Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  30 Rabi' II 1442 Na: HTS 1442 / 36
M.  Jumanne, 15 Disemba 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Serikali ya Mpito Yaziba Kufeli Kwake na Furaha Kizushi, kwa Uamuzi Usiofaa wa Amerika Ambayo Inalipia Gharama Kubwa kwa Kuupiga Vita Uislamu na Kusawazisha Mahusiano na Umbile la Kiyahudi
(Imetafsiriwa)

Jana, Wizara ya Mambo ya Nje ya Amerika ilitoa taarifa ikisema: (Sudan imefutwa rasmi kama dola mdhamini wa ugaidi ... nk). Halafu shangwe kizushi ilianza kutoka kwa serikali ya mpito, na pande zake mbili, kijeshi pamoja na kiraia, kana kwamba wamepata ushindi mkubwa dhidi ya Amerika! Al-Burhan, kiongozi wa Baraza Kuu, aliandika tweet, akisema: (Uamuzi huu utachangia kusaidia mabadiliko ya kidemokrasia na kuongeza nafasi za kufanikiwa kwa kipindi cha mpito na ustawi wa watu wa Sudan.) Ama Waziri Mkuu Hamdok, alitangaza kwenye Facebook furaha yake na uamuzi huo na kuuelezea kama ukombozi, na kuongeza: (Leo tunarudi na historia yetu yote na ustaarabu wa watu wetu, utukufu wa nchi yetu, na nguvu ya mapinduzi yetu kwa jamii ya kimataifa kama nchi inayopenda amani, na nguvu inayounga mkono utulivu wa kikanda na kimataifa), hii ni pamoja na kugombana na vyombo vya habari vyenye kupotosha.

Furaha hii inayodaiwa na serikali ya mpito na vyombo vyake vya habari vya kupotosha inaonyesha kiwango cha udhalilishaji, fedheha, na kushindwa ambako tumefikia. Nchi zinazoheshimika haziombi, na hazitii wengine, bila kujali nguvu au msimamo wa dola hiyo, na hawatikiswi kwa idhini yao au hasira zao. Dola ya kimfumo ni ile ambayo inaamiliana na wengine kwa njia hiyo hiyo, haijisalimishi kwa vikwazo vinavyo lazimishwa juu yake kisha kufurahi wakati vikwazo hivi vinapoondolewa kutoka kwao, baada ya kuwa wamelipia gharama nzito kwa ajili yake, ambayo ni vita dhidi ya ugaidi (Uislamu), kusawazisha mahusiano na umbile la Kiyahudi ambalo limenyakua ardhi iliyobarikiwa ya Waislamu, na pia kulipwa zaidi ya dolari milioni 300 kwa wale wanaodaiwa kuwa wahanga wa vitendo vya Osama bin Laden ... Lakini tuko katika zama za watawala Ruwaibidha (wajinga), wanaofanana na dola!

Na ikiwa tutafikia uamuzi huo huo wa Amerika, ambao ulileta furaha hii ya kizushi, ni uamuzi usiokamilika, na hauiondoi Sudan, kama wanavyodai, kutoka kwa orodha nyeusi maadamu Bunge la Congress la Amerika halikutoa kinga dhidi ya mashtaka ya kisheria katika siku zijazo wakati wowote, kama familia za wahasiriwa wa matukio ya Septemba 11 zitasisitiza kudai fidia ya hadi dolari bilioni 4! Kwa hivyo ni uamuzi uliobadilishwa, na hauna maana kisheria.

Hakika sisi tunaona kwamba kasi hii ni uamuzi ambao haujakamilika kisheria na una makosa, ambayo serikali ilikusudia kufinika kufeli kwake katika nyanja anuwai za maisha, na kuangazia kwake maandamano ya Jumamosi 19 Desemba 2020, ambayo inayaogopa, kwani siku hii ina umuhimu wake wa kimapinduzi, kwani chanzo cha cheche ya mapinduzi ilikuwa Disemba yaliyompindua Bashir mnamo Aprili 2019.

Sisi katika Hizb ut-Tahrir / Wilayah ya Sudan, tunaonya Ummah, na kuutahadharisha kwamba usiingie katika mitego ya uhadaifu kwamba uamuzi huu wa Amerika utaunda maisha mazuri, kwa sababu maisha yenye heshima yatakuwa tu chini ya kivuli cha hukmu za Mwenyezi Mungu (swt), ambazo Khilafah Rashida ya Pili kwa njia ya Utume itazitabikisha, ambayo yatupasa sote kufanya kazi kwa ajili yake, ili tuweze kutoka katika udhalilifu na fedheha tulizomo ndani yake.

]يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [TMQ 8:24]

Ibrahim Uthman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu