali ya mtandaoni yaliyoandaliwa na Hizb ut Tahrir yalipokelewa vyema na watu wa matabaka mbalimbali na yalikuwa watu walikuwa wakishiriki pakubwa. Hapo awali kupitia kongamano la mtandaoni lililoandaliwa mwaka wa 2015 liliopewa kichwa “Khilafah Inayokaribia – Mabadiliko Yasiyoepukika katika Siasa na Uchumi wa Bangladesh”, wazungumzaji walitoa maelekezo muhimu kwa taifa kuhusu jinsi Dola ijayo ya Khilafah italeta mabadiliko katika siasa na uchumi wa nchi. Kisha mwaka wa 2019, wazungumzaji katika kongamano la kiuchumi la mtandaoni lililoitwa “Ruwaza ya Kiuchumi ya Dola ya Khilafah,” walifichua sera danganyifu za 'maendeleo' za serikali ya Hasina na kuainisha sera na matendo muhimu ya Dola ya Khilafah. Mnamo mwaka 2020, rasimu ya katiba ya Dola ya Khilafah iliwasilishwa kwa umma kupitia Kongamano la mtandaoni uliopewa jina la “Rasimu ya Katiba ya Dola ya Khilafah” kwa madhumuni kwamba Hizb ut Tahrir imeshatayarisha rasimu ya katiba ya Dola ya Khilafah yenye ibara 191 zinazotokana na Quran na Sunnah, ambayo kwayo hizb iko tayari kikamilifu kusimamia masuala ya Khilafah Rashida ya pili inayokaribia. Mbali na hayo, mwezi Machi 2022, wazungumzaji kwenye kongamano la mtandaoni lenye kichwa “Je, kweli Tuko Huru?” lilifichua uingiliaji wa wazi wa dola za kikoloni hususan Marekani-Uingereza, katika nyanja zote za siasa na uchumi wa nchi hii, na kutoa mwanga juu ya njia ya kupata uhuru wa kweli na ukombozi kutokana na minyororo ya ukoloni mamboleo. Enyi watu, je! Makongamano haya ni vitendo vya uanamgambo kwa kile ambacho ATU ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari ikiwaita wazungumzaji wa kongamano kuwa ni wanamgambo na kutafuta usaidizi wa umma ili kuwakamata? Kitengo hiki kiovu cha kigaidi cha serikali ya Hasina hakikuwasaza hata ndugu zetu wawili waliosoma tu Qur'an tu kwenye makongamano haya kutokana na uzushi huu.

Kwa kupuuza udhalimu na umwagaji damu wa utawala wa sasa, wanachama wa Hizb ut Tahrir waliokuwa wazungumzaji katika makongamano haya ya mtandaoni bila shaka ni watoto wa Ummah wenye ikhlasi na shupavu. Kwa ujasiri wao, wazungumzaji hawa wananyanyaswa kila mara na tabaka tawala na kuvumilia mateso yasiyokwisha ikiwemo kupoteza riziki. Licha ya haya, nafsi hizi shupavu zinatekeleza kwa nguvu kazi ya kuchunga mambo ya Ummah. Ni watu hawa wajasiri ndio wanaocheza dori ya watawala wa kweli, wanaofanya kazi ya kuwakomboa watu kutoka kwa mnyororo wa wakoloni na kuregesha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu kupitia kusimamisha tena Khilafah iliyoahidiwa. Kwa sababu wanaichukulia siasa (siyasah) kuwa ni ibada tukufu na wajibu wa Shariah. Mwenyezi Mungu Subhanahu Wa Ta’ala asema,

(كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ)

“Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu.” [Surah Al Imran:110]. Kwa upande mwingine, watawala vibaraka wa nchi hii wanatumia sera zote chafu za wakoloni wa makafiri ili kuzuia mwamko wa Uislamu kwa kuutangaza Uislamu kuwa ni ugaidi au uanamgambo na kuziita amali za kimpangilio na kifikra za kusimamishwa Khilafah kuwa ni misimamo mikali na uanamgambo. Baada ya kushindwa kuisitisha Hizb ut Tahrir kupitia ukandamizaji wa kudumu, ukamataji na kufungwa mara kwa mara, serikali ya Hasina sasa inatamani kabisa kukomesha harakati za Hizb ut Tahrir kwa kutafuta kile kinachoitwa kuungwa mkono na wananchi ili kuwakabidhi wazungumzaji wa hizb wa makongamano ya mtandaoni kwa polisi.

Enyi Waislamu, wale mnaofanya kazi katika polisi na vyombo vya sheria, msiwaache watawala madhalimu wawanyonye ili kutekeleza njama zao fisadi za kisiasa. Tunakuiteni muwaasi hawa wapotovu ambao wametelekeza sheria za Mwenyezi Mungu (swt) na kujisalimisha kwa matakwa ya dola za kikoloni za Kikafiri. Mtume (saw) amesema: «لَا طَاعَةَ لِمَخْلُوقٍ فِي مَعْصِيَةِ الْخَالِقِ» “Hakuna utiifu kwa kiumbe katika mambo kumuasi Muumba (Mwenyezi Mungu”. Utiifu ni wajibu katika yaliyo mema pekee” (Al-Bukhari).

Enyi Ndugu! Wanachama wa Hizb ut-Tahrir wameichagua njia hii ya mapambano na kujitolea mhanga kwa ajili ya kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu (swt) na wanajikinga Kwake (swt) kutokana na wale wanaojaribu kuwadhuru. Jihadharini na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, Enyi Ndugu! Mwenyezi Mungu Al-Muntaqim Al-Jabbar anasema katika Wahyi wa uhakika:

(إِنَّ الَّذِينَ فَتَنُوا الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ ثُمَّ لَمْ يَتُوبُوا فَلَهُمْ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَلَهُمْ عَذَابُ الْحَرِيقِ)

“Hakika walio wafitini Waumini wanaume na Waumini wanawake, kisha hawakutubu, basi watapata adhabu ya Jahannamu na watapata adhabu ya kuungua.” [Surah Al Burooj: 10].

Jiepusheni na kuwakamata, kuwatesa, au hata kuwanyanyasa viongozi na wanaharakati wanaolingania Uislamu na mfumo wa utawala wa Mwenyezi Mungu - Khilafah. Watawala hawa wasaliti ni vibaraka wa mabwana zao wa Magharibi ambao wako katika vita na Uislamu kwa jina la "vita dhidi ya ugaidi" yaani, "vita dhidi ya Uislamu" ili kung'oa mapambano ya kifikra na kisiasa yanayoendelea nchini Bangladesh na Hizb ut Tahrir. Tayari watu wameshawakataa vibaraka hawa wakandamizaji wa kimagharibi ambao wamefeli kabisa kuhakikisha haki, usalama na ustawi. Watoto wa kiume na mabinti wanyofu wa Umma huu mtukufu wanaunga mkono kwa moyo wote na kusubiri kwa hamu kusimamishwa tena kwa Khilafah. Tunakutahadharisheni kwamba, mkiingia katikati ili kuchelewesha utabikishaji wa Hukmu ya Mwenyezi Mungu (swt), bila shaka mtapata laana ya watu wanaodhulumiwa hapa duniani, na Mwenyezi Mungu (swt) atakuhisabuni kwa vitendo vyenu. Na siku hiyo watawala wenu hawatakuja kukuokoeni kwani watakukaneni. Mtaungua ndani ya moto wa majuto kabla hamjatupwa kifudifudi kwenye moto wa Jahannam. Mwenyezi Mungu Subhanahu Wa Ta’ala asema:

(إِذْ تَبَرَّأَ الَّذِينَ اتُّبِعُواْ مِنَ الَّذِينَ اتَّبَعُواْ وَرَأَوُاْ الْعَذَابَ وَتَقَطَّعَتْ بِهِمُ الأَسْبَابُ * وَقَالَ الَّذِينَ اتَّبَعُواْ لَوْ أَنَّ لَنَا كَرَّةً فَنَتَبَرَّأَ مِنْهُمْ كَمَا تَبَرَّؤُواْ مِنَّا كَذَلِكَ يُرِيهِمُ اللّهُ أَعْمَالَهُمْ حَسَرَاتٍ عَلَيْهِمْ وَمَا هُم بِخَارِجِينَ مِنَ النَّارِ)

“Walio fuatwa watakapo wakataa wale walio wafuata, na hali ya kuwa wamekwisha iona adhabu; na yatakatika mafungamano yao. Na watasema wale walio fuata: Laiti tungeweza kurudi tukawakataa wao kama wanavyo tukataa sisi! Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu atakavyo waonyesha vitendo vyao kuwa majuto yao; wala hawatakuwa wenye kutoka Motoni.” [Al-Baqarah 166-167].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu