Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 431
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Kashmir inaashiria wazo la Pakistan. Wazo la Pakistan lilikuwa juu ya kukataa kusalimu amri kwa Mabaniani, kupitia kuasisi jamii inayotawaliwa na Uislamu.
“Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa Watu wa Kitabu nao wameamini ingeli kuwa bora kwao. Wapo miongoni mwao waumini, lakini wengi wao wapotovu.”
Januari 6 mwaka huu mwili wa Edwin Chiloba mwenye umri wa miaka 24 mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Eldoret, ulipatikana ndani ya sanduku ukiwa umeshindiliwa vitambara mdomoni na puani mwake. Kifo chake kimezuwa gumzo ndani na nje ya nchi haswa katika vyombo vya habari na katika mitandao ya kijamii kwa sababu Chiloba ni mtetezi wa LGBTQ+
Wizara ya Wanawake na Watoto ilitangaza matokeo ya ripoti ya takwimu juu ya arifa za hali zilizo hatarini za watoto na kuwatishia watoto kwa sheria ya miaka 2020 na 2021, iliyowakilishwa na uzinduzi wa jukwaa la ulinzi wa watoto ambalo hutoa uwezekano wa arifa ndogo
Ripoti ya habari ya CNN siku 5 baada ya tetemeko la ardhi la Uturuki kuonya juu ya maafa makubwa zaidi nje ya kuporomoka kwa awali kwa miundombinu katika maeneo yanayopakana na Syria.
Tangu kuvunjwa kwa Khilafah mwaka 1924, kila kona ya dunia imekuwa katika machafuko ya kuendelea. Hii ni licha ya kuwa kumekuwa na maendeleo katika teknolojia, matibabu, kilimo, jeshi, na inaonekana maendeleo katika siasa na katika kujenga haki sawa kati ya jinsi na jinsia.
Hali chungu ya Waislamu na maisha yao duni katika sehemu zote za ardhi haifichiki kwa mtu yeyote. Popote unapogeuza macho yako, utaona mataifa yanayopigana dhidi yao na nchi zao na uwezo wao, na watawala wao wahalifu wanawatawala, na utaona vita, umaskini, njaa, ukosefu wa usalama na vikwazo juu yao katika kutekeleza ibada zao na kushikamana na ibada za dini yao.
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Sudan ukiongozwa na Ustadh Abdul-Azim Issa- Mwanachama wa Hizb ut Tahrir, ukifuatana na Ustadh Bilal Ali - Mwanachama wa Hizb ut Tahrir, na Issam Yusuf, na Abdullah Mahjoub, ambao ni waungaji mkono wa hizb, walikutana katika ziara ya kwanza mnamo Jumapili tarehe 12/02/2023 na Brigedia Jenerali Sir Al-Khatam Ahmad Othman - Mkurugenzi wa Polisi wa Forodha wa Wadi Halfa.
Mapema mwezi huu wa Februari 2023, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alisema kuwa serikali yake inachunguza akaunti ya benki ya nje iliyoko nchini China ambako zimefichwa fedha zilizokusanywa kutokana na ‘Makubaliano ya Kukiri Makosa’ (Plea bargain).