Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  18 Rabi' II 1442 Na: HTS 1442 / 34
M.  Alhamisi, 03 Disemba 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Khiyana ya Viongozi wa Serikali ya Mpito Inaendelea katika Faili ya Usawazishaji Mahusiano na Umbile la Kiyahudi!

(Imetafsiriwa)

Gazeti la The New York Times la Amerika lilifichua kuwa mipango inafanywa katika Ikulu ya White House ya kutiwa saini kwa makubaliano ya amani kati ya Sudan na umbile la Kiyahudi mnamo Disemba hii, baada ya Bunge la Amerika kupitisha uamuzi wa kuliondoa jina la Sudan kwenye orodha ya ugaidi. Ili al-Burhan kufinika usaliti wake, aliitaka Congress ipitishe Sheria ya Kinga ya Kiongozi, na mazungumzo haya yalikuwa ni suala la kutupa majivu machoni, kwani gazeti hilo hilo lilithibitisha kuwa yaliyomo kwenye mazungumzo ya simu kati ya al-Burhan na Pompeo yalizungumzia mipango ya hafla ya kutia saini.

Watawala wa Sudan wametufanya tumezoea kukubaliana na kujadiliana katika kadhia nyeti za Umma, pamoja na Amerika ambayo ina ujuzi wa kutoa masharti na maelezo ili zaidi kufikia ajenda na maslahi yake, kwa hivyo ni vipi mtawala wa Kiislamu anaweza kukubali kuchafuliwa kwa matukufu na kuhatarisha usalama wa nchi yake kwa sharti la kupitisha sheria ambayo inaweza kubadilishwa na kugeuzwa kulingana na mhemko na matamanio ya wanasiasa wa Amerika?! Sheria za Amerika zinaweza kubadilika, Amerika ni dola la kikoloni la kirasilimali, na haidhuruki ikiwa itavunja ahadi zake na kuvunja mzunguko wake. Ilikiuka ahadi nyingi mno na Al-Bashir hadi ikamtupa gerezani kwa fedheha. Kadiri Al-Bashir anavyofanya uhalifu na usaliti, iliwatafuta wengine kando naye. Na hii hapa tena inafanya maudhui yale yele na kumlazimisha juu ya usawazishaji mahusiano na umbile la Kiyahudi kwa badali ya kuliondoa jina la Sudan kutoka kwa orodha yake nyeusi.

Amerika imekuwa ikifanya usaliti na serikali hizi za vibaraka, kwani ilikuwa ikiunganisha kuondolewa kwa jina la Sudan kwenye orodha hiyo na kujitengwa kwa kusini, kisha kwa uchungaji wa vijidola vyake chipuzi ambavyo vilianzisha kusini, na kisha kuilazimisha serikali ya Bashir kushiriki katika vita vichafu vya Amerika ulimwenguni dhidi ya Uislamu na watu wake kwa jina la vita juu ya kile kinachoitwa (ugaidi) ..

Halafu Amerika ilimtaka al-Bashir abadilishe kanuni kadhaa zilizojengwa juu ya msingi wa Sharia, na serikali ya mpito ilipokuja, serikali ya Amerika iliagiza kwamba Sudan ilipe dolari milioni 70 fidia kwa familia za wahasiriwa wa bomu la Cole, na $335 milioni kwa familia za wahanga wa balozi za Washington nchini Kenya na Tanzania. Na pindi serikali ya mpito ilipojisalimisha, Amerika iliiamrisha usawazishaji wa mahusiano na umbile la Kiyahudi maadui ambao wameiteka nyara ardhi ya Israa na Mi'raj, na wakati wowote serikali hizi ndogo zinapojisalimisha, mate ya Amerika hutiririka katika kutoa masharti ya ziada ya kidhalimu, hii hapa tena inaahidi na inawataka watoe kinga kutoka kwa Bunge la Amerika kama badali ya kuwasilisha usawazishaji wa mahusiano na umbile chipuzi la Kiyahudi. Mwenyezi alisema:

يَعِدُهُمْ وَيُمَنِّيهِمْ وَمَا يَعِدُهُمُ الشَّيْطَانُ إِلَّا غُرُوراً﴿

“Anawaahidi na anawatia tamaa. Na Shet'ani hawaahidi ila udanganyifu.” [Surah An-Nisaa: 120].

Hakika sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan daima tumekuwa tukionya dhidi ya serikali hizi za hila ambazo zinaungana na maadui katika kuuza nchi na kuwadhalilisha waja, na uhalisia umethibitisha kuwa hakuna izza na hakuna dola itakayo kata mkono wa maadui wenye ulafi isipokuwa dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo ni ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt) na bishara njema ya Mtume Wake (saw), Mwenyezi Mungu (swt) asema:

وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُم فِي الأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْناً﴿.

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao.” [An-Nur: 55].

Ibrahim Uthman (Abu Khalil)

Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu