Ijumaa, 24 Rajab 1446 | 2025/01/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  10 Jumada I 1444 Na: 1444 H / 12
M.  Jumapili, 04 Disemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kutii Maagizo ya IMF ya Kuongeza Bei ya Mafuta ni kwa ajili tu ya Kudumisha Uhai wa Utawala wa Fisadi wa Hasina pekee, lakini ni Kujiua kwa Uchumi wetu

(Imetafsiriwa)

Katikati ya mateso ya wananchi kutokana na kupanda kwa bei ya bidhaa muhimu na kuzorotesha uzalishaji viwandani kutokana na tatizo la umeme, serikali ya Hasina danganyifu imeamua kuongeza bei ya umeme kwa asilimia 19.92 hadi Tk6.20 kWh kutoka bei ya awali ya Tk5.17 kWh. kwa kutii agizo la Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF). Ingawa serikali yake iliwahakikishia wananchi wiki chache zilizopita kwamba bei ya umeme katika kiwango cha reja reja haitaongezeka na kuwataka wananchi wasiwe na wasiwasi. Si hivyo tu, serikali imepokonya mamlaka ya kuongeza bei ya mafuta, gesi na umeme bila kusikilizwa na wananchi kwa kupitisha sheria kwenye baraza la mawaziri (Govt wrests control of energy pricing, The Daily Star, 29 November, 2022). Kwa hivyo, serikali ya Hasina inajisalimisha kwa chombo cha kikoloni cha Magharibi, IMF, kwa dolari bilioni 4.5 kwa gharama ya watu jumla na nchi. Mikopo hii midogo kutoka kwa IMF-Benki ya Dunia haitasaidia kukabiliana na upungufu wa akiba kwa sababu mahitaji ya kila mwezi ya Bangladesh ya kufadhili uagizaji nje ni zaidi ya dolari bilioni 7 na, zaidi ya hayo, italazimika kulipa dolari bilioni 20 mwaka ujao kama malipo ya deni la nje ikiwemo riba. Kwa hakika, alikimbilia IMF ili kuzuia kuanguka kwake kusikoepukika kutokana na uporaji mkubwa na usimamizi mbovu wa kifedha kwa kuwa na 'cheti cha maadili mema' kutoka IMF. Cheti hiki kitasaidia kupata mikopo zaidi ya nje na miradi mikubwa zaidi ya Benki ya Dunia (WB), ADB, IDB, JICA, nk. ambayo itahakikisha kuwepo kwa utawala wake mbovu. Na kwa masharti magumu yanayojulikana sana ikiwa ni pamoja na mamlaka ya ubinafsishaji na huria, IMF/WB inataka kuchukua udhibiti zaidi juu ya uchumi wetu na kuhakikisha kwamba Mabepari wa ndani tu na Wakoloni wa Magharibi US-UK-EU na washirika wao ndio wanaovuna manufaa ya maagizo ya IMF. Inafahamika kuwa nchi hizi za kibepari za kimagharibi zilinyonya nchi nyingi zenye rasilimali na kuwafukarisha watu wao kwa chombo chao cha ukoloni mamboleo, IMF-WB. Wakoloni wa makafiri waliivamia Iraq na kupora rasilimali zake za mafuta kupitia vita haramu vilivyowagharimu pesa nyingi. Kwa hivyo sasa wananyonya nchi zenye rasilimali nyingi kama Bangladesh na watawala wao vibaraka kama Hasina ndani ya sera za IMF-WB za Kibepari. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alituonya kuhusu kuporwa rasilimali zetu na wakoloni makafiri. Akasema (saw):

«يُوشِكُ أَنْ تَدَاعَى عَلَيْكُمُ الْأُمَمُ كَمَا تَدَاعَى الْقَوْمُ إِلَى قَصْعَتِهِمْ»

“Hivi karibuni watu wataitana wao kwa wao ili kuwashambulia kama watu wanavyoitana kuishambulia sahani ya chakula...” (Sunan Abi Dawud).

Enyi Watu, kwa hakika tumenaswa katika mgogoro ambao sio tu wa kiuchumi bali ni tatizo la kisiasa linalohusiana kihalisi na mfumo mbovu wa Kirasilimali. Kutokana na kukithiri kwa ufisadi na usimamizi mbovu wa watawala wa kisekula na kufuata sera za kirasilimali za kimagharibi zilizolazimishwa na maagizo ya IMF/WB uchumi na fedha zetu zinaelekea kuporomoka. IMF/WB inafadhili ufisadi kama huo kwa kujua maslahi ya ukoloni mamboleo. Sasa tunahitaji sana ruwaza mbadala ya kisiasa. Ni mabadiliko ya kina tu kwa mfumo wa kisiasa uliopo ndio suluhisho pekee la mgogoro huu wa kudumu. Kwa hiyo, ni lazima tukatae taasisi hii ya ukoloni mamboleo na mamlaka yake ya mageuzi maovu ambayo yananyakua mamlaka yetu ya kiuchumi. Njia pekee ya kwenda mbele kwetu ni kuanzisha mfumo mpya wa kisiasa chini ya Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Huu ndio mradi halisi wa mwamko ambao kupitia kwao tutaweza kuizuia Magharibi mkolono kafiri isituchukulie kama sahani yao ya chakula na kuulinda Ummah na rasilimali zake dhidi ya ulafi wa Mabepari-Wakoloni.

Mwenyezi Mungu (swt) asema katika Quran, (إِنَّ اللَّهَ لَا يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّى يُغَيِّرُوا۟ مَا بِأَنفُسِهِمْ)  “Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo nafsini mwao.” [Surah Ar-Ra’d 13:11].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu