Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Iraq

H.  17 Dhu al-Qi'dah 1443 Na: 1443 / 06
M.  Alhamisi, 16 Juni 2022

Taarifa Kwa Vyombo vya Habari

Iraq: Kutoka kwenye Kizingiti cha Kisiasa Hadi kwenye Mporomoko wa Kisiasa
(Imetafsiriwa)

Baada ya mapambano, ushindani na mizozo kwa zaidi ya miezi 7, kiongozi wa vuguvugu la Sadri, Muqtada al-Sadr, alitangaza kujiuzulu kwa wabunge wa kambi yake kubwa zaidi ya bunge katika bunge la Iraq, ambao idadi yao ni 73, dhidi ya msingi wa mwendelezo wa Mfumo wa Uratibu - unaojumuisha vikosi vya kisiasa vya Kishia vilevile - na kuzuia uundaji wa serikali ya kitaifa ya wengi kabla ya hapo.

Ahmed Al-Mutairi, mkuu wa chombo cha kisiasa cha vuguvugu la Sadri, alisema katika taarifa iliyopokelewa na Shirika la Habari la Shafak: "Kujitolea muhanga kisiasa ambako Muqtada al-Sadr alikufanya kwa kujiondoa katika mchakato wa kisiasa na kuviacha viti vya wawakilishi wake kwa wapinzani wake kutoka kwa wanasiasa wengine ni muhanga kwa ajili ya Iraq, kwani alijifanya kuwa kondoo mtakatifu wa Ismail.”

Al-Sadr alisema katika mkutano mmoja na manaibu wa kambi ya Sadri, uliofanyika mnamo Jumatano, 15/6/2022, mjini Al-Hanana katika jimbo la Najaf: "Niliamua kujiondoa katika mchakato wa kisiasa ili nisishiriki kwa namna yoyote ile na mafisadi." Aliongeza, "Iwapo mafisadi watashiriki katika uchaguzi ujao, sitashiriki ndani yake."

Kwa uamuzi huu, na baada ya Spika wa Baraza la Wawakilishi kuidhinisha kujiuzulu huko, nchi iliingia katika machafuko mapya ya kisiasa, na mbele ya madukuduku yote ambayo hayatumikii masilahi ya mwananchi wa Iraq, kinyume chake, mnyonge tu ndio hulipia gharama yake.

Hivyo, athari zake ni zipi? Na madukuduku haya ni yapi?

Kwanza: Kiongozi wa vuguvugu la Sadri, Muqtada al-Sadr, anajulikana kuwa na hali tete, na historia yake imejaa hilo. Alitangaza kikao katika Zoni ya Kijani mnamo tarehe 27/3/2016 ili kumshinikiza al-Abadi katika kuunda kwake baraza la mawaziri, na kisha akavunja kikao chake mnamo Machi 31 baada ya al-Abadi kuwasilisha muundo wake mpya wa baraza la mawaziri ambao sio tofauti na lile la awali, na akatangaza kususia uchaguzi mwaka 2013, kisha akatengua hilo, hii ni sawa na 2021 alipobatilisha uamuzi wake vilevile. Mtu kama huyo mwenye utata, asiye wa kimfumo ni vigumu kumtabiri na kuwa na yakini kwa maamuzi yake, na kubaki thabiti juu yake. Anaweza kurudi nyuma na kuingia katika mchakato wa kisiasa baada ya mazungumzo, na anaweza kuridhika na mafanikio fulani, hii ni mandhari ya kwanza.

Pili: Kuegemea kwa kiongozi wa Harakati ya Sadri katika kushindwa kwa Mfumo wa Uratibu kuunda serikali, na kisha bunge kujivunja lenyewe, na serikali ya Al-Kazemi kubakia, na kwenda kwenye uchaguzi mwingine wa mapema, ambapo Muqtada al-Sadr anatamani kushinda viti ambao kwao kambi ya tatu inaondolewa, hii ni mandhari ya pili.

Tatu: Mafanikio ya Muundo katika kuunda serikali, na hili ni gumu bila ya baraka za vuguvugu la Sadri, kwa sababu wanatambua uwezo wa vuguvugu la Sadri kutembea mitaani, na kiwango cha kutoridhika kwa mitaa ya Iraq, na kutokubali kwao miundo hii iliyokataliwa. Mandhari hii ndiyo hatari zaidi, kwani inaweza kuipeleka nchi katika machafuko na mapigano makubwa, ambayo moto wake huwaunguza watu wasio na hatia kabla ya wahalifu na mafisadi.

Enyi Waislamu wa Iraq: Tangu Iraq ilipokaliwa kimabavu mwaka 2003, na mateso na matatizo yaliyofuata ambayo yameenea nyanja zote za maisha, na kila mnapokuwa karibu na wokovu, mvamizi anawashangaza kwa mchezo mpya miongoni mwa michezo yake. Katika kila duru ya uchaguzi, mnatangaza lawama na majuto yenu, kwamba mlidanganywa na kwamba hamtapiga kura tena baada ya hapo. Kisha mvamizi huleta kamba zake ambazo anawavuta tena, ili mutii kamba yake na mushiriki kwa hiari! Kamba ya madhehebu, kamba ya utaifa, kamba ya walio na nguvu zaidi, na kamba ya watu huru, zote ni za uongo na mitego, ambayo madhumuni yake ni kufanikisha uchaguzi na kuuokoa mchakato wa kisiasa ulioundwa na mvamizi Marekani kutokana na kuporomoka. Haya ndiyo mliyoyapitia katika uhalisia. Hali ya nchi tangu kukaliwa kwake kimabavu hadi sasa imekuwa mbaya zaidi, na kila mzunguko mbaya unapopita, mzunguko mbaya zaidi hufuata.

Enyi Waislamu wa Iraq: Jueni kwa hakika kwamba hakuna mwanasiasa anayewajali, iwe anadai uzalendo, madhehebu au uhuru. Kila mtu anafanya kazi tu kwa ajili ya maslahi yake binafsi na ya chama chake, na kuridhika kwa mabwana wake wa kikoloni pekee. Hali mnazoishi nazo leo, ni thibitisho bora la hili. Kwa zaidi ya miezi 7 kwa ajili ya uchaguzi wao wa mapema kwa mujibu wa madai yao, kila mtu amejikita katika kufikia maslahi yake, huku akivuruga maslahi ya wananchi wote kwa kisingizio cha kupitisha bajeti ambayo haijapitishwa hadi baada ya kuundwa kwa serikali.

Wokovu kutokana na mateso yote haya, na kupatikana kwa maisha ya starehe, si kwa kukusanyika pambizoni mwa As-Sadr, au muundo wake, wala pambizoni mwa mgombezi chama, au wa kibinafsi. Kwani vyote hivi ni vidubwasha kwenye mchezo wa chesi vilivyoundwa na mvamizi, anavyeviendesha namna anavyotaka, wote hao wanatangaza kufuata katiba iliyowekwa na mvamizi huyu, ambayo ndiyo shina la ugonjwa na chanzo cha mateso. Hii ndio hali ya kimaumbile ya Ummah unapopotoka kutoka katika Shariah. Unakuwa dhaifu na mataifa huitana kuushambulia na kuupora rasilimali zake, na mafisadi huzunguka ndani yake na Ruwayibidah (wajinga) huliamua mambo yao.

Ni wajibu wenu kuubadilisha kimsingi mfumo mzima wa kisiasa uliopo, kuutupilia mbali mchakato wa kisiasa na watu wake, kusimamisha mfumo wa kisiasa ambao katiba yake inatokana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu (swt) na Sunnah ya Mtume Wake (saw), kutoa ba’yah kwa mtawala kuitabikisha na kumhesabu ipasavyo. Hapo ndipo mtakapoondolewa katika ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na duara la hasara na ugumu wa maisha hadi kwenye radhi za Mwenyezi Mungu (swt) na mzunguko wa uongofu, na maisha ya furaha.

Basi, kunjeni mashati yenu na fanyeni kazi kwa bidii ili kuondosha dhulma kutoka shingoni mwenu na mutii maneno ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw):

«إِنَّ النَّاسَ إِذَا رَأَوُا الظَّالِمَ فَلَمْ يَأْخُذُوا عَلَى يَدَيْهِ أَوْشَكَ أَنْ يَعُمَّهُمْ اللَّهُ بِعِقَابٍ مِنْهُ»

“Pindi watu watakapomuona dhalimu na wasimzuie mikono yake, Mwenyezi Mungu atakaribia kuwachanganya wote kwa adhabu itokayo kwake.”

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Iraq

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Iraq
Address & Website
Tel: 
E-Mail: hutiraq@yahoo.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu