Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 24 Rabi' II 1442 | Na: 05/ 1442 |
M. Jumatano, 09 Disemba 2020 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Serikali Inaendelea Kudai kuwa Mlinzi wa Haki za Wanawake kwa Jina la Kupambana na Unyanyasaji Dhidi ya Wanawake Bila ya Kujua Sababu Halisi za Unyanyasaji!
(Imetafsiriwa)
Jukwaa la Shirika la Habari la Sudan (SUNA) lilikuwa mwenyeji wa Kitengo cha Kupambana na Unyanyasaji dhidi ya Wanawake na Watoto ili kuzungumza juu ya kampeni ya kupambana na unyanyasaji dhidi ya wanawake na kutangaza uzinduzi wa kampeni ya siku 16 ya kupambana na unyanyasaji na ubaguzi, mbele ya Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Jamii Lena el-Sheikh.
Siku mithili hii ya mwaka uliopita na katika sehemu hiyo hiyo, kampeni iliyotangulia kutajwa hapo juu ilizinduliwa chini ya kauli mbiu: "Pamoja kwa ulinzi endelevu wa wanawake" ili kuboresha hali za wanawake katika Sudan yote, pamoja na uwepo wa Massimo Liana, mwakilishi wa Shirika la Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa nchini Sudan, ambaye aliahidi kujitolea kwa Mfuko huo kwa mipango ya kiraia ya serikali ya kupambana na unyanyasaji dhidi ya wanawake, waziri alisisitiza kuhakiki au kufuta kanuni na sheria ili kuhakikisha amani na usalama kwa wanawake, na kuendeleza juhudi za kuboresha hali za kisiasa, usalama, kijamii na kisheria kwa wanawake, na pia alitangaza kuwasilisha hati ya mageuzi kwa familia.
Jitihada zote hizi zilizofanywa ili kupunguza unyanyasaji dhidi ya wanawake zilifanikiwa kuitia hatiani sheria ya hadhi ya kibinafsi na kila kitu kinachohusiana na vifungu vya Uislamu katika katiba, lakini hawajagusia unyanyasaji halisi wanaopitia wanawake kuanzia mgogoro mkali wa kiuchumi, haswa katika mafuta na mkate, na kushiriki wa wanawake kupiga foleni kwa muda mrefu ili kupata mkate. Ama bei ya juu ya bidhaa nyingi, na ukosefu wa zingine, pamoja na kuzorota kwa huduma zote, pamoja na usafirishaji, afya na elimu kote Sudan, wanawake wengi wamelazimika kufanya kazi katika sekta isiyo rasmi kama wauzaji wa chakula, vinywaji, au bidhaa za kilimo, kwa hivyo wanalazimika kukaa mitaani na sokoni kuanzia asubuhi hadi Saa za usiku huku ushuru ukitozwa kwa kila kitu kinachouzwa na wanawake hawa... Kazi hii bila ya udhibiti wowote wa kisheria imewafanya wanawake wawe katika hatari ya kila aina ya unyanyasaji, kati ya shinikizo la maisha na mgogoro wa hali ya uchumi wa kirasilimali .. Hakuna lakabu nyengine ya wanawake ila unyanyasaji.
Amani na usalama ambayo Waziri aliwaahidi wanawake wakimbizi katika kambi za Darfur katika kampeni ya mwaka uliopita sasa yamepotea, na mateso yakajitokeza; Kuanzia ukosefu wa usalama, unyanyasaji wa kimwili na kingono, kuzuka kwa utapiamlo kati ya wajawazito na akina mama, ukosefu wa huduma za afya na elimu, na wanawake wengi katika eneo la Darfur na kwengineko wanalazimika kufanya kazi za sulubu kama kusafirisha mawe na vifaa vya ujenzi na kukandika matope, na pia kufanya biashara ya rejareja, na vile vile viwanda vya kazi za mikono kama vile kutengeneza mapambo, kamba na vikapu. Mgogoro wa kiuchumi pia ulisababisha kuongezeka kwa bei na malighafi kwa kazi za mikono, na msimu dhaifu wa kilimo kutokana na gharama kubwa ya mbegu. Je! Serikali haioni unyanyasaji wote huu ambao haujawahi kutokea ?!
Hakika serikali ya mpito, ambayo inajibu madai ya makafiri kuhusu wanawake, inapuuza sababu za mateso yao. Inadai kwamba inabeba wasiwasi wao na kumtetea wakati kwa kweli inaweka mikono yao mikononi mwa maadui wa Ummah ili kusababisha unyanyasaji na ukiukaji dhidi ya wanawake, na haifanyi lolote kuondoa sababu halisi za unyanyasaji mkali, unaowakilishwa na hali mbaya ya maisha ambayo Wanawake wanaishi nchini Sudan kama matokeo ya sera za serikali ambazo zinajibu maagizo mabaya ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, na sababu ni kwamba serikali ina vipimo vilevile vya mtazamo wa kirasilimali wa kimagharibi, ambavyo husababisha kutengana kwa familia na wanawake kupoteza maadili na kitambulisho chao wakati wakiendelea kuteseka kutokana na hali wanayoishi.
Serikali ya mpito ilipofushwa na uharibifu wa Magharibi wa familia, wanawake na watoto kutokana na fahamu za unyanyasaji dhidi ya wanawake, kwa hivyo iliuleta ugonjwa kuutibu! Kama Waislamu wanaoamini kuwa Uislamu ndio mfumo pekee unaopanga maisha ya familia kwa ukamilifu, hutatua matatizo yanayotokea kati ya waume na wake kwa hekima na uadilifu, na kuigeuza familia kuwa ngome ambayo inapaswa kulindwa na kuhifadhiwa. Na kwa kutabikisha nidhamu za maisha za Kiislam katika Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, wanawake wataishi kwa hadhi kama kina mama na wake nyumbani, kama heshima ambayo ni lazima ihifadhiwe.
Msemaji Rasmi wa Kike wa Kitengo cha Wanawake katika Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: |